Kijijini tu

Mkuu, sio zinaonekana ni anasa....ni kwamba hazipatikani, labda kama Mwenge wa uhuru utakuwa unalala kwenye kijiji hicho ndo mwenyekiti wa kijiji anapewa maagizo ahakikishe kondom zinapatikana kwenye ofisi za kijiji.

Issue ni kwamba,
-dispensary pekee iliyopo ni ya kanisa.....hawaweki condom
-maduka matatu au manen yaliyopo hawauzi condom, ya mzee Macha, Kisambeke and Kasiamaka, wote ni waumini wa kanisa katoliki na wanaheshimika kijijini.......how gross it is kuuza condom.

Lakini ukumbuke watu wana pigana kipara kama kawa, ndom hamna, je waache ku do? wanaweza kuwa kama bht na wakina dark city......wasafi wa moyo na mwili?

bht na dark city hilo ni pande tu kwa misimamo yenu isiyotikisika japo undani mnaujua nyie peke yenu

mweee B ina maana sie malaika eeeh????
 
Ndiko bado ambako maambukizi ya ukimwi yanashika kasi; kwani mondoc inaonekana ni anasa!

Kwnye baadhi ya vijiji wanajua hiyo zana inaweza kutumika zaidi ya mara moja, so unafua na kuanika then twende kazi.

11. Ndiko ambako unaweza kuzunguka mwezi mzima ukitafuta chenchi elfu kumi (10,000)
 
Kwnye baadhi ya vijiji wanajua hiyo zana inaweza kutumika zaidi ya mara moja, so unafua na kuanika then twende kazi.
Kweli,

11. Ndiko ambako unaweza kuzunguka mwezi mzima ukitafuta chenchi elfu kumi (10,000)
Na mtu akipata hii elfu kumi anakaa nayo kama wiki hivi akiitazama kutokana na kutoiona kama miezi kadhaa hivi. Very serious kabisa
 
Ndiko kuna wazee wa kutosha na wenye busara ukipeleka shauri lako mara moja linatatuliwa
 
Ndiko ambako mtu anaweza kuvizia kwa jirani chakula kiive akale
Ndiko ambako mtu anaweza kwenda kwa jirani yake na kuomba chumvi maana kwake imemwishia
Ndiko ambako watu wanakula "natural food" n.k
 
....ndiko wajawazito wanalazimika kutembea kilometa za kutosha kufuata huduma ktk hospitali za wilaya.
...ndiko takrima za fulana, khanga, pilau, pombe, pesa n.k hutolewa kwa wingi wakati wa uchaguzi.
..ndiko miundombinu ni hafifu au mibovu kabisa.
..ndiko mazao yanaozea ghalani kwa kukosa soko la uhakika na kama soko lipo basi bei ni ya kumkandamiza mkulima
...ndiko teknolojia ya habari na mawasiliano mf. internet bado ni ndoto.
...ndiko mgeni toka mjini anapoandamwa na kuombwa chochote (hasa pesa)
 
umekumbushwa wapi uko GS?

Eti alikwenda kijijini kwao na noti za mia tano na buku zenye thaman ya laki2 ili atatue tatizo la kuombwa hela na kitu mtu..
Kweli kijiji ndui nyingi sana
 
Eti alikwenda kijijini kwao na noti za mia tano na buku zenye thaman ya laki2 ili atatue tatizo la kuombwa hela na kitu mtu..
Hii mbinu wanaitumia wengi sana kwani ukija kijijini na buku kumi au tanoi tano tu utaishiwa ndani ya siku mbili za ugeni wako pale na hasa kama ni kijijini kwako ambako kitambo hujafika na unajulikana kuwa unaishi DSM
 
1.kijijini ndio sehemu ukitongoza binti anajiuma uma kidole au anaanza kuchora ramani chini kwa dole gumba la mguu
 
Back
Top Bottom