Kijiweni leo: kwanini hakuna wazee wenye majina ya kelvin?

Kijiweni leo: kwanini hakuna wazee wenye majina ya kelvin?

Youbettersleep

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2019
Posts
944
Reaction score
1,628
Habari tena!
Leo kijiweni mzee mjuaji sana (Kamugisha) alikuja na jibu baada ya kuulizwa jana kuwa kwanini hawajawahi kusikia Mzee yeyote anaitwa KELVIN.

SABABU!
Baada ya mzee kufikiria akaja na jibu kuwa, jina la KELVIN lilikuja Tanzania miaka ya 90's hivyo lilianza kutumika kuanzia mikoa ya Mwanza na Dar na akasema kuwa wenye umri mkubwa kwasasa wana 35 kwasababu hiyo hadi sasa KELVIN wengi bado ni vijana.

Tutegemee kupata wazee wenye majina ya KELVIN ifikapo mwaka 2040 - 2060.

Mmeridhika na UTAFWITI???
 
Wazee wenye hayo majina wapo lakini katika jamii zetu mwanaume akifikisha miaka 50 na kuendelea huitwa Kwa jina la mwisho (la ukoo) kwahiyo inakuwa ngumu kujua jina la awali. Katika mfumo huohuo wazee wenye majina hayo nao hawajulikani
 
Nina miaka 28 lakini jina la mwisho ndo maarufu
Wazee wenye hayo majina wapo lakini katika jamii zetu mwanaume akifikisha miaka 50 na kuendelea huitwa Kwa jina la mwisho (la ukoo) kwahiyo inakuwa ngumu kujua jina la awali. Katika mfumo huohuo wazee wenye majina hayo nao hawajulikani
 
Sijaona mtanzania anaitwa MURPHY OR MURPHIE lakini nimeonA EDDIE OR EDDY
 
Back
Top Bottom