Kijana Ben

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,742
215,933
Habari za Ijumaa wapenzi,

Leo nimekumbuka kisa kilichomtokea kijana Ben jamani maisha haya, Ben alitoka mikoani kuja kusoma chuo mlimani, wazazi wa Ben walikuwa waajiriwa wa serikalini tunaweza kuwaita middle class, hawa kuwa na pesa ya kukufuru lakini mahitaji ya kila siku pesa ya kubadilisha mboga ilikuwepo.

Ben alikuwa na girl friend wake ambea walitoka nae mbali sana aliitwa Flora, yule Flora baada ya kumaliza form four alichaguliwa kujiunga na chuo cha ualimu. Ben alishaweka kuwa she is not a wife material, yeye hawezi kuoa KCC (Kima Cha Chini). Basi akiwa chuo alikutana na mtoto wa professor nae anasoma chuo kwa jina Deborah.

Walidate, lakini dada alikuwa matawi na kwakua Ben hakusoma Dar primary wala secondary, alimuona bwiga flani hivi, lakini hivyo mradi maisha yanakwenda. Mdada ku catch up na wakati alikuwa na chat na marafiki zake wa A-level wanaosoma wengine nje ya nchi, wengine ndiyo wanadate wazungu, mara huyu ameolewa na mkurugenzi gani sijui, basi bwana, Ben kabla hajamaliza shule alipropose kwa Deborah, khe mwana wane, Ben alijisikia mdogo siku ile, aliambiwa wewe ukishanioa utanipeleka wapi? Una nini wewe?

Ben alirudi chumbani kwake alilila sana kwa uchungu, mwisho wa yote alirudi kwao, alikwenda kumpigia goti Flora will you marry me? Flora hakutegemea, alifurahi mno kwakuwa alimpenda Ben kutoka moyoni. Walifunga ndoa na Ben aliapa kumwendeleza Flora. Mwisho wa siku Flora alipata Masters in Education.

Huwezi kujua Mungu alichopanga, kamwe usimdharau mtu hapa duniani.
 
Umenena vema sana mtu wa Mungu ulieandika hii thread. Ungekuwa hapa karibu ningenunua angalau Cocacola tugonge cheazi maana napenda sana watu wenye elimu dunia kama ya kwako
 
Ben kanikera kitu kimoja

Mwanaume unaliaje bhana mambo madogo hayo!!?
Halafu Flora ni bora angesoma MA ya kitu kingine, hiyo MA ya educationa alikuwa ana taka kuja kuwa nani!?

Stori nzuri lakin
 
Ben kanikera kitu kimoja

Mwanaume utaliahe bhana mambo madogo hayo!!?
Halafu Flora ni bora angesoma MA ya kitu kingine, hiyo MA ya educationa alikuwa ana taka kuja kuwa nani!?

Stori nzuri lakin
Head Mistress mkuu na hukawii kupelekwa wazarani au kuwa REO.
 
Napenda the way unavyowasilisha ujumbe wako dada.

Na nashangaa kwanini kila siku ukipotray majina lazima yahusiane na mimi.

Last time was Anna
Today Ben.
 
Back
Top Bottom