Kijana amuua baba yake mzazi kisa ng'ombe

King Octavian

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
403
250
Hili tukio limetokea huko mkoani Rukwa, manispaa ya Sumbawanga, stori inaanza hivi.

Inadaiwa kuwa kijana huyo ambae ni kitinda mimba katika familia ya marehemu, mzee aliyefahamika kama Mzee Kifwema, kijana huyo inasemekana alikuwa ana mgogoro na baba yake huyo akidai kugawiwa mali ambao ni ng'ombe, lakini baba yake alimkatalia, ndipo kijana huyo akawa akimlalamikia mzazi wake huyo hasa kwa madai kuwa kwa sababu gani hataki kumgawa ili hali baba huyo kawagawia ndugu wa kijana huyo ambao ni dada zake walioolewa ili wauze wapate pesa wawalipie watoto wao ada ya shule.

Jambo hilo lilimkasirisha kijana huyo ndipo, siku ya jumapili ya tarehe 25.05.2014 majira ya asubuhi, mzee Kifwema akiwa anaenda zake Kanisani, kijana wake akamvizia barabarani huku ameshika Machette.

Akamzuia baba yake na kukazuka majibizano, namnukuu kutokana na mashuhuda walivyoeleza "" utanipa ng'ombe haunipi?" mzee kajibu "sikupi" ,ndipo kijana kamkata mzee na panga mara tatu tu kichwani na kumfumua ubongo, mzee kakata roho pale pale.

Wananchi wakamvamia kijana na kumpa kipigo hatari sana, hivi tunavyoongea yupo Hospital ya Manispaa amelazwa kutokana na kipigo hicho, na mzazi wake huyo marehemu amezikwa siku ya Jana tarehe 27.

Je? ni lazima mzazi wako akupe mali baada ya kukuleta duniani? kama anazo? au ni ubidamu wake tu kukuwezesha?
 

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
31,259
2,000
Poleni sana wafiwa wote;

Kwani yeye mzee mali alipewa na nani? Si katafuta mwenyewe.

Wakati mwingine hawa watoto ni kama wamerogwa vile;
ni heri mtu uuze mali zako ule pesa yako kidogo kidogo hadi siku
yako ya kuondoka.
 

King Octavian

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
403
250
Poleni sana wafiwa wote;

Kwani yeye mzee mali alipewa na nani? Si katafuta mwenyewe.

Wakati mwingine hawa watoto ni kama wamerogwa vile;
ni heri mtu uuze mali zako ule pesa yako kidogo kidogo hadi siku
yako ya kuondoka.


Dah! ni balaa kijana kadai chake sasa sijui kama atakipata kwa style hii, hapo ndo tayar keshapoteza ukoo mzima sidhani kuna hata kati yao mwenye roho nyepesi atamkaribisha
 

COCKINGTON

JF-Expert Member
Oct 16, 2013
222
0
Mimi natamani kuwa karibu na baba yangu yeye anaua babaye.Hakika huyu ni zaidi ya mwana mpotevu

Kama alihisi kupewa ng'ombe ni rahisi kama kula kipper fillets wa kule ziwani,basi imekula kwake

R.I.P KIFWEMA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom