Kigwangallah matatani kwa tuhuma za ufisadi

Kigwangallah matatani kwa tuhuma za ufisadi

tunduruboy

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
423
Reaction score
218
MBUNGE wa Nzega, Dk.Hamisi Kigwangalla (CCM), anadaiwa kuliibia taifa kwa kutumia vibayamisamaha ya kodi ya mamilioni ya shilingi kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha afyaeneo la Uchama, wilaya ya Nzega.

Kwa mujibu wa nyaraka ambazo Tanzania DaimaJumatano imezipata, Dk. Kigwangallah amejipatia misamaha ya kodi ya ongezeko lathamani na ushuru wake kupitia kampuni ya Emergent Africa Limited, anayoimilikikwa asilimia 78 na Bayoun Kigwangallah ana asilimia 22.

Kupitia kampuni hiyo, mbunge huyo ameingiza nchinibidhaa mbalimbali ambazo badala ya kuzielekeza katika ujenzi, amefungua duka lakuuza vifaa vya ujenzi eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam na nyingine anaziuza kwawafanyabiashara wengine.

Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa kampuni yaEmergent Africa Ltd, ilisajiliwa katika Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC)Septemba 27, 2011 na iliruhusiwa kupata misamaha hiyo kuanzia Septemba 2011hadi Agosti 2014.

Kwa mujibu wa makubaliano kati ya kampuni yaEmergent Afica Ltd na TIC, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliombwa kuisamehekodi kampuni hiyo ya Dk. Kigwangallah vitu mbalimbali vyenye orodha toka namba1 hadi 390.

Bidhaa hizo kwa uchache ni kompyuta 1042,mashine za kutolea kopi 12, printa 12, ‘binding machines' 12, vikokotozi(calculator) 640, projekta 12, video kamera 12, feni 30, vifaa vya simumasanduku 28, jenereta moja, magari aina ya Toyota 13, lori 3, Nissan NavarraPik up 4, Mitsubishi Canter 2 na mabasi madogo manane.

Pamoja na msahama huo, Dk. Kigwangallahkupitia kampuni hiyo, aliingiza nchini vitu bidhaa mbalimbali vikiwemo vigaevya sakafuni 2500 vyenye ukubwa wa 600X600 na 1000 vyenye ukubwa wa 400 X 400pamoja na vigae vya ukutani.

Katika orodha hiyo viko viti na meza za kulia,hema la bustanini, sofa, kabati za kuwekea nguo, mazulia, vitanda na magodoro,televisheni na vingine.

Aidha nyaraka hizo zinaonyesha baada yakupokea bidhaa hizo kutoka nchini China, ziliuzwa katika madukambalimbali ya Kariakoo na vigae vingine kuuzwa kwa mkuu wa wilaya moja mkoaniTanga (hatukumtaja) kwa kuwa hakupatikana kujitetea.

Hata hivyo, kumeonekana utata katika nyakarahizo kwani kampuni ya Delmas iliyosafirisha kontena la bidhaa hizo kuja kwa Dk.Kigwangallah, ziko tofauti na ankaraza malipo.

Ankarahizo zinaonyesha kuwa zilitolewa na makampuni ya Louis Valentino Investment andDevelopment Co. Ltd iliyopo Na. 19 Ji Hua 3 Road Foshan na Sharpeye Furniture.

Wakati manunuzi yakionekana kufanyika ChinaOktoba mosi, 2012, nyaraka nyingine zinaonyesha kuwa mali zilishaingizwa nchini tanguAprili 14 mwaka huo, kupitia kampuni ya Innovative Freight yenye TIN100-145-596, risiti namba 2012/0000002986.

Na nyaraka za mamlaka ya mapato zinaonyeshabidhaa hizo ziliingia nchini Aprili 3 mwaka jana, hali inayoonyesha kupishanakatika tarehe za kununua na kuingiza bidhaa hizo.

Pia utata huohuo unaonekana katika taarifa zaShirika la Viwango Tanzania (TBS) ambazo zinaonyesha bidhaa hizo zilikaguliwaMachi 28, 2012.

Huku kukiwa na orodha zinazotofautiana zamakampuni mawili ya kibiashara wakati ankaraya malipo ilikuwa moja.

Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa kontena hilo lilipofika nchini lilionekana kuwa na vitu tofauti navile vilivyoorodheshwa, hivyo kusababisha kontena hilo kufanyiwa uchunguzi usio wa kawaida kwakupekua mzigo mmoja mmoja.

Dk. Kigwangallah alipotafutwa kwa simukufafanua tuhuma hizo, alisema amebanwa na kazi. Na alipoambiwa ametumiwamaswali kwenye barua pepe yake, aliahadi kujibu lakini hakufanya hivyo.

Alipopigiwa tena jioni, alisema, "Sema harakaunataka nini?" Alipoulizwa juu ya tuhuma hizo alikata simu.

Lakini baadaye aliandika ujumbe kwa simu:"Nitakupigia jioni nikitoka bungeni."

Alipoambiwa inaandikwa habari gazetini,alijibu kwa ujumbe mfupi kuwa tuhuma zilikuwa za uongo bila kufafanua.

Source:
TANZANIA DAIMA
 
nimesoma hoja hii kwa makini lakini nilipoona tanzania daima eti ndiyo chanzo cha taarifa poleni bola nikalale.
 
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
ZeMarcopolo usiwe kipofu hata kwa maambo yaliyo wazi kiasi hiki.
Huyu Dkt. Vitumbua HKigwangalla hajaanza leo kuwaibia watanzania. Aliwahi kuwadhulumu wasukuma wenzake wakulima wa pamba wakati wa financial crunch kupitia kampuni yake nyingine inayoitwa MSK SOLUTIONS.

Aliwadhulumu fedha alizopewa na serikali kwa ajili ya kufidia bei ya pamba iliyokuwa imeporomoka lakini kwa sababu ya ubinafsi wake na kukosa uzalendo akatia ndani fedha yote na wakulima wa pamba wakabaki wakitanga na njia bila msaada wowote kwa hasara kubwa waliyoipata.

Kampuni yake ya MSK SOLUTIONS ilipewa na serikali kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 100 lakini hakuwasaidia chochote wakulima wa pamba zaidi ya kuwadhulumu. Kwahiyo hili la kukwepa kulipa kodi na kuagiza vifaa ambavyo havikuwemo katika orodha ya vitu vinavyopata msamaha kwangu sio nhabari ngeni, ni muendelezo tu wa tabia yake ya wizi.
 
Last edited by a moderator:
Huyu ni yule aliyesema Lisu ni mgonjwa wake au ni mwingine?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
ZeMarcopolo usiwe kipofu hata kwa maambo yaliyo wazi kiasi hiki.
Huyu Dkt. Vitumbua HKigwangalla hajaanza leo kuwaibia watanzania. Aliwahi kuwadhulumu wasukuma wenzake wakulima wa pamba wakati wa financial crunch kupitia kampuni yake nyingine inayoitwa MSK SOLUTIONS.

Huyo charlatan ni Msukuma wa wapi huyo? Maana nijuavyo Nzega iko Tabora na Tabora ni kwa Wanyamwezi.
 
ZeMarcopolo usiwe kipofu hata kwa maambo yaliyo wazi kiasi hiki.
Huyu Dkt. Vitumbua HKigwangalla hajaanza leo kuwaibia watanzania. Aliwahi kuwadhulumu wasukuma wenzake wakulima wa pamba wakati wa financial crunch kupitia kampuni yake nyingine inayoitwa MSK SOLUTIONS.

Aliwadhulumu fedha alizopewa na serikali kwa ajili ya kufidia bei ya pamba iliyokuwa imeporomoka lakini kwa sababu ya ubinafsi wake na kukosa uzalendo akatia ndani fedha yote na wakulima wa pamba wakabaki wakitanga na njia bila msaada wowote kwa hasara kubwa waliyoipata.

Kampuni yake ya MSK SOLUTIONS ilipewa na serikali kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 100 lakini hakuwasaidia chochote wakulima wa pamba zaidi ya kuwadhulumu. Kwahiyo hili la kukwepa kulipa kodi na kuagiza vifaa ambavyo havikuwemo katika orodha ya vitu vinavyopata msamaha kwangu sio nhabari ngeni, ni muendelezo tu wa tabia yake ya wizi.

Mkuu Mwita,

Hicho kiasi ndicho ulichodhamiria kuandoka au keyboard yako imeghafilika?
 
Huyo charlatan ni Msukuma wa wapi huyo? Maana nijuavyo Nzega iko Tabora na Tabora ni kwa Wanyamwezi.

Mkuu Nyani Ngabu ni kweli uraia wa HKigwangalla bado una ukakasi, si tu kwamba ni wa nzega-mnyamwezi kwakuwa hata wanyamwezi wenyewe wanasema ni mrundi. Hata hivyo hoja yangu ni kwamba aliwadhulumu wasukuma (napenda kuwajumuisha wanyamwezi ndani ya wasukuma) kama vile unavyoweza kuwataja wangoreme kuwa ni wakurya wenzangu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom