Kwa mshahara wa Benchika ni ngumu kusajili wachezaji wazuri

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Mpaka sasa tumeshuhudia sajili mbalimbali kwa baadhi ya timu za ligi kuu ya NBC na baadhi ya wachezaji kuwaona kwenye michuano ya mapinduzi wengi wao viwango vyao nivya kawaida kabisa.

Simba nao wamefanya usajili kwa baadhi ya wachezaji wa kimataifa huku wengi wao wakiwa ni wachezaji huru tumeshuhudia kiwango cha Sarr wao wanamwita kiungo fundi mkata umeme ila binafsi sijaona tofauti yake kubwa na Sawadogo.

Sarr hajakidhi viwango vya wanasimba, uzuri wa wanasimba wanapendea kusikia maneno ya dizaini ya Mane ametwambia Sarr ni mali au Etoo ametwambia Onana ni mali nop football haipo hivi siku hizi hapo inaonyesha udhaifu kwenye upande wa scouting.

Kwanini Simba imekua na shida kusajili wachezaji wa bei kubwa au hata kuvunja mikataba ishu ni hii kumchukua Benchika kama kocha wao.

Ukweli kumtoa benchika pale Algeria na kumleta Tanzania ni pesa kubwa imetumika kutokana na profile kubwa ya kocha mwenyewe, mshahara anaolipwa benchika pamoja na wasaidizi wake ni mkubwa tambua jamaa amekuja na watu wake kocha wa viungo na msaidizi wake.

Simba walimsajili Benchika wakiwa na pressure kubwa, Simba walimsajili Benchika kupunguza moto wa mashabiki wao baada ya kupokea zile tano kutoka kwa Yanga kwa kifupi walifanya ghafla bin vupu.

Simba walimsajili Benchika bila kusajili wachezaji wapya wakiamini atakuja na miujiza hapana bila wachezaji wazuri hakuna kocha mzuri.

Tambua mwekezaji wa Simba ni mfanyabiashara pesa yake inamuuma sana baada ya kufanya usajili wa pesa nyingi kwa kocha tusitegemee Simba itasajili mchezaji wa bei ghali mpunga mwingi unatumika kulipa Benchi la ufundi ni ngumu tajiri kumwaga mpunga wake mwingi tena.

Kumbe Simba waendelee kuvumilia tu wataendelea kuwatumia wachezaji hawahawa na sio ajabu wakaanza kumtafutia visa Benchika aondoke na kumleta kocha wa bei rahisi.

Wazee...
 
Mpaka sasa tumeshuhudia sajili mbalimbali kwa baadhi ya timu za ligi kuu ya NBC na baadhi ya wachezaji kuwaona kwenye michuano ya mapinduzi wengi wao viwango vyao nivya kawaida kabisa...
Madini tupu...
 
Kuna faida gani ya kusajili kocha bora na kumletea wachezaji wa kawaida?

Kocha sio mtenda miujiza. Siwezi hukumu usajili kwa dirisha dogo moja kwa moja, ni ngumu sana kuvunja mikataba ya wachezaji.

Endapo ataendelea, basi nangoja kuona dirisha kubwa la usajili kipi kitafanyika.
 
Kuna faida gani ya kusajili kocha bora na kumletea wachezaji wa kawaida?

Kocha sio mtenda miujiza. Siwezi hukumu usajili kwa dirisha dogo moja kwa moja, ni ngumu sana kuvunja mikataba ya wachezaji.

Endapo ataendelea, basi nangoja kuona dirisha kubwa la usajili kipi kitafanyika.
Unauliza swali na kujijibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kundi la Simba likiongozwa na mbwa Vs kundi la mbwa likiongozwa na Simba.
 
Eti tajiri mo pesa inamuuma, Sheria zinasema wawekezaji wasipungue 3 yeye kinachomfanya awe peke take ni Nini, Yale matengazo ya kampuni zake ningapi?
 
Back
Top Bottom