Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 93,479
- 119,309
Kiswahili ni lugha nzuri na iliyo tamu sana.
Na ni moja ya lugha zilizo rahisi kujifunza.
Tatizo moja kubwa nilionalo mimi ni ukosefu wa taasisi imara za kukikuza.
Baadhi ya watu hudai Kiswahili hakijitoshelezi kimsamiati kama ambavyo Kiingereza kinavyojitosheleza.
Hiyo dhana sikubaliani nayo. Ni dhana potofu.
Kiingereza kimeazima maneno hadi kwenye Kiswahili! Huko kwenye Kilatini ndo usiseme kabisa.
Kila mwaka taasisi za lugha ya Kiingereza huingiza maneno mapya kwenye kamusi zake.
Kwenye Kiswahili sijawahi kuliona hilo.
Sasa kwa mfano kama maneno flani ya Kiingereza hayapo kwenye Kiswahili kwa nini tusiyaazime na tukayaswalihisha tu ili nasi tuwe nayo?
Mbona mengine tumeyaswalihisha? Polisi tumeliswalihisha...hospitali tumeliswalihisha.....shule tumeliswalihisha...na mengineyo mengi tu tumeyaswalihisha.
Sioni kwa nini tusiyaswalihishe na hayo mengine ambayo hatunayo kwenye msamiati kwa sasa.
Waingereza hadi neno 'safari' wameliazima na kuliingiza hadi kwenye kamusi zao.
Hata sisi naamini tunaweza kufanya hivyo hivyo kwa yale ambayo tunaona hatunayo.