Kigwangwalla: Si sahihi kuweka kikomo cha ubunge!

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,028
144,382
Mh.Hamisi Kigwangwala amesema si sahihi kuweko ukomo kwa mbunge kugombea jimbo fulani kwani wenye maamuzi ni wananchi.

Katika kutetea hoja yake hiyo,mh.Kigwangala amesema hata mataifa ambayo ni vinara wa demokrasia duniani kama Marekani na Uingereza,mbunge anaweza kudumu(kuchaguliwa) hata kwa muda wa miaka 30.

Wakati huo huo, mh.Mnyika ameunga mkono kuwepo kwa ukomo wa vipindi vitatu.

Kuhusu posho,Kigwangala amekataa kabisa kuzungumzia posho kwa maelezo sio hoja ya msingi.Kwa upande wa Mnyika,yeye amepinga posho hiyo ya 300,000 na kusema wasihukumiwe wabunge wote kwa hoja hiyo.

CHANZO:Star tv

MY TAKE:
kuna tofauti kubwa sana ya wabunge wa CCM na CHADEMA.

Tafakari na utajionea mwenyewe ni nani mbunge kimeo hapo.
 
mbowe ndio kinara wa kudai posho, mnyika atapinga ana uwezo gani??

kigwangallah anachemka. vipindi vitatu vinatosha sana, hoja zake hazina mashiko
 
Sasa kama.mnapinga enyi Chadema si muitishe press tuwasikie sio kila mtu kutoa tamko alikojifichia!!!!!!!

Suala la bei ya umeme huyo Mnyika wako bado anakusanya signatures???!!!!!!

Kwa sasa wote kundi moja tu tofauti rangi!!!!!!!
Na watu kama wewe ndio maadaui wa ukombozi sababu kila wananchi wanapokaribia kuungana mnaleta utenganishi wa makundi ya kisiasa hii ni tabia ya kisyenzi kabisa na wewe ni mmoja kati ya wasaliti wa ndani!!!!!!!

Unafaa kabisa kuchinjwa wewe!!!!
 
mkuu hapa nadhani hawaelewi hoja ya Tume ya katika.RAsimu inazungumzia wabunge wa bunge la Muungano ambao wanatokana na Mikoa na sio majimbo ndo hawatatakiwa kugombea zaidi ya mara 2.Ila haijazungumzia wabunge watokanao na majimbo ya uchaguzi ambayo yatakuwa chini ya katiba ya Tanganyika.
 
sheria ni msumeno, itakata pande zote
 
mbowe ndio kinara wa kudai posho, mnyika atapinga ana uwezo gani??

kigwangallah anachemka. vipindi vitatu vinatosha sana, hoja zake hazina mashiko

Mkuu vipindi viwili vinatosha saaana kwa mtu mchapa kazi na kama ana nia ya kutumikia wananchi kwa vipindi hivyo atakuwa tayari kaanzisha CBO na akimaliza second term basi atashughulikia jimbo kupitia CBO!!!!!

Yaani mtu aanze undergraduate mpaka PhD huyo mbunge awe bado tu hapo hapo NO waaaay mkatafute kazi bhana kwanza si wamesoma wengine warudi kwenye fani wakajenge Taifa pia kutumikia nchi sio lazima awe mbunge!!!!!!!!
 
Sasa kama.mnapinga enyi Chadema si muitishe press tuwasikie sio kila mtu kutoa tamko alikojifichia!!!!!!!

Suala la bei ya umeme huyo Mnyika wako bado anakusanya signatures???!!!!!!

Kwa sasa wote kundi moja tu tofauti rangi!!!!!!!
Na watu kama wewe ndio maadaui wa ukombozi sababu kila wananchi wanapokaribia kuungana mnaleta utenganishi wa makundi ya kisiasa hii ni tabia ya kisyenzi kabisa na wewe ni mmoja kati ya wasaliti wa ndani!!!!!!!

Unafaa kabisa kuchinjwa wewe!!!!

Mjumbe hauwawi!
 
he he he, anaogopa umri wa kustaafu kumfikia mapema?

Ajabu ya Mungu kijana anaogopa mapambano aje huku tukomae si anajipambanua ni msomi????!!!
Aje huku atumie cheti chake tuone professionalism sio kukomalia ubunge!!!!!!
 
Kigwangala Ana tamaa ya madaraka eti swala la posho analikwepa hv Huyu ni mtz kweli au kule nzenga wananchi wake hawana shida??
 
Ujinga tu.

Vipindi vi3 vya ubunge vinatosha sana, kwanza inamsaidia kuwa kukusanya mtaji, connected, kupata tenda kwa mahsarti nafuu, kufungua makampuni at minimuma cost(ujue mbunge hazinguliwi)

Akitoka hapo anaendesha makampuni yake tu.
Kumbe Kigwa ni kiazi kikuu?
Ajabu ya Mungu kijana anaogopa mapambano aje huku tukomae si anajipambanua ni msomi????!!!
Aje huku atumie cheti chake tuone professionalism sio kukomalia ubunge!!!!!!
 
Hii ndo tweet yake wakati akiendelea na mjadala hapa ndo utajua yuko upande gani wa sakata hili la posho.

Hamisi Kigwangalla ‏@hkigwangalla 53m Tunajadili 'posho' badala ya mambo mazito kama 'muundo wa muungano'. Opinion makers wote wamekubali kuhamisha mjadala...Taifa la siasa siasa

hataki kuzungumzia suala ka posho kwa kuwa yeye nae ana maslai nayo, wote hao wachumia tumbo wanataka kujinufaisha within those 76 dayz, hivi wanamfikiria yule mwalimu wa shule ya msingi huko tandaimba anaefanya kaz katika mazingira magumu(no water,eletricity,roads,hospitali etc) anaelipwa laki 3 net bila posho?
 
Ujinga tu.

Vipindi vi3 vya ubunge vinatosha sana, kwanza inamsaidia kuwa kukusanya mtaji, connected, kupata tenda kwa mahsarti nafuu, kufungua makampuni at minimuma cost(ujue mbunge hazinguliwi)

Akitoka hapo anaendesha makampuni yake tu.
Kumbe Kigwa ni kiazi kikuu?

Dada weee vipindi viwili kwa mtu serious ndio nitoleee na jimboni unaacha legacy yaani miaka kumi haitoshi! !!!!!??????
Sasa mtu kaa huyu ndio eti damu changa na watu wanategemea ukombozi kutoka kwa watu kama hawa!!!!!!

Mimi binafsi ndio maana kwa mfumo uliopo nikimuona kijana yupo karibu sana na chama cha siasa jambo la kwanza kabisa ni kutokumuamini!!!!!!
 
Niwambie tu kuwa kipengele cha ukomo wa ubunge hakitopitishwa na hilo bunge liliojaa ma-ccm.

Kigwangwala anawakilisha maoni ya wenzake kwa mtindo usio rasimi ila habari ndio hio!
 
Mheshimiwa soma alama za nyakati, hiyo hoja yako haina mashiko kwa kipindi hiki. Tafakari tena.
 
Hoja ya kwamba tusiweke ukomo wa ubunge kwa sababu uamuzi ni wa wananchi haina nguvu kwa sababu hata urais ni uamuzi wa wananchi lakini ukomo upo. Pia kujaribu kuhalalisha ubunge wa maisha kisa eti Marekani wako hivyo ni makosa kwa kuwa changamoto zetu na zao ni tofauti. Si vema kuiga kila kitu kisa kinafanywa na wakubwa, mwisho tutahalalisha hata bangi na ushoga kwa huu mtindo wa kufyonza kila jambo linalofanywa na nchi zilizoendelea. Naunga mkono hoja ya ukomo!
 
Back
Top Bottom