Kijana tambua kuna kushiriki na kushirikishwa....!

MtotoWaMzeeWaSiku

New Member
Jan 2, 2017
3
2
Kijana tambua kuna kushiriki na kushirikishwa Je katika utaratibu wako wa maisha yako ya kila siku ukigawa mawazo na utendaji wako katika % wewe ni mshikriki au mshikishwaji....?

katika muktadha wa maisha yetu hasa sisi vijana nafasi yetu ya kusimama na kusimamia kile tunachofikiri na kuchagua katika vyote tupangavyo kufanya uwa ni ndogo sana hii ya weza kuwa sababu ya kutojitambua,uelewa finyu kwa yale tunayotaka,kutokupewa nafasi ya kuthubutu kwa yale tunayo amini tunaweza.

Na kutoka katika mlolongo huo vijana wengi hujikuta wakiangukia katika pahala pasipo sawa kwakuwa % kubwa ya mambo wafanyayo siyo yale ambayo wanauwezo nayo na sio wao wanao amua kufikia hapo hapa kijana anageuka kuwa MSHIRIKISHWAJI kwa maana yeye siyo upande wa wale wanao amua kufanyika kwa jambo fulani ila ugeuka kuwa mpokeaji wa mawazo na matakwa ya watu wengine USHIRIKI wake unafinywa na kupotezwa katika mitazamo ya wengine, Kazi kwako we kijana jiulize leo katika utaratibu wako wa maisha yako ya kila siku ukigawa mawazo na utendaji wako katika % wewe ni mshikriki au mshikishwaji....?
 
Back
Top Bottom