Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amefanya ziara kijiji cha Msula kata ya Misughaa kukagua miradi minee ya maendeleo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,886
938
MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu, Januari 13 2023,amefanya ziara kijiji cha Msula Kata ya Misughaa na kukagua miradi minne ya maendeleo inayotekelezwa kwenye kijiji hicho.

Katika ziara hiyo aliyoambatana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ikungi Ikimbia Khangaa na viongozi wa chama na serikali wa kijiji cha Msule,amekagua mradi wa ujenzi wa barabara Misughaa-Msule-Sambaru yenye urefu wa kilomita 27, ujenzi wa Zahanati ya Msule, mradi wa usambazaji wa Umeme na mradi wa maji.

Akizungumza mara baada ya kukagua miradi hiyo Mtaturu ameishukuru na kuipongeza serikali kwa jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo.

Amesema katika mradi wa barabara unaogharimu Sh Bilioni 1.1 kwa sasa umefikia asilimia 85 na kwamba kazi ilikuwa kufungua barabara na kujenga madaraja ambapo eneo la Misughaa-Msule imekamilika na sasa mkandarasi anaendelea na kazi eneo la Msule-Sambaru.

"Katika mradi wa ujenzi wa zahanati ya Msule wananchi walihamasika kuibua na kuanzisha ujenzi huu na serikali ilipoona jitihada hizo imewaunga mkono kwa kuleta Sh Milioni 50 ambapo ujenzi umefikia asilimia 75 na kinachoendelea ni umaliziaji wa kufunga madirisha,milango,kuweka marumaru na kupiga rangi,"amesema.

Mtaturu amesema katika mradi wa usambazaji wa Umeme nguzo zinaendelea kusimikwa kwenye vitongoji ili nyaya zisambazwe na hatimaye transfoma ifungwe ili wananchi wapate huduma.

Amebainisha kuwa upande wa mradi wa Maji tayari kisima kirefu kimechimbwa kinachotosheleza kijiji kizima na hatua inayofuata ni kutafuta fedha ili kujenga miundombinu.

"Kiukweli wana Singida Mashariki tuishukuru sana serikali,kila tukitembea tunaona kazi nzuri inayoendelea kufanyika katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma,kweli tunaposema CCM imetimia kazi iendelee tunamaanisha kweli Ilani ya Uchaguzi ya CCM inatekelezwa,"amesisitiza.

Ziara ya Mtaturu ni muendelezo wa utaratibu aliojiwekea wa kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi kabla ya kuhudhuria vikao vya bunge na baada ya kumalizika kwa vikao vya bunge ili kutoa fursa kwa wananchi kubainisha changamoto zao na yeye kupata wasaa wa kutoa mrejesho wa masuala yaliyojadiliwa bungeni yanayohusu jimbo hilo.

IMG-20230114-WA0034.jpg
IMG-20230114-WA0041.jpg
IMG-20230114-WA0039.jpg


#SingidaMashariki#TumedhariaMaendeleoYanayoonekanaKusemaNaKutenda#KaziIendelee#
 
Nafurahi sana kuona wananchi wakichangia maendeleo yao kwani sio kila kitu kusubiri tu
Charities nyingi wangefungua
 
Back
Top Bottom