Kihongosi: Mahakama haiingiliwi

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
"Wenzetu wa CHADEMA wamekuwa wakitoa kauli za kuitaka mahakama kumuachia kiongozi wao, tunapenda kuwaambia kuwa mahakama haingiliwi,waiache ifanye kazi yake ya utoaji wa haki kama kiongozi huyo ameonewa au tuhuma hizo ni za kweli mahakama itasema".

Darmpya

IMG_20211026_213901.jpg
 
Kijana aambiwe kuwa, Mahakamani haitengeneza kesi... ni serikali ndio inatengeneza kesi.
 
"Wenzetu wa CHADEMA wamekuwa wakitoa kauli za kuitaka mahakama kumuachia kiongozi wao, tunapenda kuwaambia kuwa mahakama haingiliwi,waiache ifanye kazi yake ya utoaji wa haki kama kiongozi huyo ameonewa au tuhuma hizo ni zakweli mahakama itasema"

DarmpyaView attachment 1987736
Ni upuuzi kusema eti wanasubiri mahakama itoe hukumu wakati wewe uliyembambikia kesi unajua kabisa kuwa umembambikia.
 
Hata kuiteulia majaji ni kuingilia uhuru wa mahakama pia, hawa watoto wamepewa vyeo naona hata uwezo wa kufikiri vizuri hawana.
Kihongosi, Kingai, sabaya wote Ni walewale, na hii inshu ya kesi ya ugaidi waliompa mbowe anaijua vizur sana!

Wametengeneza mazingira kuona Sabaya kafungwa ili wamfunge Mbowe ionekane Mahakama inatenda haki kotekote!

Ukwel Ni kwamba, mbinu inajulikana, sabaya atatoka very soon mara baada ya Mbowe kufungwa!

Wasituhadae Hawa watu
 
Pelekeni upuuzi wenu,kirongosi amesema kweli ...watu wa chadema ni much know..angali ni mazuzu ...mahakama imemuhukumu sabaya imetenda haki leo mwenyekiti wao kuna ushahidi wa moto shidi yake wanaanza kurukaruka kama maharage jikoni...sema Kirongosi..usiwasikilize hawa wahuni.
 
Bado vijana wengi wa upinzani nchi hii hawasimami kwenye kile wanachokiamini.
 
Huyu bwana mdogo ana vinasaba sawa na yule sijui ndio mwenezi wa CCM sasa, huwa wao wanaendeshwa na matukio ili kupata chochote cha kusema...

Ukifikiria sababu haswa ya yeye kuanza kuongea hayo ni nini, utaishia kupata jibu ni kubwabwaja tu asisahaulike...
 
"Wenzetu wa CHADEMA wamekuwa wakitoa kauli za kuitaka mahakama kumuachia kiongozi wao, tunapenda kuwaambia kuwa mahakama haingiliwi,waiache ifanye kazi yake ya utoaji wa haki kama kiongozi huyo ameonewa au tuhuma hizo ni zakweli mahakama itasema"

DarmpyaView attachment 1987736
Mpuuzi sana huyu, mwambie Sabaya amemtaja huko, akae kwa kutulia
 
Kihongosi, Kingai, sabaya wote Ni walewale, na hii inshu ya kesi ya ugaidi waliompa mbowe anaijua vizur sana...
Sabaya aliyekutwa na hatia na kuhukumiwa hawezi kuwa wa maana kwenye kutoa ushahidi dhidi Mbowe na wenzake, inajulikana wazi mipango yao ya hovyo waliilanga mapema bila kujua Magufuli atakufa, baada ya hapo kilichotokea hata wao hawajui wafanye nini.
 
Hii ndiyo shida ya Tanzania, uchaguzi serikali za mitaa waliharibu , uchaguzi mkuu nao waliharibu, CHADEMA ikagoma kuwapeleka wabunge viti maalumu, wao wakawarubuni COVID-19, wamewapiga kwa risasi, wengine wameponea chupuchupu bado wanataka kumfunga m/kit kisa katiba mpya ingawa wanapindisha kuwa ni Ugaidi!!

Matendo ya Viongozi wetu ya namna hii yaleta kinyaa kwa Taifa letu pia tunanekana Ni wa hovyo!!
 
"Wenzetu wa CHADEMA wamekuwa wakitoa kauli za kuitaka mahakama kumuachia kiongozi wao, tunapenda kuwaambia kuwa mahakama haingiliwi,waiache ifanye kazi yake ya utoaji wa haki kama kiongozi huyo ameonewa au tuhuma hizo ni zakweli mahakama itasema"

DarmpyaView attachment 1987736
Yakweli hayo, mbona hisia ni nyingi zakutokuwepo kutenda na kutendewa haki katika kesi, hii kama taifa tulikosea, tumekosea ama tunakosea wapi. Maneno ya kisiasa huaminiwa zaidi na wanasiasa, ila matendo ya mifumo imara huonekana Kwa vitendo.
 
"Wenzetu wa CHADEMA wamekuwa wakitoa kauli za kuitaka mahakama kumuachia kiongozi wao, tunapenda kuwaambia kuwa mahakama haingiliwi,waiache ifanye kazi yake ya utoaji wa haki kama kiongozi huyo ameonewa au tuhuma hizo ni zakweli mahakama itasema"

DarmpyaView attachment 1987736
Kihongosi nae anatakiwa atuambie baada ya Sabaya ku kwapua pesa kwa Saad walikutana na Sabaya akagawana na Kihongosi pesa za ujambazi wa kutumia silaha. Iko siku ataelezea hili
 
"Wenzetu wa CHADEMA wamekuwa wakitoa kauli za kuitaka mahakama kumuachia kiongozi wao, tunapenda kuwaambia kuwa mahakama haingiliwi,waiache ifanye kazi yake ya utoaji wa haki kama kiongozi huyo ameonewa au tuhuma hizo ni zakweli mahakama itasema"

DarmpyaView attachment 1987736
Hakuna anaetaka mahakama imwachie Mbowe kwani haina uwezo huo kikatiba. Kinachosemwa hapa ni kuzitaka taasisi zenye mamlaka kisheria za kuitoa hii kesi mahakanani zifanye hivyo kama zilivyofanya kwa masheikh wa uamsho, vijana wa BAVICHA pale Dodoma, na kesi zile 147 ambazo rais mwenyewe alisema watu wa TAKUKURU walizifuta na kuwaagiza polisi nao wafanye hivyo. Kesi ya Mbowe iko kwenye kundi hilo la kesi za kubumba na kwa hiyo inastahili kufutwa.
 
Back
Top Bottom