Kigwangalla: Mange Kimambi uongozi ni kiti cha moto, tunahitaji support sio matusi na lawama

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,104
5,102
Hongera naibu Waziri wa Afya.Hongera kwa kumfuata Mange kwenye page yake na kujibu baadhi ya tuhuma.
Umeeeleza kwa uzuri na naamaini naye amekuelimisha vya kutosha.Hongera Mange kwa kujizuia kutoa tusi ndani ya majadiliano hayo,kwa kweli tukienda hivi angalau watu wataielewa serikali na serikali itazielewa baadhi ya hoja za wapinzani wake.

========

Hamis kigwangalla leo ameamua kufunguka kwa mwanaharakati Mange Kimambi huko Instagram baada ya mwanadada huyo kupost picha na maombi kibao kutoka kwa wananchi wakimwomba awasaidie kufikisha vilio vyao serikalini.

Majibu hayo yamekuja siku chache baada ya mwanadada Mange kufululiza kupost picha na post mbali mbali zikionyesha hali mbaya ya huduma za afya kwenye baadhi ya hospitali zetu.

Nyingi ya post zinaonyesha jinsi wanawake kwenye baadhi ya hospitali kubwa ( including MUHIMBILI ) wakiwa wamelala chini sakafuni na watoto wao baada ya kutoka kujifungua, na baadhi ya post nyingine ni message anazotumiwa na watu mbalimbali wakilalamika jinsi wanavyopata tabu kupata huduma za afya mahospitalini .

Siwezi kuweka post zote hapa ila unaweza pitia kwenye page yake kujionea mwenyewe Mange Kimambi - Instagram

Naibu Waziri amesema wana changamoto nyingi, kila siku zinapatiwa ufumbuzi, lakini pia suluhu ya changamoto moja huzaa changamoto nyingine. alimalizia kwa kumwomba Mange amtumie hizo kesi ili aweze kuzishungulikia.

hamis.png

Maoni yangu : Nampongeza mheshimiwa Naibu waziri, kwa kuona hilo na kuahidi kulifanyia kazi, tunachoomba ni kuwa yasiwe ni maneno tu ya mtandaoni, bali yaende kufanyiwa kazi kweli.

By
RobyMi
 
Hongera naibu Waziri wa Afya.Hongera kwa kumfuata Mange kwenye page yake na kujibu baadhi ya tuhuma.
Umeeeleza kwa uzuri na naamaini naye amekuelimisha vya kutosha.Hongera Mange kwa kujizuia kutoa tusi ndani ya majadiliano hayo,kwa kweli tukienda hivi angalau watu wataielewa serikali na serikali itazielewa baadhi ya hoja za wapinzani wake.

Amshauri na bashite nae akajibu thuhuma....huko huko kwa mange
 
Sidhani kama amejiabisha!!Binafsi nimefurahi alivyoiteteta serikali kwa maelezo mazuri mno.Pia naamini suala la matibabu ndani ya USA limemuingia na leo ataisoma OBAMACARE vizuri.
kwa waziri kwenda kwenye page ya huyo anaetukana serikali na watu binafsi kila siku ni kujiaibisha sana.....mbona kuna watu wa heshima wanaotoa hoja zao vizuri hawajibu anaenda kumjibu Mange....mimi hata kuitembelea tu page yake siwezi
 
Hongera naibu Waziri wa Afya.Hongera kwa kumfuata Mange kwenye page yake na kujibu baadhi ya tuhuma.
Umeeeleza kwa uzuri na naamaini naye amekuelimisha vya kutosha.Hongera Mange kwa kujizuia kutoa tusi ndani ya majadiliano hayo,kwa kweli tukienda hivi angalau watu wataielewa serikali na serikali itazielewa baadhi ya hoja za wapinzani wake.
Ungeweka hata screenshots za majibizano ktk uzi wako.
 
kwa waziri kwenda kwenye page ya huyo chizi anaetukana serikali na watu binafsi kila siku ni kujiaibisha sana.....mbona kuna watu wa heshima wanaotoa hoja zao vizuri hawajibu anaenda kumjibu Mange....mimi hata kuitembelea tu page yake siwezi ni wapumbavu pekee wanaoweza kuingia page ya huyo mwehu
Mind you,Mange ana 1million folowers!!
 
kwa waziri kwenda kwenye page ya huyo chizi anaetukana serikali na watu binafsi kila siku ni kujiaibisha sana.....mbona kuna watu wa heshima wanaotoa hoja zao vizuri hawajibu anaenda kumjibu Mange....mimi hata kuitembelea tu page yake siwezi ni wapumbavu pekee wanaoweza kuingia page ya huyo mwehu
Ukienda milembe utakuta chizi anamwita chizi mwenzake chizi.....na anamuona ni chiz kweli kweli bila kujua na yeye ni chizi pia.....mange ana mazur yake na mabaya yake....no one is 100% perfect.....she knows a lot of things na ana exposure kubwa.......tumshukuru kwa kujitolea kuanika mambo mbalimbali ambayo yanaendelea hapa tz.....asingekuwa yeye sijui tungejuaje.....ukienda kwake chukua unayoona yanakufaa mabaya muachie yeye.
 
Back
Top Bottom