Kiingilio cha madhabahu za giza

Kiingilio cha madhabahu za giza

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,938
Reaction score
828,620
Unapoenda kwa mganga wa kienyeji unaenda kutengeneza maagano
Ukifika pale lazima yatatokea haya

1. Atavaa mavazi rasmi ya kazi (inaitwa kuvaa miongozo)

2. Mtakuwa kwenye chumba chenye madhabahu inayoendana na shughuli zake(kilinge)

3. Utajieleza ama atakueleza matatizo yako!

4. Utatoa pesa na kuiweka kwenye chombo maalum kilichopo madhabahuni ama karibu na hapo! Hupangiwi kiasi(hapa unatoa kiingilio bila kujua)
Ukishatoa yatafuata matibabu utatumwa vya kuleta, lazima damu itahusika in most cases! Kwanini damu? Kwakuwa ni chakula cha kuzimu! Na hapa baada ya kuingia kwa kutoa kiingilio sasa unaanza kutumikia, unaanza kuhudumia

Yatakayoendelea yote ni utumwa, utaelekezwa ya kufanya na utaambiwa ufuate masharti la sivyo hutafanikiwa! Unatii bila kujua kuwa tayari umeshaingia kwenye milki na maagano mabaya kabisa

Kwa kiasi kidogo kabisa cha pesa, unaharibu mchoro wako wa maisha kwa kuingiza visivyotakiwa! Yani unajaribu kuiedit asili! Unataka kuusahihisha uumbaji!

Utapata utakacho lakini kwa masharti utatumikia maagano na mamlaka za kuzimu! Utakuwa ni MTU wa kutoa makafara ya damu kwenye madhabahu za giza... Utapata mafanikio lakini ni ya muda,..

Kadiri muda unavyoenda utaanza kuchoka na kuanza kugundua ukweli kwamba huna amani tena huna furaha tena na unaishi kwenye utumwa wa maagano na masharti mengi!
Unajiona tofauti kabisa na ulivyokuwa mwanzo! Unaikumbuka asili yako(ukibahatika)...sasa vita kamili huanzia hapa! Kutaka kufuta yale marekebisho uliyofanya tena kwa kiingilio na kafara!

Ushirikina haujawahi kumuacha mtu salama! Kuwa makini unapotafuta suluhisho la matatizo yako!!!!
 
Madhabahu za kichawi zinatesa sana watu. Mwanzo wake huwa mtamu kama asali, ila mwisho wake mchungu KAMA shubiri.
Madhabahu za kichawi ni magereza ya mateso iliyo wameza wengi
20140429_103320.jpg
 
Mshana Jr kuna ile wanasema kutambulisha watoto kwenye ukoo...!
Mbuzi anachinjwa nyama inaliwa na wanaukoo wote, kama MTU atagoma kufanya hivyo basi wanae watakuwa na shida mbali mbali. Mfano uncle wangu amegoma ila wanae wa kwanza wa kiume na kike wana shida kubwa sana ya macho,
Niliwahi kumsikia bibi akisema ni kwa sababu baba yao amekataa kuchinja mbuzi ya kuwatambulisha kwenye ukoo. Nadhani haina tofauti na mganga wa kilingeni. Ile mizimu inakuamdama popote uendapo lazima itataka uje utukuze mizimu kwa mbuzi labda uwe tasa
 
Haya maagano ya koo na families zetu nayo ni mabaya mno! Yani mnatengeneza roho na kuilisha nanyi mnashiriki ile ibada kwa kula ile nyama bila kujua
Na ili hii roho iendelee kupata uhai inabidi kila wakati ipate damu, si kama chakula as such bali lile tendo
 
Mshana acha tu na wanaopingana Nazi wanapata changamoto kuuubwa sana. ! Kuna uncle wangu alienda German bariidi ikamzidia kule akarudishwa, ndugu zake wakasema ni kwa vile hajachinjiwa mbuzi, mbuzi ikachinjwa.. Trust me anaendaga tena na tena hata misimu ya baridi ila hajawahi rudishwa...! Hapa naona shetani anavyowaletea tricks
 
Back
Top Bottom