Kijana mwenye akili za Kizee!

Ehud

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
2,685
337
Wiki iliyopita tarehe 20/01/2011 Waziri mkuu wa Kenya Mh. Raila Odinga alikuwa amekwenda kwao mkoa wa Nyanza kuhudhuria maazimisho ya Miaka 17 tangu kufariki Makamo wa Kwanza wa Jamhuri ya Kenya Marehemu Jaramogi Oginga Odinga.

Siku moja kabla ya maazimisho hayo Rais Mwai Kibaki naye alikuwa huko mkoa wa Rift Valley akiwa mgeni wa Wabunge wapatao 12 toka katika mkoa huo ambao wameunda muungano wao wakishirikiana na Wakikuyu ili kuhakikisha kuwa wanakamata urais wa Kenya hapo mwakani na kumzuia Raila kwa nguvu zote asipate nafasi hiyo kwa madai kuwa ni mzee.

Kwenye maazimisho ya marehemu Jaramogi Waziri Raila alisema "mtu anaweza kujiona kijana lakini kiukweli ana akili za kizee kuliko wazee wenyewe!"

Nimeona nilete hii mada hapa ili wana JF tubadilishane mawazo kwani inaonekana hata sisi tuna tatizo kubwa la kuona tuna viongozi ambao kwa umri wanaonekana vijana lakini kifikra na mawazo ni wazee kuliko Mugabe. Sitataja listi lakini ukweli ni Kuwa kwenye serikali yetu ya sas ya TANZANIA kuna vijana wengi mawaziri lakini hakuna kinachobadilika mambo ni vile vile hadi mtu unadhani bora wazee warudishwe labda kutakuwa na afadhali.
 
Hili limekaa kinyume kinyume. Labda tusaidie unavyoona nawewe?
Mimi naamini kadri umri unavyozidi kuongezeka na hikma huzidi. Hata wazee kama mzee Madiba na Mwl Nyerere.
Pia hutokea kijana akapata kipaji hicho . Kipimo ni matokeo yatavyokua kwenye uongozi au uwamuzi hata mawazo .
Mawazo yangu!.
 
mkuu hmethod..... Raila Odinga ni kichwa.... na hawa jamaa wa KKK wanapoteza muda tu...
 
kwa kweli ngeleja hata mie simuelewi. naona kama kabanwa mno na wenye pesa zao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom