Kijana Allen Achiles aliyefariki baada ya kupigwa na Polisi azikwa na mamia Mbeya

justin mwanshinga

Senior Member
May 22, 2014
179
619
Usafwani Mbeya.

DZYlR9-XUAAWsao.jpg:large.jpeg

Maelfu ya Vijana mbeya wamsindikiza kwenye makazi ya milele kijana Allen, Ni kijana wa miaka 20 aliyekuwa mfanyabiashara wa machungwa mkoani Mbeya.

Leo March 28, 2018 Mazishi ya Allen Achiles Mapunda (20) aliyefariki March 25, 2018 katika hospitali ya Kanda Rufaa Mbeya na kifo chake kuzua utata yamefanyika katika makaburi ya Iyela jijini Mbeya na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali jiji la Mbeya.

Mwili wa marehemu umepokelewa kutoka hospitali ya Rufaa majira ya saa kumi eneo la Mafiat na kushushwa kwenye gari na kubebwa begani hadi nyumbani kwao huku vijana wakiimba nyimbo za maombolezo.

Akiongoza ibada ya mazishi mchungaji Andrew Kalata wa Kanisa la EAGT Kisima cha Bubujiko lililopo mtaa wa Iyela II amesema maisha ya mwanadamu yanaweza kutoweka muda wowote lakini unapokufa uwe na ushuhuda mzuri kama ulivyo kwa Allen,

“Allen alikuwa ni Shemasi wa Kanisa na mwalimu wa uimbaji na mtoaji mzuri wa sadaka nami nilikula matunda ya biashara yake machungwa “ -Mchungaji Kalata.

Habari zaidi,soma=>Polisi mkoani Mbeya watoa tamko baada ya vurugu kubwa za wananchi wakilituhumu Jeshi hilo kwa kifo cha mtuhumiwa mmoja

MBEYA: Kijana afariki saa chache baada ya kuachiwa kutoka Kituo cha Polisi, yadaiwa alipata kipigo kikali

Mbeya: Serikali kugharamia mazishi ya Alen Achiles aliyefariki baada ya kutoka Polisi
 
RIP Kijana wetu. Polepole Tanzania tunaanza kufanya mazishi ya hamasa kwa style ya wapalestina! Ukiona watu wanapokwenda kuzika wapo kwenye hamasa namna hii ujue makovu hayatafutika kwa waliobaki na wengi wataona ni bora kufa kishujaa kuliko kuishi kiuoga!
Video imenikumbusha mazishi ya palestina. Tofauti hamna jeneza tupu la mhanga atakayefata.
 
Leo March 28, 2018 Mazishi ya Allen Achiles Mapunda (20) aliyefariki March 25, 2018 katika hospitali ya Kanda Rufaa Mbeya na kifo chake kuzua utata yamefanyika katika makaburi ya Iyela jijini Mbeya na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali jiji la Mbeya.

Mwili wa marehemu umepokelewa kutoka hospitali ya Rufaa majira ya saa kumi eneo la Mafiat na kushushwa kwenye gari na kubebwa begani hadi nyumbani kwao huku vijana wakiimba nyimbo za maombolezo.

Akiongoza ibada ya mazishi mchungaji Andrew Kalata wa Kanisa la EAGT Kisima cha Bubujiko lililopo mtaa wa Iyela II amesema maisha ya mwanadamu yanaweza kutoweka muda wowote lakini unapokufa uwe na ushuhuda mzuri kama ulivyo kwa Allen,

“Allen alikuwa ni Shemasi wa Kanisa na mwalimu wa uimbaji na mtoaji mzuri wa sadaka nami nilikula matunda ya biashara yake machungwa “ -Mchungaji Kalata.
 
Kauliwa akiwa kijana mdogo sana inauma sana akwelina na huyu dogo wamefariki wakiwa hawana hatia nchi inaanza kuzoea haya mambo ukiangalia huo msiba waliopo hapo ni vijana wengi wadogo hadi wanawake wamo sasa si ajabu mioyoni mwao zinajengeka chuki dhidi ya vyombo vya dora tunakoenda kuna hatar kubwa hii ya kulazimisha mtu kumtawala na kumuongoza kimabavu.
 
Back
Top Bottom