Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Kelvin Muriuki alikuwa bora katika shule yake katika mtihani wa mwisho wa shule za msingi, lakini umasikini ukamlazimu kufanya kazi katika timbo, familia yake imesema
Muungano huo wa maafisa wa zamani wa jeshi la angani ulijitolea kumlipia Karo na kumsafirisha kwa ndege hadi katika shule yake mpya
Sasa ndoto ya Kelvin imefufuka na anataka kuwa rubani
Muungano huo umesema kuwa utamlipia Karo Kelvin za dola 530 kila mwaka hadi atakapomaliza shule ya upili 2020
Aliwasili katika shule yake mpya mjini Karicheni huko mkoa wa kati baada ya kupewa usafiri wa ndege hiyo iliyochukua dakika 20 kutoka shule anayotoka, kulingana na ripota wa BBC Abdinoor Aden katika mji mkuu wa Nairobi.