Nimepoteza kaka zangu wawili kwa ukimwi.. Hadi Leo huwa naogopa sana kuhusu huu ugonjwa.. Nakumbuka kaka yangu alivyofariki kwa huu ugonjwa mwaka 2010 nikiwa form four nililia sana. Acheni Jamani mambo ni hatari sana kuhusu huu ugonjwa.. Hapa ninapoandika Kuna kaka zangu tena wawili wanaishi na maambukizi ya ukimwi.. Tumebaki wawili tuu ambao tupo safe.. Kila nikiona habari za Ukimwi nasononeka nawakumbuka kaka zangu waliotangulia mbele za haki pia mawazo yananijia kuhusu Hawa kaka zangu wanaoishi na maambukizi ya ukimwi. Inauma sana yaani ndugu zangu acha kabisa omba yasikukute maana sisi tuliobaki ndo tumekuwa walezi wa watoto walioachwa.
Onyo.. Mungu akikujalia Hali nzuri ya maisha itumie vizuri kwa sifa na utukufu wake Usije ukamkufuru mungu. Mungu akikutelekeza utapata pigo la maisha.. Hawa ndugu zangu waliofariki walikuwa na maisha mazuri sana kipindi sisi tupo wadogo ila walikosa hekima ya kutumia Mali zao badala yake wakaendekeza anasa.. Yaani Mimi hapa nilipo naogopa kweli ukimwi.
Sent using
Jamii Forums mobile app