Kijijini tu

Mokoyo

JF-Expert Member
Mar 2, 2010
15,145
5,553
Haya yanapatikana Kijijini tu
1. Wanafaunzi wa shule kumpokea mgeni anapokuwa kwenye maeneo ya shule kwa heshima na taadhima na kupelekwa moja kwa moja kwa headteacher
2. Watoto kusimama wanapopita watu waliowazid umri na kuwaamkia kwa heshima na kusubiri wapiti ndio wakae
3. Ndiko ambako hakuna siasa za matope
4. Ndiko ambako bado wlimu wanaheshimika na kupewa heshima ya wataalamu tofauti na hapa mjini
5. Ndiko ambako Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere anatambulika na kuendelea kukiuza chama tawala kwa kasi ya juu sana
6. Ndiko ambako vocha zinauzwa 1,100; 2,200; 5,200 n.k
7. Ndiko ambako maana ya ndoa na heshima ya ndoa bado ipo juu sana
8. Ndiko ambako watoto wanaenda shule pasipo kuwa na viatu wala kandambili
9. Ndiko ambako kuna wimbi la wawekezaji kwenye Ardhi ya vijiji
10. Ndiko magazeti yanapatikana kila baada ya au zaidi ya wiki moja
 
............pia ndio mahala maji ya kunywa hayachemshwi lakini watu wanadunda kwa kwenda mbele................!!!
 
Nakumbuka nilipokuwa nasoma shule ya msingi kiloleli, massanza kona, pale magu mkoani mwanza, nilikuwa ndiye mwanafunzi pekee niliyekuwa navaa viatu.
Mwalimu alikuwa ananiambia nivue viatu ili nichapwe fimbo za kwenye nyayo.
 
unyayo wako ulikuwa mlaini kama viganja vya mikono ndio maana teachers waliona uko ndiko pouwa pa kuweka mboko
 
Haya yanapatikana Kijijini tu
1. Wanafaunzi wa shule kumpokea mgeni anapokuwa kwenye maeneo ya shule kwa heshima na taadhima na kupelekwa moja kwa moja kwa headteacher
2. Watoto kusimama wanapopita watu waliowazid umri na kuwaamkia kwa heshima na kusubiri wapiti ndio wakae
3. Ndiko ambako hakuna siasa za matope
4. Ndiko ambako bado wlimu wanaheshimika na kupewa heshima ya wataalamu tofauti na hapa mjini
5. Ndiko ambako Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere anatambulika na kuendelea kukiuza chama tawala kwa kasi ya juu sana
6. Ndiko ambako vocha zinauzwa 1,100; 2,200; 5,200 n.k
7. Ndiko ambako maana ya ndoa na heshima ya ndoa bado ipo juu sana
8. Ndiko ambako watoto wanaenda shule pasipo kuwa na viatu wala kandambili
9. Ndiko ambako kuna wimbi la wawekezaji kwenye Ardhi ya vijiji
10. Ndiko magazeti yanapatikana kila baada ya au zaidi ya wiki moja

.......SI KWELI labda kwenu!!!

11.Ndiko ambapo bado wanakijiji wanafanya kazi za pamoja
mf. kusafisha barabara,mifereji nk
 
Ndiko bado ambako maambukizi ya ukimwi yanashika kasi; kwani mondoc inaonekana ni anasa!
 
Mkuu, sio zinaonekana ni anasa....ni kwamba hazipatikani, labda kama Mwenge wa uhuru utakuwa unalala kwenye kijiji hicho ndo mwenyekiti wa kijiji anapewa maagizo ahakikishe kondom zinapatikana kwenye ofisi za kijiji.

Issue ni kwamba,
-dispensary pekee iliyopo ni ya kanisa.....hawaweki condom
-maduka matatu au manen yaliyopo hawauzi condom, ya mzee Macha, Kisambeke and Kasiamaka, wote ni waumini wa kanisa katoliki na wanaheshimika kijijini.......how gross it is kuuza condom.

Lakini ukumbuke watu wana pigana kipara kama kawa, ndom hamna, je waache ku do? wanaweza kuwa kama bht na wakina dark city......wasafi wa moyo na mwili?

bht na dark city hilo ni pande tu kwa misimamo yenu isiyotikisika japo undani mnaujua nyie peke yenu
 
Ndiko bado ambako maambukizi ya ukimwi yanashika kasi; kwani mondoc inaonekana ni anasa!

Si wanaotoka town wakifika uku wanaonekana wametoka kwenye mipesa na wametakata kwahiyo wanagawa kwa kwenda forward

Halafu usiandike mondoc andika CONDOM, unaficha kitu gani wewe bwana
 
..Ndiko Sehemu ambapo Condom zinaazimwa baada ya matumizi ili na mwingine akatumie...
 
Hizi data bado ni valid kweli kwa vijiji vya sasa? Halafu inategemeana kijiji na kijiji kuna viji vina kila kitu tofauti ulivyolist hapo. Siasa za matope nenda vijiji vya kyela huko utaona
 
wewe una akili na unaijua nchi yako
 
Ndio mahala pekee watu wanaposhirikiana pasipo unafiki wala kudai fidia kwa mfano kwenye misiba, sherehe, chakula na mengineyo ukiondoa yale yasiyo na utu
 
Pia
-ndipo mahali pekee ambapo baadhi ya watu wangali wanajua Nyerere bado rais wa tz
- Ndipo mahali pekee ambapo kuku na mayai ni muhimu kupelekwa kwa mwalimu .
- Ndipo pekee ambapo wakati mwingine inbidi uende mbali sana kutafuta kichaka cha kujisaidia
- Pekee penye vifo kama kugongwa na nyoka,kuliwa na simba/chui
- mahali pekee ambapo mbuzi na binadamu waweza lala chumba kimoja
- unaweza kufanya kazi mwaka mnzima usilipwe mshahara= kilimo mvua isiponyesha
 
ili kuwa vijiji vya zamani sasa hivi thubutu akuna hayo tena kabisa
 
Pia
-ndipo mahali pekee ambapo baadhi ya watu wangali wanajua Nyerere bado rais wa tz
- Ndipo mahali pekee ambapo kuku na mayai ni muhimu kupelekwa kwa mwalimu .
- Ndipo pekee ambapo wakati mwingine inbidi uende mbali sana kutafuta kichaka cha kujisaidia
- Pekee penye vifo kama kugongwa na nyoka,kuliwa na simba/chui
- mahali pekee ambapo mbuzi na binadamu waweza lala chumba kimoja
- unaweza kufanya kazi mwaka mnzima usilipwe mshahara= kilimo mvua isiponyesha

labda kijijini kwenu kwetu hayapo hayo kabisa
 
Back
Top Bottom