Kigwangallah matatani kwa tuhuma za ufisadi

Kigwangallah matatani kwa tuhuma za ufisadi

Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
Kama kutoa taarifa zilizofichika tena na vithibitisho ni udaku oooh saaafi sana CCM mwaka huu mtakoma, nendeni mkaangalie huo mnaoitwa udaku unaisha saa ngapi kwa wauzaji saa nne asubuhi hulipati mahali popote na ukiuliza unashangawa!

ila nakusaidia, mwandishi wa habari mzuri ni yule anayetafuta habari za kuandika sio yule anayesubiri kulipwa ili aweke habari hewani!
 
nimesoma hoja hii kwa makini lakini nilipoona tanzania daima eti ndiyo chanzo cha taarifa poleni bola nikalale.

Kigwangala ni member humu si muache aje akanushe mwenyewe!
 
E Mungu wetu Mwenye huruma tuhurumie sisi waja wako watanzania, tuondelee hii CCM na majangili wake katika madaraka ya nchi yetu.amina
 
Kiwanda cha uongo in action.

Mjinga wewe, huu ndo upuuzi wa kutumwa tu kutetea huja bila kuambiwa utetee vipi hoja nzito kama hii. Mwacheni kingwangallah mwenyewe ajitee, we umejuaje kama ni uwongo? Gazeti limekuja na facti, we kazi kuandika tu uwongo bila facti... ni ijinga mkubwa sana. Ndiyo maana mnaambiwa kuwa watetezo wote wa ccm humo jamvini mko kibaruani. Hakunaga mnachosema zaidi ya kuandika, si kweli, uwongo, umbeya, n.k. toeni hoja mnapopinga hoja.
 
Doctor kingwalangwala vitumbua uko wapi?
njoo ujibu hizi tubuma kabla hatujakuburuza mahakaman!
 
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
Boss wangu nipe mautundu ya kunifanya na mie niweze post kama wewe kila dakika post moja! Wangu sio siriTzs 7000x60minx24hrs...du unapata mahela wewe acha tu
 
Tunawalaumu wabunge kwa kutoa michango yao kwa hisia, lakini inaonekana wanajf we are not immune from that syndrome, Mtoa mada ameongelea ufisadi watu manjadili gazeti wapi na wapi. Let us be objective and stay focused
 
Uhuru na Mzalendo ni sehemu ya historia ya nchi yetu...
So we do not have to live the present and aspire for a bright future.

Do we have to live our past no matter what?

Mtu mwenye akili kama wewe ZeMarcopolo akiamua kuwa mpiga propaganda anashuka mno.

Pole na mafisadi unaowatetea bila kujua unachotetea.
 
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
Udaku haumaanishi uongo, wala si lazima uwe kweli. Mwandishi kafanya sehemu yake, liliobaki ni jukumu la vyombo vya dola (KAMA VIPO) kuthibitisha au kukabatilisha (kwa ushahidi) kama alivyofanya mwandishi.
 
Sishangai sana maana nchi imeoza na inanuka rushwa toka bagamoyo mpaka monduli.
 
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
Hata kama ni la udaku unatakiwa kusema kama ni kweli au uongo. Kwa habari hii je, hakusamehewa kodi? Je hakuingiza bidhaa hizo? Je kampuni si yake? Je, hakuuza hivyo vifaa vilivyo samehewa kodi? Ujue kwa kariba yako hukutakiwa kusema tu ooooh! Tanzania daima ni gazeti la udaku. Jibuni tuhuma hizo
 
Huyo charlatan ni Msukuma wa wapi huyo? Maana nijuavyo Nzega iko Tabora na Tabora ni kwa Wanyamwezi.

Ngosha, kiundani Tabora kuna wadakama. Maana inasemwa kwamba, wadakama (kama sikosei inamaanisha wakusini) na wasukuma (kama sikosei pia inamaanisha wakaskazini) ni kabila moja.
Mimi nimesikia kabila hilo ndiyo uitwa Wanyamwezi.

Sasa pengine historia hiyo haiko hivyo. Kama ndivyo, ebu nisaidie hapa.
Balantanda Sikonge Mzee Mwanakijiji na wadakama na wasukuma wote msaada tafadhali.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, upo sawa kabisa kuwa kuna Wa Kaskazini (Wa Sukuma) na Wa Kusini (Wa Dakama).

Ndiyo maana kwenye Data za ukweli, Wasukuma na Wanyamwezi (Wadakama) wote huitwa Wanyamwezi na ndiyo wanaoleta hiyo idadi inayosema Wanyamwezi ndiyo kabila kubwa Tanzania kwa asilimia zaidi ya 14.
Ngosha, kiundani Tabora kuna wadakama. Maana inasemwa kwamba, wadakama (kama sikosei inamaanisha wakusini) na wasukuma (kama sikosei pia inamaanisha wakaskazini) ni kabila moja.
Mimi nimesikia kabila hilo ndiyo uitwa Wanyamwezi.

Sasa pengine historia hiyo haiko hivyo. Kama ndivyo, ebu nisaidie hapa.
Balantanda Sikonge Mzee Mwanakijiji na wadakama na wasukuma wote msaada tafadhali.
 
MBUNGE wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla (CCM), anadaiwa kuliibia taifa kwa kutumia vibaya misamaha ya kodi ya mamilioni ya shilingi kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha afya eneo la Uchama, wilaya ya Nzega.

Kwa mujibu wa nyaraka ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, Dk. Kigwangallah amejipatia misamaha ya kodi ya ongezeko la thamani na ushuru wake kupitia kampuni ya Emergent Africa Limited, anayoimiliki kwa asilimia 78 na Bayoun Kigwangallah ana asilimia 22.

Kupitia kampuni hiyo, mbunge huyo ameingiza nchini bidhaa mbalimbali ambazo badala ya kuzielekeza katika ujenzi, amefungua duka la kuuza vifaa vya ujenzi eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam na nyingine anaziuza kwa wafanyabiashara wengine.

Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa kampuni ya Emergent Africa Ltd, ilisajiliwa katika Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) Septemba 27, 2011 na iliruhusiwa kupata misamaha hiyo kuanzia Septemba 2011 hadi Agosti 2014.

Kwa mujibu wa makubaliano kati ya kampuni ya Emergent Afica Ltd na TIC, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliombwa kuisamehe kodi kampuni hiyo ya Dk. Kigwangallah vitu mbalimbali vyenye orodha toka namba 1 hadi 390.

Bidhaa hizo kwa uchache ni kompyuta 1042, mashine za kutolea kopi 12, printa 12, ‘binding machines' 12, vikokotozi (calculator) 640, projekta 12, video kamera 12, feni 30, vifaa vya simu masanduku 28, jenereta moja, magari aina ya Toyota 13, lori 3, Nissan Navarra Pik up 4, Mitsubishi Canter 2 na mabasi madogo manane.

Pamoja na msahama huo, Dk. Kigwangallah kupitia kampuni hiyo, aliingiza nchini vitu bidhaa mbalimbali vikiwemo vigae vya sakafuni 2500 vyenye ukubwa wa 600X600 na 1000 vyenye ukubwa wa 400 X 400 pamoja na vigae vya ukutani.

Katika orodha hiyo viko viti na meza za kulia, hema la bustanini, sofa, kabati za kuwekea nguo, mazulia, vitanda na magodoro, televisheni na vingine.

Aidha nyaraka hizo zinaonyesha baada ya kupokea bidhaa hizo kutoka nchini China, ziliuzwa katika maduka mbalimbali ya Kariakoo na vigae vingine kuuzwa kwa mkuu wa wilaya moja mkoani Tanga (hatukumtaja) kwa kuwa hakupatikana kujitetea.

Hata hivyo, kumeonekana utata katika nyakara hizo kwani kampuni ya Delmas iliyosafirisha kontena la bidhaa hizo kuja kwa Dk. Kigwangallah, ziko tofauti na ankara za malipo.

Ankara hizo zinaonyesha kuwa zilitolewa na makampuni ya Louis Valentino Investment and Development Co. Ltd iliyopo Na. 19 Ji Hua 3 Road Foshan na Sharpeye Furniture.

Wakati manunuzi yakionekana kufanyika China Oktoba mosi, 2012, nyaraka nyingine zinaonyesha kuwa mali zilishaingizwa nchini tangu Aprili 14 mwaka huo, kupitia kampuni ya Innovative Freight yenye TIN 100-145-596, risiti namba 2012/0000002986.

Na nyaraka za mamlaka ya mapato zinaonyesha bidhaa hizo ziliingia nchini Aprili 3 mwaka jana, hali inayoonyesha kupishana katika tarehe za kununua na kuingiza bidhaa hizo.

Pia utata huohuo unaonekana katika taarifa za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambazo zinaonyesha bidhaa hizo zilikaguliwa Machi 28, 2012.

Huku kukiwa na orodha zinazotofautiana za makampuni mawili ya kibiashara wakati ankara ya malipo ilikuwa moja.

Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa kontena hilo lilipofika nchini lilionekana kuwa na vitu tofauti na vile vilivyoorodheshwa, hivyo kusababisha kontena hilo kufanyiwa uchunguzi usio wa kawaida kwa kupekua mzigo mmoja mmoja.

Dk. Kigwangallah alipotafutwa kwa simu kufafanua tuhuma hizo, alisema amebanwa na kazi. Na alipoambiwa ametumiwa maswali kwenye barua pepe yake, aliahadi kujibu lakini hakufanya hivyo.

Alipopigiwa tena jioni, alisema, "Sema haraka unataka nini?" Alipoulizwa juu ya tuhuma hizo alikata simu.

Lakini baadaye aliandika ujumbe kwa simu: "Nitakupigia jioni nikitoka bungeni."

Alipoambiwa inaandikwa habari gazetini, alijibu kwa ujumbe mfupi kuwa tuhuma zilikuwa za uongo bila kufafanua.

CHANZO: Tanzania Daima
 
Back
Top Bottom