Hata hivyo unaeza kuwa Rais wa Tanzania siku moja. Hiyo ni dalili nzuri (utani).
Mimi nilikuwa katika hali yako. Ninapenda sana kufanya kazi mashirika ya kimataifa lakini ikija kwenye ngeli, shida. Unajua tena Kiingereza cha kujifunzia ukubwa. Walimu wenyewe wa sekondari na chuo wanafundosha masomo ya Kiingereza kwa kutumia Kiswahili. Walimu ndio hawa hawa akina Magufuli (Sengerema Sekondari).
Nimejitahidi sana kujilazimisha kuongea ongea kama sehemu ya practice. Baadaye nikapata fursa ya kuwa nje ya Tanzania, nikajitahidi sana. Kwa sasa naweza kuwasiliana vizuri tu. Unapojifunza usijali watu kukucheka. Mbona Wachina, Wajapan, Wafaransa hawana aibu wanapovunjavunja Kiingereza? Sisi Waswahili shida yetu ni aibu na kuchekana.
Lakini pia kumbuka kuwa ukijifunzia ukubwani, hata ukiongea hauwezi kuwa kama mtu aliyeanza wakati ni mtoto. Isitoshe public speaking pia ni skill ambayo inaweza isihusiane na uwezo wa lugha.
Kuna watu hata kwa Kiswahili ama kilugha chao hawawezi kusimama mbele za watu na kuongea. Ndio maana Englsih medium/International schools wanafundisha watoto kujieleza tangu madarasa ya mwanzo. Wanasimamishwa kwenye majukwaa mbele ya wenzao na kuimba, kujieleza nk. Wanazoea. Na waliopitia mfumo huu huwa wanashinda tu interview hizo unazosema huwa unashindwa.