Kijana usiogope kuandika Wosia, kuuandika si uchuro kwako, lolote laweza Tokea

Mimi la mke wa pili kurithi siafikiani nalo ..! Hivi inakuwaje usote na mke wa kwanza na labda alikukuta huna kitu na sasa mnamali nyingi tu .. Kumpa mke wa pili si uonevu?
 
Habari za vijana na wazee

Kuna Kuna dhana moja ambayo imejengeka kwetu vijana ambao tuna umri chini ya miaka 50 kwamba ukiandika Wosia umejitabiria kifo hapana lolote laweza tokea,

HIVI NI NANI ANAPASWA KUANDIKA WOSIA??

Kijana yeyote anayemiliki Chochote kihalali anapaswa kuandika wosia ili ikitokea Jambo Mali alizoacha ziwe salama,

Uandishi wa wosia
Mwandishi wa wosia hupaswa kuwa na mashahidi wawili au Zaid wakati wa kuandika wosia ule, na mashahidi wasiwe miongoni mwa warithi,

Warithi hawapaswi kujua wosia unazungumzia nini ni Kwa sababu zifuatazo
1. Usalama wa aliyeandika wosia ule maana akiwa na warithi wakatili na waroho wanaweza kumuondoa mapema ili wakalie alichoandika wao kumiliki

2. Usalama baina ya warithi , kwasababu ni vema warithi wasijua Nani atarithi nini na wapi

3. Misingi na hekima za familia, kuna watu kuanza kutoheshimu kabisa wazazi kisa ameshajua kapewa kidogo au kaambulia patupu,

Wosia hutunzwa wapi?

1.Wosia Kwa zamani ulitunzwa Kwa wazee wa ukoo ambao ni wasiri mnoo , lakin ambao wana hekima si rahisi kuwarubuni

2. Bank
Wosia siku hizi hutunzwa bank Kwa usalama Zaid
3. Mahakama

Wosia pia hutunzwa mahakamani Kwa usalama Zaid na kuepuka kubadirissha ,

Mambo muhimu ya kuzingatia

1. Hakikisha kila mwaka unarekebisha wosia wako maana
A .unaweza kuwa na Mali zilizoongeze
B. Unaweza kuwa na Mali zikizopungua
C. Unaweza kuwa na mtu aliyeongezeka kwenye familia
Mtoto au mke WA pili
D. Unaweza kuwa kuna mtu kapungua, kama taraka au kifo Kwa mwanàfamilia
E.mahusiano na mtoto kupungua au kuongezeka pia usababisha kubadilisha wosia

2. Hakikisha unapobadili wosia wa mwanzo ueleze kwenye unaofuata kwamba maamuzi yaliyobadirika ni Kwa sababu ya kutengua maamuzi ya awali Kwa sababu ya ili na ili

Jiulize maswali muhim

1. Una hela mpesa
2. Una hela bank
3. Una kiwanja
4. Una kigari kidogo
5. Una unaowadai

Lakin hakuna nduguyo hata mmoja anayejua unayemdai wala account ulizo nazo je umetenda haki??

Jamani tuandikeni wosia maana wengi wanakufa kwenye ajali wakiwa wadogo

Wanao na mkeo watakavyotolewa kwenye nyumba na ndugu uliojiaminisha hawawezi kufanya hiyo,wosia nimhimu sana watakaozulumiwa ni mkeo na wanao sasa kwa nini uachie shida?
 
Wanao na mkeo watakavyotolewa kwenye nyumba na ndugu uliojiaminisha hawawezi kufanya hiyo,wosia nimhimu sana watakaozulumiwa ni mkeo na wanao sasa kwa nini uachie shida?
Kabisa wosia ni muhim mnoo
 
Mimi la mke wa pili kurithi siafikiani nalo ..! Hivi inakuwaje usote na mke wa kwanza na labda alikukuta huna kitu na sasa mnamali nyingi tu .. Kumpa mke wa pili si uonevu?
Kama wa kwanza mmetarakiana
 
Patamu hapo.! Hapo sasa sheria itaamua mmekaa muda gani , watoto na mengineyo ..Ngoja wajuzi waje watusaidie hili maana hata Mimi huwa linaniweka njia panda.
Sawa Ila sasa wanawake nao hawatulii
 
Dini inafundisha uandike ili kupunguza mtafaruku.
sio kwa dunia ya sasa.uandike usiandike watu watapanga ya kwao.
Mimi ni muhanga Wa wosia.
mwisho Wa Sikh mzee alivyokufa.wakafanya vya kufanya.
SINTOKUJA KUANDIKA WOSIA.
 
sio kwa dunia ya sasa.uandike usiandike watu watapanga ya kwao.
Mimi ni muhanga Wa wosia.
mwisho Wa Sikh mzee alivyokufa.wakafanya vya kufanya.
SINTOKUJA KUANDIKA WOSIA.
Kaka inaelekea wosia wa mzee haukuwa wa kisheria, laiti ungetambulika kisheria basi sheria ingewazuia kwenda kinyume na wasia halali.
 
Mimi la mke wa pili kurithi siafikiani nalo ..! Hivi inakuwaje usote na mke wa kwanza na labda alikukuta huna kitu na sasa mnamali nyingi tu .. Kumpa mke wa pili si uonevu?
Dada wacha kuumiza roho yako, uislam unazingatia hayo yote, ngoja nikijaaliwa nitamwona mjuzi wa mambo ya kisheria katika uislam atufafanulie hili.
 
Kaka inaelekea wosia wa mzee haukuwa wa kisheria, laiti ungetambulika kisheria basi sheria ingewazuia kwenda kinyume na wasia halali.
hahahaa.
DUNIANI HAKUNA HAKI.
uwa sipendi kuanika maisha yangu.Ila nakwambia watu Wa siku hizi hawana utu.
uandike wosia au usiandike watagawana wanavyotaka wenyewe.
na kama unavyojua wosia.
HAUWAHUSU WARITHI WA HALALI.
ndo maana watu waliowekwa kwenye wosia wananyanyasika.
ukiwa na roho nyepesi.
UTAAMUA KUMUACHIA MUNGU.
 
Asisahau kufanya amendments kadhaa za huo wosia maana kuna jamaa alisahau kua amend wosia wake akaachana na mke wa kwanza kisheria alimwachia mke wa kwanza kila kitu, akaoa mwingine ndoa ya kikristo safi kakusanya mali upya sema alisahau kumtoa mke wake wa awali kwenye wosia kimbembe kashafariki bila kumbadilisha mke wa awali watu wanataka kuuana huko acha kabisa
 
hahahaa.
DUNIANI HAKUNA HAKI.
uwa sipendi kuanika maisha yangu.Ila nakwambia watu Wa siku hizi hawana utu.
uandike wosia au usiandike watagawana wanavyotaka wenyewe.
na kama unavyojua wosia.
HAUWAHUSU WARITHI WA HALALI.
ndo maana watu waliowekwa kwenye wosia wananyanyasika.
ukiwa na roho nyepesi.
UTAAMUA KUMUACHIA MUNGU.
Pole sana kaka, kuwa na subra japo subra nayo ni bidhaa adimu mno duniani.
 
sio kwa dunia ya sasa.uandike usiandike watu watapanga ya kwao.
Mimi ni muhanga Wa wosia.
mwisho Wa Sikh mzee alivyokufa.wakafanya vya kufanya.
SINTOKUJA KUANDIKA WOSIA.
Pole we ni.mwenyeji wa.wapi na jina lako nani pole sana aisee
 
Back
Top Bottom