Kiini cha mahusiano ya CIA na Vatican

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939
220px-William_Donovan.jpg

Jenerali William J Donovan "Wild Bill"

Baada ya vita ya kwanza ya dunia Marekani ilikua haijapata taasisi bora itakayo kusanya taarifa nzuri za kiuchumi na kisiasa katika kuijenga Marekani ndipo Rais wa Marekani miaka ya Franklin D. Roosevelt kwa kushauriana na shujaa wa vita kuu ya kwanza ya dunia Jenerali William "Wild Bill" Donovan kuanzisha taasisi inayoitwa office of Co-ordination of Informations ( COI ), mwaka mmoja baadae yani tarehe 11/julai/1942 ikaboreshwa ziadi na kuitwa OSS yaani office of strategy Services na jenerali William“Wild Bill” Donovan kuwa Mkuu wa taasisi hiyo hadi ilipobadilishwa tena mwaka 1945 kuwa Strategy Service Unit (SSU), mwaka 1946 ikabdilishwa tena kuwa Central Intelligence Group (CIG) na mwaka 1947 kuitwa Central Intelligence Agency yaani CIA.

Siku moja ya mwezi wa Julai mwaka 1944 wakati vita kuu ya pili ya dunia inapamba moto katika bara la Ulaya, wakati huo aliekua Mkuu wa huduma za kimikakati ya nje ya Marekani yaani OSS baadae kupitia maboresho mengi hadi kubadilishwa kuwa CIA Jenerali William “Wild Bill” Donovan alikutana na Papa Pius XII katika misa kubwa jijini Vatican, ndipo Papa Pius XII akamvalisha Jenerali Donovan zawadi ya msalaba mkubwa wa dhahabu ulioitwa " Grand Cross of the Order of Saint Sylvester" zawadi hii hutolewa kwa watu 100 tu duniani ambao wamelitendea kanisa katoliki mambo ya kupendeza,kulinda kanisa kwa hali na mali, msalaba huu ni zawadi ya juu kutoka ofisi ya Papa mtakatifu, alipewa zawadi hiyo kwa kuwa amelilinda kanisa katoliki dhidi ya hujuma za kinazi na kikommunist yaani alizuia kanisa katoliki kutodondokea mikononi mwa Wanazi wa komuninist wabaya, wakati huo wajerumani walikua katika jitihada za kutawala Ulaya Magharibi ili kusambaza propaganda za kikomunisti, ndipo Jenerali Donovan alikutana na mwasisi wa shughuli za kijasusi kanisa katoliki Ulaya kwa kifupi Pro Deo yaani Father Felix Morlion na kujadili mjini vatican jinsi gani ya wanaweza kuliepusha kanisa na wanazi wa ukommunist hasa wajerumani, ndipo jenerali William "Wild Bill"Donovan alimsaidia Father Morlion kuhamisha harakati za operesheni za kijasusi wa kanisa katoliki kutoka Ureno mji wa Lisbon mpaka sehemu za New York Marekani,Wakati huo kanisa katoliki lilihitaji kabisa kuzuia ukommunist ndipo Jenerali Donovan alipofadhili shughuli hizo za kuzima ukommunisti na sera zao uliokua unalinyemelea kanisa katoliki kutokana na mali nyingi za kanisa katoliki lilizochuma kupitia maajenti wake mbalimbali duniani, Jenerali William Donovan akijua fika kwamba fadhila hizo zitazaa matunda katika kulimulika kanisa katoliki na kupata taarifa za dunia nzima kupitia mapadri na watoa huduma za kiroho, kielimu, kiafya na kiuchumi watakaosambazwa duniani kupitia kanisa katoliki,Jenerali Donnovan alibashiri kwamba kwa wingi wa waumini wa kanisa duniani CIA wangeweza kuimulika dunia kupitia watu hao hata wawakilishi wa mapapa duniani kupata hata habari za dunia inavyopanga na kwenda, vilevile aliamini kanisa katoliki kupitia ofisi ya Papa ndio taasisi itakayopata habari nyingi na kila siku za haraka duniani kupita taasisis zozote zile duniani kupitia wahudumu wakaosambazwa kupitia ufadhili huo wa Jenerali Donovan ndani ya taasisi ya OSS yaani Office of Strategic Services, baada ya mafanikio ya kuzima ndoto za wakommunist kutimia na kufanikiwa kuunganisha taasisi zilizochini ya kanisa kupitia waumini na vikundi tajiri kama vile "The Knights of Malta" wenye mabenki, taasisi za utangazaji na makampuni makubwa ya tekinolojia na ufundi duniani

Father Morlion ndipo aliposambaza wahudumu wa kiroho duniani kote na kuisaidia CIA kupata habari kila siku na kila dakika duniani kutoka kwa mapadri na wahudumu wote habari hizo ziliratibiwa na sekretariet ya Papa huo ndio ukawa mwanzo wa mahusiano ya kupendeza kati Kanisa katoliki na CIA, hivyo basi baada ya vita kuu ya dunia CIA wakaendelea kufadhili taasisi zilizo chini ya kanisa katoliki kuwapenyeza mapadiri ili waitumikie CIA kwa manufaa ya Marekani, kuweka maajenti wake karibu na Papa ili asijaribu kubadili msimamo wa uhusiano kati ya CIA na Vatican hususani sera za kisiasa na kiuchumi duniani pia kujaribu kuchagua Papa mwenye msimamo mzuri hasa wenye maslahi ya Marekani na CIA.
 
Rc ni kanisa pekee litakalofunga historia ya dunia na mikakati yàke ya kuunganisha makanisa lazima itekelezwe
 
Nafikiri umeandika kitu usichokijua vizuri
Unachoshindwa kuelewa tu kama kanisa halina maslahi na kitu chochote basi halipelekeshwi na yeyote labda tu kama kuna maslahi ya kanisa yatapotea hapo kanisa lishirikiana na yeyote
Ni kanisa pekee lisilopelekeshwa na yeyote kwa kuwa haliombi msaada kwa mtu hivi sasa

Na kingine nikuambie labda tu hujui namna uchaguzi wa kumchagua Papa ulivyo
Hata hao wanaochagua wenyewe wanakua hawajui ni nani atakuwa Papa maana maana anaweza kujichagua yeye mwenyewe pia
 
Nafikiri umeandika kitu usichokijua vizuri
Unachoshindwa kuelewa tu kama kanisa halina maslahi na kitu chochote basi halipelekeshwi na yeyote labda tu kama kuna maslahi ya kanisa yatapotea hapo kanisa lishirikiana na yeyote
Ni kanisa pekee lisilopelekeshwa na yeyote kwa kuwa haliombi msaada kwa mtu hivi sasa

Na kingine nikuambie labda tu hujui namna uchaguzi wa kumchagua Papa ulivyo
Hata hao wanaochagua wenyewe wanakua hawajui ni nani atakuwa Papa maana maana anaweza kujichagua yeye mwenyewe pia

Sawa
 
NDO MAANA KUTOKUWEPO KWA CATHOLIC CUBA NA KOREA KASIKAN ,KUMEFANYA KAZI YA CIA KUWA NGUMU !!!.

NDIO MAANA MAHALI AMBAPO HAMNA CATHOLIC POPOTE PALE LAZIMA MAREKAN AMUONE NI ADUI .

REFERS... CHINA,,,CUBA,,,IRAN,,,,N.KOREA,,RUSSIA. N.K

Upo sahihi kabisa Mkuu
 
Back
Top Bottom