Kijana usiogope kuandika Wosia, kuuandika si uchuro kwako, lolote laweza Tokea

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Habari za vijana na wazee

Kuna Kuna dhana moja ambayo imejengeka kwetu vijana ambao tuna umri chini ya miaka 50 kwamba ukiandika Wosia umejitabiria kifo hapana lolote laweza tokea,

HIVI NI NANI ANAPASWA KUANDIKA WOSIA??

Kijana yeyote anayemiliki Chochote kihalali anapaswa kuandika wosia ili ikitokea Jambo Mali alizoacha ziwe salama,

Uandishi wa wosia
Mwandishi wa wosia hupaswa kuwa na mashahidi wawili au Zaid wakati wa kuandika wosia ule, na mashahidi wasiwe miongoni mwa warithi,

Warithi hawapaswi kujua wosia unazungumzia nini ni Kwa sababu zifuatazo
1. Usalama wa aliyeandika wosia ule maana akiwa na warithi wakatili na waroho wanaweza kumuondoa mapema ili wakalie alichoandika wao kumiliki

2. Usalama baina ya warithi , kwasababu ni vema warithi wasijua Nani atarithi nini na wapi

3. Misingi na hekima za familia, kuna watu kuanza kutoheshimu kabisa wazazi kisa ameshajua kapewa kidogo au kaambulia patupu,


Wosia hutunzwa wapi?

1.Wosia Kwa zamani ulitunzwa Kwa wazee wa ukoo ambao ni wasiri mnoo , lakin ambao wana hekima si rahisi kuwarubuni

2. Bank
Wosia siku hizi hutunzwa bank Kwa usalama Zaid
3. Mahakama

Wosia pia hutunzwa mahakamani Kwa usalama Zaid na kuepuka kubadirissha ,

Mambo muhimu ya kuzingatia

1. Hakikisha kila mwaka unarekebisha wosia wako maana
A .unaweza kuwa na Mali zilizoongeze
B. Unaweza kuwa na Mali zikizopungua
C. Unaweza kuwa na mtu aliyeongezeka kwenye familia
Mtoto au mke WA pili
D. Unaweza kuwa kuna mtu kapungua, kama taraka au kifo Kwa mwanàfamilia
E.mahusiano na mtoto kupungua au kuongezeka pia usababisha kubadilisha wosia

2. Hakikisha unapobadili wosia wa mwanzo ueleze kwenye unaofuata kwamba maamuzi yaliyobadirika ni Kwa sababu ya kutengua maamuzi ya awali Kwa sababu ya ili na ili


Jiulize maswali muhim

1. Una hela mpesa
2. Una hela bank
3. Una kiwanja
4. Una kigari kidogo
5. Una unaowadai

Lakin hakuna nduguyo hata mmoja anayejua unayemdai wala account ulizo nazo je umetenda haki??

Jamani tuandikeni wosia maana wengi wanakufa kwenye ajali wakiwa wadogo
 
Britannica ahsante kwa kutumbusha
Mi nshauandika

1. Bank kiasi nilichonacho japo cha muhimu hi kuandika namba ya Siri ya ATM yako, maana process za hela ya bank kwenda Kwa next of kin huwa process Bora uandike namba umpe, atoe taratibu taratibu Hadi ziishe

2. Na Mali nyingine pia
 
mtaalam Britannica.
kwa kweli Mimi siwezi.
yaani niwarithishe watu kabla sijafa?
HAPANA.
acha nife ndo wagawane.Mimi muislam.
sharia ya miradhi ya kiislam ndo itatumika.
Hahaha duh ukifa leo kuna Mali hazijulikani unazijua wewe
 
mtaalam Britannica.
kwa kweli Mimi siwezi.
yaani niwarithishe watu kabla sijafa?
HAPANA.
acha nife ndo wagawane.Mimi muislam.
sharia ya miradhi ya kiislam ndo itatumika.
Kaka huohuo uislam ndio umehimiza wosia, katika uislam kuna ambavyo tayari vimeshapangwa na sheria kwamba ukifa tu utaratibu uweje, lakini mlango wa wasia ukaachwa wazi kwa kiasi chake, kwa hiyo ndugu yangu mjinga mimi tumia nafasi yako ulopewa na Allah kwa kuandika wasia.
Mfano waweza usia moja ya tatu ya mali yako apewe rafiki yako mpendwa ambaye hali yake kiuchumi si nzuri au ukatoa wakf moja kati ya nyumba zako tatu, na mengi mfano wa hayo.
 
yaani naona kama vile nawatengenezea mazingira ya kuja kufaidi Mali zangu.
wakijua wapo kwenye wosia si wanaweza kuniua?
acha Mimi niondoke.alafu ndo wakawane.
ILA WAKE ZANGU HAWARITHIWI.
Kaka hao hatutawarithi ila tutakuwa tunawahesabia siku za eda zikisha tu! fasta tunaenda kuvuta.
 
Wosia hapana aiseeh kila mtu atafute pesa yake na mali yake.. nitakacho kiacha itakuwa ni assignment kwao kupima akili yao kama wanafaa kirithi nitakachoacha....wakigombana shauli yao mimi nilishakufa zangu
 
Back
Top Bottom