Kijana wa mtaani asiye na kazi anakutaka kimapenzi...

Ni kama vile mtu mfupi anavyotumia nguvu na sauti kubwa kuonyesha kwamba mimi nipo.......Ili asifunikwe na warefu yani.
Ahii staki kabisa....Practically ni ngumu bwana.
Ngoja waje wenyewe waombe uthibitisho hapo shauria yako dada LD
 
  • Thanks
Reactions: LD
Ngoja waje wenyewe waombe uthibitisho hapo shauria yako dada LD

Kuhusu watu wafupi anavyosema LD ni kweli si kwenye mahusiano tu hata kwenye pilika za kawaida za maisha tu huwa wana complication kwa kutaka recognition kwenye jamii
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: LD
Dah hulka ya mwanaume wa kiafrika sijui hao wengine lakini wakiafrika ni kuwa juu ya mwanamke, kutambuliwa nafasi yake, kuheshimiwa ikibidi kuabudiwa kabisa.....ndio walivyo kwa asili ni wachache sana labda kutokana na malezi labda au kupondeka moyo tu wanaweza wasiyatamani hayo. Kwa hiyo ikiwa kuna kitu ambacho anahisi/ona kwa hili huyu mwanamke anaoneka yuko juu yangu which can be true atajitahidi kutunisha misuli ya ziada ili mradi tu uitambue nafasi yake.

Ni kama vile mtu mfupi anavyotumia nguvu na sauti kubwa kuonyesha kwamba mimi nipo.......Ili asifunikwe na warefu yani.
Ahii staki kabisa....Practically ni ngumu bwana.

Nadhani kwenye mahusiano mwanaume anatakiwa ajiamini hata kama kielimu yupo chini lakini pia kama hana future plan ndio kabisa confidence inapungua, nawashangaa hata mwanaume mwenye diploma nae hajiamini kwa mwenye shahada wakati hapa kama atajipanga vizuri na yeye atakuwa na shahada ikiwezekana na zaidi. Kinachotakiwa mwanaume ajiamini, awe future oriented na akili ya maisha in addition awe tayari kujiendeleza.

Ila kuna wanaume wengine nao ni mzigo maana umeishia form four unakuta future yake mwenyewe haijui hapa sidhani hata mwanamke alieishia form four kama yeye sidhani kama atakubali kujenga maisha nae hasa ukizingatia hata mababu zetu sifa za mwanaume ziliangaliwa kwenye uwezo wa kufanya kazi za kijamii na kiuchumi kama kulima, kuwinda na busara ambapo kwa kizazi cha mjini cha sasa ndio elimu, kujituma na akili za maisha kwa ujumla (akiwa navyo viwili at least)
 
  • Thanks
Reactions: LD
Nadhani kwenye mahusiano mwanaume anatakiwa ajiamini hata kama kielimu yupo chini lakini pia kama hana future plan ndio kabisa confidence inapungua, nawashangaa hata mwanaume mwenye diploma nae hajiamini kwa mwenye shahada wakati hapa kama atajipanga vizuri na yeye atakuwa na shahada ikiwezekana na zaidi. Kinachotakiwa mwanaume ajiamini, awe future oriented na akili ya maisha in addition awe tayari kujiendeleza.

Ndio hivyo....wanaume wanataka hata mkikaa Sebuleni inasomwa taarifa ya habari pale wote mnaona lakini angependa wewe umuulize kasema je eti....au sasa ndio nini hivyo wanamaanisha...basi akuelezee paleeee ndio furaha yake. Sio we uanze ooh unajua Ndugai shenzi kabisa kamstopisha Sugu leo bwana..unaanza kuelezea weee......atakupotezea.

Ila we anza hivi umemuona Leo Ndugai Bungeni alivyomuambia Sugu? Hapo muache akuelezee kama aliona/sikia na maswali muulize akujibu. hapo sasa dah life linakwenda.

Ohh eti umepita JF leo wakati hata Intenet hajui ni nini....na ikiwa amepita utasikia kwa nini? Kuna ile habari hivi hivi...muachie yeye aseme Ni mambo ya ajabu sana nchi hii.....kama pale hivi hivi...afu wewe hata ulichokielewa unakileta kama swali, sasa kama wamesema hivi, walikuwa na maana gani? Muachie ajibu....

NDO HULKA YA WANAUME hiyoo...we ukijifanya unajua anakupotezea tu au ukimbishia anakuambia Ina maana unaona mi kenge sikuelewa pale au?
 
Kazi ipo kuondoa huu mfumo dume nadhani pia kuna haja wanaume nao wawe wanaandaliwa kisaikolojia kabla ya kuingia kwenye ndoa maana mwanamke wa sasa wengi huandaliwa japokuwa kwa siku moja lakini anapewa ABC za namna ya kum-handle mwanaume lakini kwa wanaume imekuwa business as usual unaingia hivyohivyo based on experience yako ya kijiweni na the way baba yako alivyokuwa anaishi. Nadhani ifike mahala wanaume na sisi tuambiwe nini mwanamke anapenda kufanyiwa na nini hapendi vinginevyo migogoro mingine ukiingalia haina msingi na watu hawaaminiani kwani hisia zaidi ndio zinawatuma vibaya na sio hali halisi.
 
  • Thanks
Reactions: LD
Mtu anaweza akawa na kazi na kisomo chake ila akawa hana malengo. Ni bora kuwa na mtu ambae hajapata kazi bado ila anaeonyesha uchakarikaji, malengo na anaefikiria mbali. That way unajua atafika tu anapotaka kufika muda utakapofika.

Binafsi sisemi tu kwamba naweza kuwa kwenye mahusiano na mtu asiye na kazi ila nimeshajaribu na Mungu sio Athumani muda ulipofika alipata kazi yake ya maana kabisa. Sasa hivi ungekuta namwangalia kwa mbaaaali na kutamani anitokee tena kwakua 'amekidhi vigezo' vya kileo.
 
Mimi kwa kweli naamini katika mapenzi, utu na uelewa wa kawaida kuhusu maisha, I do not care about formal education. Nina experience katika hili; nilidate kijana aliyeishia form four wakati huo mimi nina master. Nilienjoy coz he was so loving na wakati ananipenda hakujua nina elimu wala kazi gani, aliniona ni mtu wa mtaani tu.Ila nikiri pamoja na kwamba aliishia form four, ana akili sana za maisha. Imagine, alijifunza udereva, akafanya kazi kwa watu, akanunua gari yake akaifanya taxi bubu na pia akawa anaikodisha, pia alifanya biashara mbalimbali ndogondogo. So to me he was a right person kumdate, he has a potential in life sio zoba.Tulikuja kuachana maana tulishindwana kwenye mambo fulani ambayo siwezi kusema yanatokana na elimu yake ndogo. Nawaencourage wadada wenzangu wasiignore boys because of low education, consider them jamani, they can be good and give the love and happiness you need.Mimi kweli ningempata mwingine kama yule namkubali tu!!
 
mmmmmmmmmmmmh Mtambuzi upooo??

kama nimeelewa vizuri, inaonekana unaogopa kuchezewa na lengo lako ni ndoa bila kuangalia kiasi cha mapenzi ulichonacho kwa mwanaume. Je hakuna wa level yako anayetaka kukuoa?
Kama unampenda huyo mvulana kikwelikweli na unauhakika kuwa anakupenda kweli mkubalie akuoe,hatokuwa hana shughuli ya kufanya kilasiku, siku moja atapata.
Lakini kama unachotaka ni ndoa tu na wewe uwe umeolewa, basi fahamu kuwa utamnyanyasa na utam-treat kama mtoto mdogo, na yeye atatoa malalamiko hayohayo ambayo wadau wameshaeleza. Mapenzi sio maigizo hautaweza ku-act kila siku, utachemsha tuu.
 
Last edited by a moderator:
Sio rahisi wivu wa kitoto ulimzidi.halafu bwana tukubalitu ukweli kwamba mwanaume anatakiwa awe juu au muwe at per vinginevyo utavuliwa nguo.unless mimi ndo nimekuwa na bahati mbaya ya kukutana na rafiki wanonyanyasika na waume zao wasio na elimu.siku moja toka party ya office mara boss mam mtu mzima kaangusha kilio kisa mume wake "miundombinu"a.k.a marioo kampigia simu na kumwaga mitusi eti anadate a staff wenzake.mifano mingi mingi mingi ni wachache sana waelewa.tena labda awe na mipesa asiwe na elimu huyu anaweza kuwa na afadhali
 
hawajui mapenzi,kwao mapenzi ni ngono tu ...yaani madikodiko ya mapenzi wao hawaelewi ..
mimi huko siruki kabisa....
 
Back
Top Bottom