Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,136
- 871,458

Katika pitapita zangu leo nikakumbana na hiyo picha hapo juu ambayo ilinikumbusha kijiji cha Mjimpya, Muheza Tanga.
Nilipita hapo kwa mara ya kwanza mwaka 1994 ni kijiji kipo katikati ya mji wa Muheza na Kicheba mkoani Tanga.
Ni kijiji kisafi mno ambacho naamini kinaweza kuchukua no moja kitaifa na kimataifa kwa swala zima la usafi japo nyumba nyingi ni za makuti na misonge miti na matope.
Unapopita hapo kijiji urefu wa kilometer moja kasoro huwezi kutema hata mate jinsi barabara inavyowaka kwa usafi pamoja na kuwa kuna miembe minazi na michungwa pembezoni mwa barabara miti ambayo inadondosha majani mara kwa mara.
Mitaa michache ya kijiji hiki nayo ni misafi kupindukia nyumba ziko kwenye mistari iliyonyooka mashamba yamepaliliwa hasa mazao makubwa yakiwa ni mahindi maharagwe migoho huku kukiwa na miti ya michungwa miembe dodo na minazi.
Shida moja ya kijiji cha Mjimpya ni kwamba kila kitu kilikuwa na hirizi kuanzia binadamu mimea mazao wanyama mpaka miti.
Kwa macho yangu nilishuhudia paka,mbuzi, tetea, bata mimea ya maharagwe,mahindi na miti ya matunda mbalimbali vikiwa na hirizi vimevalishwa.
Kijiji cha Mjimpya ndio kilikuwa na kiwango kidogo kabisa cha uhalifu na migogoro ya ardhi.
Hapa ndipo palinipa hamu na mshawasha wa kujifunza hii sayansi ambayo kumbe ikitumika vizuri inaweza kuleta matokeo chanya.

