Hakuna kitu hapa.
Hizi ni rongorongo tu za JANUARI/CCM. Huyu jamaa alikuwa ndani ya Ikulu,siji mwandishi au karani wa Ikulu au sijui nani.
Hili SWALA LA UMEME SI GENI KWA JANUARI. Ila anajifanya hamnazo.
Tayari kule mjengoni keshapewa Uwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.
Ngeleja tayari ameshaelekezwa na Spika Makinda kuandaa TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU MGAWO WA UMEME UTAISHA LINI baada ya swali kutoka kwa mheshimiwa Mbowe.
Januari,Ngeleja,Makinda wanachofanya kwa sasa ni dilly dallying za kisiasa za kutaka kuwachanganya Watanzania na waone kwamba CCM wanashughulikia TATIZO LA UMEME ilhali siyo kweli.
Kama ulimsikiliza Ngeleja akijibu hoja za Wabunge hasa wa Upinzani kuhusiana na swala la Umeme utagundua kwamba ni POROJO ZILEZILE ZA KUEDELEA KUWADANGANYA WATZ NA BUNGE LOTE KWA UJUMLA. Majibu yake yamejaa mipango na mikakati hewa ambayo haina mashiko.
Watanzania tunataka UMEME na siyo UUME WA NGELEJA,JANUARI AU KIWETE. We want POWER and nothing else,failure to which PEOPLES' POWER shall apply.