Masaa 48, Maandamano ya Mange yaweza kufanikiwa?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
40,000
magunamange_phixr.png

Na. M. M. Mwanakijiji

Itakuwa ni makosa makubwa kwa watu kupuuzia, kukejeli au kudharau mwamko ambao mwanadada wa Kitanzania anayeishi Marekani Mange Kimambe ameuanzisha, kuuchochea na kuuhamasisha. Mwamko huo unaelekea kilele chake Alhamisi hii tarehe 26 Aprili kwa kile kinachotarajiwa kuwa ni maandamano ya papo kwa papo (impromptu demonstrations) ambayo yanatarajiwa kufanywa sehemu mbalimbali nchini.

Msingi wa Maandamano Haya ni Nini?

Kimsingi maandamano haya yanalenga katika kutaka kutuma ujumbe kwa Rais Magufuli na serikali yake kuwa siyo wananchi wote wanapenda uongozi wake, utawala wake na mwelekeo wa serikali yake. Kwamba, lipo kundi kubwa ambalo limegeuza njia na kwamba na kundi hili linatamani kuona kuwa Serikali ya Magufuli inabadili mwelekeo wake. Mwelekeo ambao kundi hili linadai ni ule unaohusiana na namna serikali inashughulikia uhuru wa maoni, habari, kukutana na haki mbalimbali za kisiasa na kiraia.

Nani Anayemsikiliza na Kumfuata Mange?

Wapo watu wengi wanaoripoti kwenye ukurasa wa Mange – maarufu kama “Da’Mange” – kila siku asubuhi kama watu wanavyoripoti kwenye mstari shuleni au darasani. Wapo ambao wanaweza kuwepo bila kukosa na siku kwao inaanza kwa kuangalia kwanza Mange ameposti kitu gani. Yawezekana kwa mtazamo wangu kuna makundi makubwa manne ambayo yanamfuatilia Mange – mimi niko kwenye kundi mojawapo.

Lipo kundi la kwanza la wenye manung’uniko na malalamiko mbalimbali dhidi ya serikali. Yawezekana kundi hili ni kubwa Zaidi. Kundi hili linahusisha wale wote ambao wanaona kuwa hawana mahali pa kulalamika au kusikilizwa na ambao wanaona kama wametupwa pembeni mwa maslahi ya uongozi wa serikali. Kundi hili linahusisha watu waliobomolewa nyumba zao, walionyang’anywa viwanja vyao, waliofukuzwa kazi, waliofukuzwa kwa tuhuma za kugushi vyeti au elimu, na wale wengine wote ambao wanaona kuwa ujio wa uongozi wa Magufuli umeleta adha katika maisha yao na kuyavuruga.

Hivi majuzi kulikuwa na posti ya mtoto mdogo – labda miaka minne hivi – ambayo baba yake alituma video kwa Mange akionesha jinsi gani mtoto huyo hataki kabisa kusikia jina la Magufuli. Maelezo ambayo mzazi wa mtoto huyo aliyatoa ni kuwa baada ya wao kuvunjiwa nyumba zao Kimara, mtoto huyo anahusisha mahangaiko aliyoyaona kwa wazazi wake kiasi cha kuwa na chuki dhidi ya Magufuli. Mtoto huyo ameonekana kusema kuwa hampendi kabisa Magufuli kwa sababu “amewavunjia” nyumba yao.

Kundi hili la wenye malalamiko na manung’uniko linahusisha watu ambao wako ndani ya serikali, nje ya serikali, wenye kuunga mkono upinzani, na hata wengine nje ya upinzani. NI kundi la walioumizwa na kujeruhiwa – iwe kutokana na maamuzi halali ya kitawala au la kwao haijalishi.

Kuna kundi la pili la wale ambao wao Mange ndio chombo kikubwa cha habari sasa hivi nchini Tanzania. Kwa wale ambao wanatafuta habari za mambo ambayo hayawezi kupostiwa au kuripotiwa kwenye vyombo vya habari vya kawaida Mange ndio chombo chao kikuu cha habari. Wanajua wakienda kwa Mange watapata habari zote zenye ukweli, zenye uongo, na zenye chumvi na pilipili. Wanamfuatilia Mange kwa sababu wanajua Mange hana bodi ya uhariri ambayo inaweza kuzima habari zao.

Ni kwa sababu hiyo utaona watu wanaposti habari za matatizo kwenye hospitali – kama ilivyotokea kule Mwanza Hospitali ya Wilaya, au siku hizi chache kwenye adha ya mafuriko Dar na jinsi ilivyoathiri hali ya usafiri Jijini Dar. Kwa Mange watu wanaweza kupata habari hata za kashfa mbalimbali zinazonukia ndani ya serikali; kashfa ambazo watu wanajua haziwezi kuripotiwa kwenye vyombo vya habari vya kawaida. Mfano mzuri ni suala la malumbano kati ya Mange na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam. Kwa wanaofuatilia, mara baada ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar Bw. Alhad Mussa Salum kuamua kumvaa Mange na kumpiga mkwara wa nguvu. Majibu ya Mange kwenye akaunti yake ya Instagram yalifungua taarifa mbalimbali kuhusiana na Sheikh huyo kiasi cha kufanya watu waone kuwa Mange hakuwa saizi ya Sheikh huyo.

Ukiondoa mfano huo, upo mfano wa mgongano unaoendelea kati ya Mange Kimambi na Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Bw. Paul Makonda. Katika mgongano huo inaoenaka vijana hawa wawili wanapimana nguvu mmoja akitumia ngumu ya mtandao mwingine akitumia nguvu ya ofisi yake. Watu wanafuatilia kwa Mange kuona mnyukano huu utaishia vipi. Kundi hili basi linamfuatilia Mange kama watu wanavyofuatilia CNN; lakini ikiwa na utamu wa magazeti ya udaku kama National Inquirer la Marekani au DailyMail la Uingereza.

Lipo kundi la tatu vile vile. Kundi hili ni la wale ambao hawakubaliani kabisa na Mange Kimambi, hawapendi lugha anayotumia, hawapendi jinsi ambavyo anahamasisha watu wengine na wanaona kuwa anajaribu kuzui kile wanachoamini kuwa kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli. Kundi hili limeonekana kupata nguvu siku za karibuni hasa kufuatia tishio la Maandamano ya Aprili 26. Kundi hili linajitokeza kujibu na hawachelewi kujibu kwa lugha ile ile ya mtaani ambayo imemfanya Mange kuwa maarufu. Kundi hili laweza kuwa linatokana na wanachama watiifu wa CCM, mashabiki wa Magufuli au watu wengine ambao wanaamini maslahi yao yako salama chini ya Magufuli.

Ukubwa wa kundi hili ni vigumu kukisia kwa sababu wakati zipo video mbalimbali za watu wanaojiandaa kuandamana (wengi wao wakiwa ni vijana) Mange haposti video yoyote ambayo inahamasisha kinyume na video hizo nyingine. Hata hivyo, maoni ya wale walioko kinyume anayaacha na hivyo kuonekana yuko ‘fair’ kwa kiasi chake kuliko vyombo vingi vya habari.

Na lipo kundi la nne. Hili ni kundi linaloangalia makundi haya matatu yanavyonyukana. Kundi hili linaangalia kwa karibu madai ya kundi lile la kwanza likisikiliza kwa makini na wakati mwingine kwa huruma (sympathetic) kwa madai yao. Linafuatilia yanayosemwa kwa Mange kama wanavyofanya kundi la pili – kwani nao hawana chombo kingine cha habari kilicho huru. Na kundi hili la nne pia linaangalia majibu yanayotolewa na kundi la tatu. Hata hivyo, kundi hili haligongi “like” halitoi maoni yoyote na halisemi lolote; kazi yake kubwa – na inawezakana ni kundi kubwa Zaidi – ni kuangalia.

Ndani ya kundi hili wapo pia watendaji wa serikali ambao hawataki habari zao zifike kwa “Da Mange” na mara nyingi linakuwa tayari kujibu n ahata kushughulikia malalamiko yanayotolewa kwa Mange kwa mtindo wa “Da Mange ficha my ID”. Ndani ya kundi hili yawezekana wapo wana usalama na watu mbalimbali ambao jukumu lao pia ni kufuatilia nani yuko hasa kwenye kundi la kwanza la wajumbe wa Baraza la Kudumu la Mange. Kazi yake ni kufuatilia na kutoa taarifa kwa vyombo husika. Lakini pia ni kundi ambalo linajali mambo yake; kwa kadiri ya kwamba hawajaandikwa kwa Mange, kundi hili liko salama. Lakini kwa kiasi kikubwa linasoma yote yanayoendelea kwa Mange tena kwa kuripoti kila siku kama lile kundi la kwanza, lakini Zaidi ya hapo halijihusishi moja kwa moja na ushabiki wa upande wowote.

Maandamano ya Aprili 26?

Tukirudi kwenye mwamko wa maandamano, Mange amefanikiwa tayari. Na ipo hatari ya kufanikiwa Zaidi kuliko watu wanavyoweza kudhania. Lakini tukiangalia kwa karibu tunaweza kusema kuwa hadi hivi sasa Mange amefanikiwa kufanya mambo kadhaa ambayo hajayafanikiwa kufanywa hata na viongozi mbalimbali wa upinzani tangu ujio wa mitandao ya kijamii. Kuna mambo kadhaa ambayo naweza kuyaonesha kuwa hata kabla ya Aprili 26 Mange amefanikiwa kuyafanya na ambayo ni ya kutufanya tufikirie mara mbili mwitikio wa serikali uweje Alhamisi hii.

1. Mange amewavutia vijana wa kawaida. Kwa mtu yeyote ambaye amekuwa akifuatilia yanayopostiwa kwa Mange (toka kundi lolote kati ya manne hapo juu) anaweza kuona kuwa kuna hamasa Fulani miongoni mwa vijana wa “kijiweni”. Kundi hili ndio kundi ambalo linaweza kweli “kukianzisha” na “kukinukisha” kwani ni kundi ambalo halina cha kupoteza Zaidi ya maisha yao. Ni kundi la vijana wanaoishi bila kazi, wenye hali ngumu na ambao hata kabla ya Magufuli maisha yao hayakuwa na tofauti.

2. Mange amemfanya Magufuli kuwa hoja. Ukiondoa Tundu Lissu na baadhi ya viongozi wa upinzani ambao wamejitahidi kumuonesha kuwa Magufuli hafai, Mange ameenda mbali Zaidi na kumfanya Rais Magufuli aonekane kama siye mtu anayetaka kweli kuiletea Tanzania mafanikio. Kwamba Mange katika maandishi yake mbalimbali amemfanya Magufuli aonekane kama adui na hivyo kuhamasisha sana kundi lile la kwanza kuwa tayari kujitokeza kuandamana.

3. Mange amepiku kazi ya vyama vya upinzani. Hili ni jambo kubwa sana ambalo linatuonesha pia udhaifu wa vyama vya upinzani katika mazingira ya utawala wa Magufuli. Mange sasa hivi anaweza kuonekana kama ndio Kiongozi wa Upinzani Mtandaoni (UM). Hata wanachama wa upinzani wengi tu n ahata viongozi tayari wamejionesha kwa namna moja au nyingine kuwa ni Wajumbe wa Kudumu Mtandaoni wa Timu Mange (WAKUMTIMA) na wao kama wengine hawakosi kufuatilia kila siku kinachopostiwa na Mange.

4. Mange pamoja na kuvutia “vijana wa kawaida” amevutia pia watumishi ndani ya serikali. Sasa hivi watu wako tayari kumrushia Mange taarifa za kinachoendelea ndani ya serikali – hasa mabaya na wanafanya hivyo wakiamini kabisa kuwa Mange atawalinda. Na kuwalinda Mange anawalinda. Watu hawana imani tena na kutoa taarifa kwenye vyombo rasmi vya uchunguzi kwani hawana uhakika kama watalindwa. Kwa vile tayari baadhi ya watu waliokuwa wakifichua maovu wamejikuta wakikutwa na mkono wa sheria kama waanzilishi wa JamiiForums; watu hawataki tena kujitokeza kama wanaofichua maovu kwani Serikali inaonekana si rafiki yao tena.

Nini Kinaweza Kutokea Alhamisi Aprili 26?

Kwa wale ambao wanafuatilia mwamko wa maandamano ya Mange hadi hivi sasa watakuwa wanajiuliza ni kitu gani kinaweza kutokea siku ya Alhamisi, masaa kama 48 tu kuanzia sasa? Ni mambo gani yanaweza kutokea na mwitikio wa serikali unatakiwa uweje? Naomba kupendekeza kuwa kuna mambo kadhaa yanaweza kutokea siku hiyo. Mambo haya naweza kuyaita kuna “Worst Case Scenario” yaani jambo linalohofiwa kabisa kuweza kutokea na “Best Case Scenario” yaani jambo zuri linaloweza kutokea. Hata hivyo, mambo haya mawili yanaweza kuwa tofauti kwa pande zote mbili; yaani baya la Mange litakuwa zuri kwa Serikali na zuri kwa Serikali linaweza kuwa baya kwa Mange.

JAMBO LA KWANZA: Hakuna Maandamano. Pamoja na kuhamasishana sana siku ile hakuna vijana watakaoamua kukutana kwenye makutano ya barabara, kwenye stendi za mabasi, kwenye njia panda au kwenye vituo ambavyo vimetangazwa na Mange. Kwamba siku ile watu wataenda kwenye sherehe za Muungano na wengine watatulia majumbani kwao na wenye shughuli zao sehemu kubwa ya nchi wataenda na shughuli zao. Hili litakuwa ni jambo jema kwa serikali na kwa Mange litakuwa ni jambo baya na kwa maneno yake mwenyewe kama watu hawatojitokeza kuandamana atakuwa amekatishwa tamaa sana kwani ataona kama Watanzania hawapiganii maslahi na haki zao.

JAMBO LA PILI: Maandamano Yanazimwa Mapema. Katika sehemu mbalimbali ambazo zimetajwa watu kukutana vikosi vya polisi na wana usalama vinaamka na kujipanga kusubiria kuona kama kuna mtu atajitokeza na yeyote atakayeonakana kujitokeza kuandamana atazuiliwa na kusekwa ndani. Uharaka wa kushughulikia wale watakaojitokeza na kusambaa kwa askari (Polisi na JWTZ) kunawatakia hofu waandamani wachache watakaojitokeza na kabla ya kufika saa sita mchana maandamano yanayeyuka. Kwamba, wachache watakuwa wamejitokeza na kutiwa ndani kunaweza kuonesha jinsi serikali haikupuuzia tishio la maandamano haya na hivyo vyombo vya usalama vikapongezwa kwa kuyadhibiti na kupiga mkwara. Maandamano yakayeyuka.

JAMBO LA TATU: Maadamano Yanafanyika Kupewa Ulinzi Hadi Yanamalizika. Vijana kweli wanajitokeza na kuhamasishana kwa nyimbo katika makundi yao mbalimbali na Serikali haiwashughulii kwa kuwatawanya kwa nguvu. Vyombo vya dola vinakuwepo kuhakikisha tu vijana hao hawatishii amani wananchi wengine wala mali zao. Pamoja na hamasa yote, mabango na makusanyiko yote vijana wanafanya maandamano yao na mwisho wa siku wanatawanyika na kumaliza kwa amani. Tatizo la jambo hili ni kuwa lengo la maandamano haya kama mtu anafuatilia kwa Mange siyo tu kuandamana na kutoa malalamiko fulani; Mange amewahamaisha vijana hawa kuandamana ili kushinikiza Rais Magufuli ajiuzulu nafasi yake. Kwa msingi huo, ni vigumu kuona ni kwa namna gani maandamano yenye lengo zito kama hili yanaweza kuisha yenyewe. Wengi wameona maandamano ambayo yamemuondoa Waziri Mkuu wa Armenia na yale yaliyosababisha mabadiliko ya Nikaragua yaondolewe; hili linaweza kuwapa watu hamasa kuwa lengo lao linaweza kufikiwa.

JAMBO LA NNE: Maandamano Yanaanza, Yanazizima na Yanachemka: Hili litategemea kabisa ni kitu gani kinafanyika katika kuzima maandamano yanapoanza. Jambo baya linaloweza kutokea ni polisi au vyombo vya usalama kutumia nguvu na kusababisha mauaji au watu kuumizwa. Kama kutatokea mauaji mahali popote nchini na habari zikaanza kusambaa kunaweza kuwachochea vijana zaidi damu kuchemka na wale wote walioripoti kwa Mange na kuahidi kuwa watajitokeza siku hiyo wakaanza kuhamasishana na kuanza kukimbizana na polisi; wanaweza wakaanza kuharibu vitu na mali na polisi wakajikuta wanalazimika kutumia risasi za moto. Lakini nini kitatokea kama pamoja na watu kuanza kupigwa risasi wakaamua kuendelea kujitokeza kwa wingi siku inavyoendelea? Serikali inaweza kuingiza JWTZ kutuliza vurugu lakini vipi kama mamia zaidi ya vijana wakazidi kujitokeza kwa kadiri siku inavyoendelea na kuelekea jioni ikaonekana hali imeshindwa kudhibitiwa?

JAMBO LA TANO: Yanafanyika Sehemu Moja Yanazimwa Sehemu Nyingine. Mojawapo ya mambo yanayoweza kutokea ni kuwa baadhi ya miji vijana wanafanikiwa kukimbizana na Polisi na kwenye miji mingine yanazimwa mapema kabisa na hivyo yanakuwa yamefanikiwa kidogo na kushindwa upande mwingine. Kwa vile maandamano haya yanatarajiwa kufanyika nchi nzima ni wazi kuwa kushindwa kufanyika katika maeneo mengine itakuwa ni mwisho wake. Hata hivyo, kufanikiwa kwa maandamano haya kunahitaji ni LAZIMA yafanikiwe Dar-es-Salaam. Ni kwa sababu hiyo vyombo vya usalama kwa upande wake vitaweka mkazo mkubwa kuhakikisha kuwa maandamano yanazimika kabla hayajaanza Dar-es-Salaam. Nitaeleza hapa chini juu ya mwitikio wa Serikali.

JAMBO LA SITA: Maandamano Yanachemka na Hayakomi kwa Siku Kadhaa: Hili ndilo “Worst Case Scenario” kwa serikali. Kama vyombo vya usalama vikishindwa kudhibiti na kuzima maandamano ndani ya masaa machache ya mwanzo; na maandamano hayo yakaanza kukolea usiku kucha na siku inayofuatia na katika siku inayofuatia maelefu wakazidi kujitokea basi Serikali ya Magufuli itakuwa matatani. Endapo Jiji la Dar litazizima kweli na shughuli za kila siku zikaathirika kwa kiasi kikubwa na kufanya watu kushindwa kwenda makazini na serikali kuendelea na kazi zake basi yatakuwa ni mafanikio makubwa kwa maandamano ya Mange. Na kama yataendelea kwa siku kadhaa yakitaka mashinikizo mbalimbali kazi kubwa itakuwa ni mwitikio wa Serikali.

Mwitikio wa Serikali Unaweza Kuwaje?

Nimeweza kuonesha mambo yanayoweza kutokea siku ya Alhamisi. Hata hivyo, Serikali ambayo iko madarakani kwa njia halali za kidemokrasia ni wazi itakuwa imejipanga kuchukua hatua mbambali kuhakikisha kuwa utulivu, na usalama unakuwepo hasa kwa vile siku hiyo ni Siku Kuu ya Kitaifa ya Muungano. Je, Serikali inaweza kuchukua hatua gani?

1. KUTUMIA NJIA ZA KITEKNOLOJIA KUZIMA MITANDAO(Internet): Jambo hili linahofiwa siyo na Mange tu bali na watumiaji wengine wa mitandao ya kijamii. Ipo teknolojia inayoweza kutumiwa na TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano) kuweza kuzuia baadhi ya mitandao na hata kuzima upatikanaji wa internet kwa nchi nzima hasa kwa kutumia simu na njia za kawaida za mitandao. Mwaka jana huko Togo serikali ya nchi hiyo ikijaribu kudhibiti mawasiliano ilizima internet na kusababisha upatikanaji wa huduma mbalimbali kuwa wa taratibu sana. Huduma za mitandao na sms ilikuwa haipatikani. Kama hili litatokea Tanzania basi itakuwa imejiunga katika kundi la nchi zaidi ya 50 ambazo kuanzia 2016 zimeweza kuzima internet kwa muda kufuatia matishio ya kisiasa. Baadhi ya nchi za Afrika ambazo zimewahi kutumia hii “kill switch” ni pamoja na Ethiopia, Uganda, Congo, Gambia, Misri, na Morocco. Kwa vile Shirika la Simu la Tanzania lina nguvu kubwa katika kusimamia mawasiliano ya simu kuna uwezekano mkubwa kwa Serikali kuagiza watoa huduma za internet (ISPs) kuzima mitandao yao kwa ajili ya usalama na kwa nchi kama ya kwetu hakuna njia ya kuwazunguka.

2. SERIKALI KUDHIBITI MAANDAMANO: Serikali baada ya kuzima au bila ya kuzima internet inaamua kutumia vyombo vyake vya usalama kuzima maandamano. Na Hili linafanikiwa sehemu kubwa ya nchi na wahusika wake wote ambao watakuwa wamejitokeza wanakamatwa. Kama hadi hivi sasa kamata kamata ya viongozi wakubwa wa upinzani haikusababisha kulipuka kwa maandamano makubwa nina uhakika kukamatwa kwa vijana wachache na kuwekwa ndani hakutasababisha maandamano zaidi.

3. SERIKALI KUAMUA KUSALIMU AMRI (Concessions and compromisse). Kama maandamano yanakuwa makubwa na ambayo yanasababisha kupoteza kwa maisha ya watu na hayaelekei kukoma huku yakisababisha vurugu kubwa nchini hakuna njia nyingine isipokuwa Rais Magufuli ajikute analazimika kuconcede kuwa baadhi ya mabadiliko na hatua alizochukua hazikukubalika kwa wananchi wengi na inabidi abadili mwelekeo. Hivi ndivyo ilivyotokea Armenia na ndivyo ilivyotokea Chile na Nicaragua hivi majuzi. Lakini ni kweli yanahitajika maandamano na vurugu kulazimisha hoja zilizotulia na vichwa vilivyotulia (cooler heads) kutamalaki.

4. SERIKAKALI KUKAZA UZI. Maandamano hata kama ni makubwa kiasi gani si lazima yabadilishe mwelekeo wa Serikali. Rais wa Ufaransa Macron amekuwa katika mgongano na vyama vya wafanyakazi ambavyo vimekuwa na maandamano ya muda kupinga mabadiliko ya masuala ya wastaafu lakini Macron amekaza uzi ule ule na mabadiliko hayo yamepitishwa juzi. Hata Rais Donald Trump anapingwa sana na Wamarekani na watu wamekuwa wakiandamana kila siku na wengine wanakesha nje ya WhiteHouse toka aapishwe lakini anaendelea na mabadiliko yake. Rais Magufuli kama anaamini yuko sahihi na kuwa anaungwa na wengi nchini basi anaweza kuendelea na mabadiliko licha ya kuwepo au kutokuwepo kwa maandamano. Haijalishi watu wangapi wataumia au kuuawa kama yuko sahihi atasimamia anachoamini na ataungwa mkon ona watu wanaomuunga mkono. Hili ndilo ujumbe wa jana wakati akifungua jengo la PSPF huko Dodoma ambapo Makongoro Nyerere amemuambia kupingwa siyo ajabu na atapingwa tu la maana ni kuwa akaze uzi.

Kinachofuatia Ijumaa Aprili 27.

Mwisho wa yote ni kuwa Watanzania wataangalia ni nini kinafuatia baada ya Alhamisi. Je, kutakuwa na maandamano au hakuna. Kama yatakuwepo Aprili 26 yataamkia wapi siku ya Ijumaa. Au yatakuwa ni gumzo la kukebehiwa na wale wote ambao walijitokeza kwa Mange kuonesha kweli wana hasira walikuwa ni sawa na kelele za debe tupu? Je, kama hakutakuwa na maandamano au yakashindwa kufanikiwa na yakapuuzwa kabla siku hata haijaisha na Serikali haikuzima mitandao wala kutumia nguvu kubwa, Mange Kimambi ataweza kuwahamasisha nini tena? Je, watu wataendelea kuripoti mambo mbalimbali au atatafuta siku nyingine au atakuwa na ajenda nyingine?

Maswali Yanayobakia

Vyovyote vile ilivyo, kufanyika au kutokufanyika, kufanikiwa au kutokufanikiwa kwa maandamano ya Mange kunaacha maswali mengi sana kwa wachunguzi wa kisiasa na wananchi wa kawaida. Imekuwaje Mange amejijengea jina kubwa na kuwa tishio la watawala? Imekuwaje, aweze kuaminiwa kuliko vyombo vya serikali? Imekuwaje aweze kuhamasisha watu kiasi hiki kiasi cha watu kuondoa hofu zao mbalimbali? Je, binti huyu akija kuamua kuunga mkono chama fulani wakati uchaguzi mkuu anaweza kuwa na mvuto mkubwa katika kuamua nani anakuwa kiongozi Tanzania? Ikumbukwe kuwa vijana wengi ambao wanajiunga na Mange yawezekana hawajapiga kura bado na watapiga kura zao kwa mara ya kwanza 2020. Je, Mange akilenga kuelekea huko ni nani atazuia wimbi la vijana linalokuja?

Je, Serikali ina namna yoyote ya kuonesha kuwa imejifunza au kuona kuna mambo ya kubadili. Je, Rais Magufuli ambaye amejionesha kuwa hayumbishwi, hatishwi na hapangiwi la kufanya anaweza kuona jambo lolote ambalo anaweza kuwa anapaswa kulifanya tofauti. Je, akifanya hivyo hatokuwa amejionesha udhaifu wake (kwa maoni ya wamoja) au hekima yake (kwa maoni ya wengine)? Je, baada ya Aprili 26, masaa 48 yajayo, ni Tanzania gani iliyoungana tutaenda kuiona? Yawezekana kuwa hadi hivi sasa tayari mambo yameanza kubadilika na Tanzania ile haipo tena na sasa tunaelekea kwenye Tanzania mpya kabisa?

Kama Mange anaamini yuko sahihi kwanini asiendelee na harakati zake licha ya kitakachotokea Aprili 26? Lakini kama damu itamwagika na maandamano yakashindwa au watu wakaumizwa na kujeruhiwa katika kujaribu kuonesha ubabe na serikali Mange atakuwa kwa kiasi gani anawajibika kama “kiongozi” wao? Je, atakubali kubeba lawama zozote zile? Lakini kama Magufuli yuko sahihi na kuwa anaamini mwelekeo wa uongozi wake ndio unaotakiwa na siku hiyo vijana wa Kitanzania wakaumizwa au kujeruhiwa na hata kuuawa, atakuwa tayari kubeba lawama au atazihamisha kwa Mange na wale walioshabikia maandamano hayo na yeye kama Rais atasema kuwa aliwaambia wasimjaribu?

Masaa 48 yajayo yataamua.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
 
In a real sense...HAKUNA CHA MAANDAMANO(Dalili ya mvua ni mawingu kama yangekuwepo kungekuwa na JOTO LA JUU SANA KUFIKIA SASA LAKINI SO FAR mambo yapo kawaida sana).....hapa kitakachofanyika ni VIKUNDI VYA KIHUNI ambavyo tayari vimeishaandaliwa na hawa wapuuzi WALIOPO HAPA NDANI wakiongozwa na HAWA UFIPA NA HATA MANGE nalitambua hili na ndio maana AMEKUWA NA CONFIDENCE SANA.... Serikali inatakiwa kuchunguza sana SAFARI ZA BAADHI YA HAWA VIONGOZI WA ufipa SIKU 20 zilizo pita.....
KINGINE AMBACHO NI KIASHRIA CHA KUFELI KWA HAYA MAANDAMNO, hili jianamke chafu lilitisha wito wa KUKUSANYA SAINI kuzipeleka UMOJA WA MATAIFA kamwe hajawahi RUDISHA MREJESHO WA ALIPOFIKIA KWENYE HILI.....
 
maandamano nyuma ya keyboard!! kama walishindwa na kunywea kwenye UKUTA.. hii ni sanaa na maigizo kama kawaida. Hakuna mtanzania mwenye nia njema na nchi hii atakayekubali kudanywa na hila za mange. Watanzani sasa hivi ni waelewa, angalia arusha ilivyo shwari baada ya Lema kukaa sawa. Kipindi cha nyuma hadi watalii walikuwa wanaogopa kuja kwa ajili ya vurugu za Arusha. Mwenye akili hawezi kukubali Ulaghai wa chadema kupitia poyoyo wao Mange.
 
Nakutumia code number itumie after 47 hrs ok

Swissme
 
It is official, Mange anaendesha serikali ya jamhuri ya Tanzania de facto president in absentia! Using the social media! It is sad na hapa ndio tumefikia!

Mwanakijiji you seems to agree she is valid, rightfully so, Sema maneno mengi kama chiruki punguza, I only read two paragraph of your long winded essay, and know what’s exactly in context what you are leading up to! Pumbuza please! This isn’t newspaper!

Cut to the chase!

Si umemuona Rais, he is panicking in calling the deposition of social media including our beloved Jamii forum!

The question is, who do we have to trust and lead us foward “nchi ya viwanda”

Magu or Mange!

I wouldn’t want either, but up to now I give Mange an upper hand!

What is your thought?!
 
In a real sense...HAKUNA CHA MAANDAMANO(Dalili ya mvua ni mawingu kama yangekuwepo kungekuwa na JOTO LA JUU SANA KUFIKIA SASA).....hapa kitakachofanyika ni VIKUNDI VYA KIHUNI ambavyo tayari vimeishaandaliwa na hawa wapuuzi WALIOPO HAPA NDANI.....
Mf

256 arusha wamejiandikisha only kijenge ya juu from yesterday

Swissme
 
Yaani kuna makalio humu naona mnaandika ati CCM damu, CDM damu, pumbavu.
Tatizo ni Pombe na Bashite, tatizo sio chama, naamini chama chochote kina watu wazuri na wabovu, shida yangu ni watu kufukuzwa kwa sababu ya vyeti alafu moja akawa special case akaachiwa huku ni wazi kabisa alifoji kila kitu, hadi identity yenyewe sio ya kwake. Hii ni double standard ya kipumbavu. Hili sio swala la chama, ni tatizo la pombe.

Bashite anaenda radio station kuwalazimisha kutangaza uongo kumsakizia gwajima alafu Nape anaweka tume kufuatilia anafukuzwa, pombe kwa nini anamlinda sana bashite kiasi hicho?

Tatizo jingine ni upumbavu kua ukiongea chochote ambacho pombe hakipendi hata kama ni ukweli basi unaitwa mchochezi, wiki inayofuata umelala polisi, au umekamatwa na watu wasiojulikana au umeitwa uhamisho kukaguliwa uraia. Hili sio tatizo la chama, hili ni tatizo la pombe.

Mi nashangaa watu mnakaa kuleta ushabiki wa kijinga, wengi wenu maskini hamna kitu ila mko mstari wa mbele kumtetea mjinga, akisema tu mniombee, ohh mungu mungu nyambafu zenu mnahisi kashushwa kweli, pombe ni sweet talker yule jamaa, ana maneno sana ila any smart guy ataona amejaa chuki, visasi, ubinafsi, very arrogant, misifa kibao, alafu anaamini conspiracy theories, he is the worst, yaani level moja na Iddi Amin au Kim Jeong Eun.

Sasa hivi kupublish online content hadi ulipie $1000 kwa mwaka, anaua maendeleo, no tech company will develop sasa hivi in Tanzania kwa style hii, yaani mimi mtanzania, nimeenda kuishi nje, serikali ambayo sio yangu ikanipa msaada wa pesa, nikafungua kampuni huko nje, nikawaingizia pesa, nikatoa ajira, alafu narudi bongo serikali yetu badala ya kufanya kitu hicho hicho kuinua companies bongo inaanza kuweka restrictions za kipumbavu, mara ulipie hiki mara kile, wakijua wazi 99% hawatoweza lipia, unaua biashara kabla hata hazijaanza sababu tu ya ego, hutaki kuambiwa kitu negative. Arsehole.

Ovyo sana lile dingi pamoja na mawaziri wake, bashite na mwakyembe ovyo number 2.
 
Haya maandamano nayaangalia tofauti sana, kwa mujibu wa Mange, tareh 26 April ni uzinduzi. Kitakachoendelea ni ugaidi mtupu kwa kila fursa itakapopatikana, hivyo sio jambo la kupuuzia. Mipanga ya kijinga kinga kama hii inaweza kutuondolea utulivu na amani kabisa na tukaja kujuta kama taifa.

Tuombe Mungu sana mambo yaishe baada ya tar 26, la sivyo mitaani kunaweza kusikalike na ikawa ni vita ya jirani na jirani mtaa kwa mtaa na ndiyo ukawa mwanzo wa vurugu. Hivyo basi nashauri ifuatavyo:
1. Vyombo vya dola vitumie busara sana siku ya tar 26, katika kuzima maandamano hayo. Vijitenge kabisa na aina yoyote ya kuchochea hasira za waandamanaji na za wananchi ambao hawataandamana. Hapa namaanisha kuwa watumie nguvu za kadri.
2. Waandamananji watumie njia mbadala ya kuwasilisha kero zao badala yamaandamano ili kuepusha taharuki katika taifa,
3. Viongozi wasikilize maoni ya wanachi na hii tabia ya kudharau maoni yao au kuzuia kabisa kutoa maoni na kukosoa watalawa ni ushamba wa kiungozi na haikubaliki popote
4. Wako baadhi ya viongozi wameteuliwa kutawala mikoa na wilaya lakn wamelalamikiwa na wananchi huku wenye mamlaka wakiwakebehi hao wananchi na kuwaacha watawaliwe kwa nguvu hata kama hawapendi. Mambo kama haya yanaleta hasira na chuki kuu vifuani mwa wanachi

Mwisho ikumbukwe kuwa wanachi ndiyo waajiri wakuu wa Serikali iliyoko madarani hivyo wasilikilizwe sana.

Ngile.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Itakuwa ni makosa makubwa kwa watu kupuuzia, kukejeli au kudharau mwamko ambao mwanadada wa Kitanzania anayeishi Marekani Mange Kimambe ameuanzisha, kuuchochea na kuuhamasisha. Mwamko huo unaelekea kilele chake Alhamisi hii tarehe 26 Aprili kwa kile kinachotarajiwa kuwa ni maandamano ya papo kwa papo (impromptu demonstrations) ambayo yanatarajiwa kufanywa sehemu mbalimbali nchini.

Msingi wa Maandamano Haya ni Nini?

Kimsingi maandamano haya yanalenga katika kutaka kutuma ujumbe kwa Rais Magufuli na serikali yake kuwa siyo wananchi wote wanapenda uongozi wake, utawala wake na mwelekeo wa serikali yake. Kwamba, lipo kundi kubwa ambalo limegeuza njia na kwamba na kundi hili linatamani kuona kuwa Serikali ya Magufuli inabadili mwelekeo wake. Mwelekeo ambao kundi hili linadai ni ule unaohusiana na namna serikali inashughulikia uhuru wa maoni, habari, kukutana na haki mbalimbali za kisiasa na kiraia.

Nani Anayemsikiliza na Kumfuata Mange?

Wapo watu wengi wanaoripoti kwenye ukurasa wa Mange – maarufu kama “Da’Mange” – kila siku asubuhi kama watu wanavyoripoti kwenye mstari shuleni au darasani. Wapo ambao wanaweza kuwepo bila kukosa na siku kwao inaanza kwa kuangalia kwanza Mange ameposti kitu gani. Yawezekana kwa mtazamo wangu kuna makundi makubwa manne ambayo yanamfuatilia Mange – mimi niko kwenye kundi mojawapo.

Lipo kundi la kwanza la wenye manung’uniko na malalamiko mbalimbali dhidi ya serikali. Yawezekana kundi hili ni kubwa Zaidi. Kundi hili linahusisha wale wote ambao wanaona kuwa hawana mahali pa kulalamika au kusikilizwa na ambao wanaona kama wametupwa pembeni mwa maslahi ya uongozi wa serikali. Kundi hili linahusisha watu waliobomolewa nyumba zao, walionyang’anywa viwanja vyao, waliofukuzwa kazi, waliofukuzwa kwa tuhuma za kugushi vyeti au elimu, na wale wengine wote ambao wanaona kuwa ujio wa uongozi wa Magufuli umeleta adha katika maisha yao na kuyavuruga.

Hivi majuzi kulikuwa na posti ya mtoto mdogo – labda miaka minne hivi – ambayo baba yake alituma video kwa Mange akionesha jinsi gani mtoto huyo hataki kabisa kusikia jina la Magufuli. Maelezo ambayo mzazi wa mtoto huyo aliyatoa ni kuwa baada ya wao kuvunjiwa nyumba zao Kimara, mtoto huyo anahusisha mahangaiko aliyoyaona kwa wazazi wake kiasi cha kuwa na chuki dhidi ya Magufuli. Mtoto huyo ameonekana kusema kuwa hampendi kabisa Magufuli kwa sababu “amewavunjia” nyumba yao.

Kundi hili la wenye malalamiko na manung’uniko linahusisha watu ambao wako ndani ya serikali, nje ya serikali, wenye kuunga mkono upinzani, na hata wengine nje ya upinzani. NI kundi la walioumizwa na kujeruhiwa – iwe kutokana na maamuzi halali ya kitawala au la kwao haijalishi.

Kuna kundi la pili la wale ambao wao Mange ndio chombo kikubwa cha habari sasa hivi nchini Tanzania. Kwa wale ambao wanatafuta habari za mambo ambayo hayawezi kupostiwa au kuripotiwa kwenye vyombo vya habari vya kawaida Mange ndio chombo chao kikuu cha habari. Wanajua wakienda kwa Mange watapata habari zote zenye ukweli, zenye uongo, na zenye chumvi na pilipili. Wanamfuatilia Mange kwa sababu wanajua Mange hana bodi ya uhariri ambayo inaweza kuzima habari zao.

Ni kwa sababu hiyo utaona watu wanaposti habari za matatizo kwenye hospitali – kama ilivyotokea kule Mwanza Hospitali ya Wilaya, au siku hizi chache kwenye adha ya mafuriko Dar na jinsi ilivyoathiri hali ya usafiri Jijini Dar. Kwa Mange watu wanaweza kupata habari hata za kashfa mbalimbali zinazonukia ndani ya serikali; kashfa ambazo watu wanajua haziwezi kuripotiwa kwenye vyombo vya habari vya kawaida. Mfano mzuri ni suala la malumbano kati ya Mange na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam. Kwa wanaofuatilia, mara baada ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar Bw. Alhad Mussa Salum kuamua kumvaa Mange na kumpiga mkwara wa nguvu. Majibu ya Mange kwenye akaunti yake ya Instagram yalifungua taarifa mbalimbali kuhusiana na Sheikh huyo kiasi cha kufanya watu waone kuwa Mange hakuwa saizi ya Sheikh huyo.

Ukiondoa mfano huo, upo mfano wa mgongano unaoendelea kati ya Mange Kimambi na Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Bw. Paul Makonda. Katika mgongano huo inaoenaka vijana hawa wawili wanapimana nguvu mmoja akitumia ngumu ya mtandao mwingine akitumia nguvu ya ofisi yake. Watu wanafuatilia kwa Mange kuona mnyukano huu utaishia vipi. Kundi hili basi linamfuatilia Mange kama watu wanavyofuatilia CNN; lakini ikiwa na utamu wa magazeti ya udaku kama National Inquirer la Marekani au DailyMail la Uingereza.

Lipo kundi la tatu vile vile. Kundi hili ni la wale ambao hawakubaliani kabisa na Mange Kimambi, hawapendi lugha anayotumia, hawapendi jinsi ambavyo anahamasisha watu wengine na wanaona kuwa anajaribu kuzui kile wanachoamini kuwa kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli. Kundi hili limeonekana kupata nguvu siku za karibuni hasa kufuatia tishio la Maandamano ya Aprili 26. Kundi hili linajitokeza kujibu na hawachelewi kujibu kwa lugha ile ile ya mtaani ambayo imemfanya Mange kuwa maarufu. Kundi hili laweza kuwa linatokana na wanachama watiifu wa CCM, mashabiki wa Magufuli au watu wengine ambao wanaamini maslahi yao yako salama chini ya Magufuli.

Ukubwa wa kundi hili ni vigumu kukisia kwa sababu wakati zipo video mbalimbali za watu wanaojiandaa kuandamana (wengi wao wakiwa ni vijana) Mange haposti video yoyote ambayo inahamasisha kinyume na video hizo nyingine. Hata hivyo, maoni ya wale walioko kinyume anayaacha na hivyo kuonekana yuko ‘fair’ kwa kiasi chake kuliko vyombo vingi vya habari.

Na lipo kundi la nne. Hili ni kundi linaloangalia makundi haya matatu yanavyonyukana. Kundi hili linaangalia kwa karibu madai ya kundi lile la kwanza likisikiliza kwa makini na wakati mwingine kwa huruma (sympathetic) kwa madai yao. Linafuatilia yanayosemwa kwa Mange kama wanavyofanya kundi la pili – kwani nao hawana chombo kingine cha habari kilicho huru. Na kundi hili la nne pia linaangalia majibu yanayotolewa na kundi la tatu. Hata hivyo, kundi hili haligongi “like” halitoi maoni yoyote na halisemi lolote; kazi yake kubwa – na inawezakana ni kundi kubwa Zaidi – ni kuangalia.

Ndani ya kundi hili wapo pia watendaji wa serikali ambao hawataki habari zao zifike kwa “Da Mange” na mara nyingi linakuwa tayari kujibu n ahata kushughulikia malalamiko yanayotolewa kwa Mange kwa mtindo wa “Da Mange ficha my ID”. Ndani ya kundi hili yawezekana wapo wana usalama na watu mbalimbali ambao jukumu lao pia ni kufuatilia nani yuko hasa kwenye kundi la kwanza la wajumbe wa Baraza la Kudumu la Mange. Kazi yake ni kufuatilia na kutoa taarifa kwa vyombo husika. Lakini pia ni kundi ambalo linajali mambo yake; kwa kadiri ya kwamba hawajaandikwa kwa Mange, kundi hili liko salama. Lakini kwa kiasi kikubwa linasoma yote yanayoendelea kwa Mange tena kwa kuripoti kila siku kama lile kundi la kwanza, lakini Zaidi ya hapo halijihusishi moja kwa moja na ushabiki wa upande wowote.

Maandamano ya Aprili 26?

Tukirudi kwenye mwamko wa maandamano, Mange amefanikiwa tayari. Na ipo hatari ya kufanikiwa Zaidi kuliko watu wanavyoweza kudhania. Lakini tukiangalia kwa karibu tunaweza kusema kuwa hadi hivi sasa Mange amefanikiwa kufanya mambo kadhaa ambayo hajayafanikiwa kufanywa hata na viongozi mbalimbali wa upinzani tangu ujio wa mitandao ya kijamii. Kuna mambo kadhaa ambayo naweza kuyaonesha kuwa hata kabla ya Aprili 26 Mange amefanikiwa kuyafanya na ambayo ni ya kutufanya tufikirie mara mbili mwitikio wa serikali uweje Alhamisi hii.

1. Mange amewavutia vijana wa kawaida. Kwa mtu yeyote ambaye amekuwa akifuatilia yanayopostiwa kwa Mange (toka kundi lolote kati ya manne hapo juu) anaweza kuona kuwa kuna hamasa Fulani miongoni mwa vijana wa “kijiweni”. Kundi hili ndio kundi ambalo linaweza kweli “kukianzisha” na “kukinukisha” kwani ni kundi ambalo halina cha kupoteza Zaidi ya maisha yao. Ni kundi la vijana wanaoishi bila kazi, wenye hali ngumu na ambao hata kabla ya Magufuli maisha yao hayakuwa na tofauti.

2. Mange amemfanya Magufuli kuwa hoja. Ukiondoa Tundu Lissu na baadhi ya viongozi wa upinzani ambao wamejitahidi kumuonesha kuwa Magufuli hafai, Mange ameenda mbali Zaidi na kumfanya Rais Magufuli aonekane kama siye mtu anayetaka kweli kuiletea Tanzania mafanikio. Kwamba Mange katika maandishi yake mbalimbali amemfanya Magufuli aonekane kama adui na hivyo kuhamasisha sana kundi lile la kwanza kuwa tayari kujitokeza kuandamana.

3. Mange amepiku kazi ya vyama vya upinzani. Hili ni jambo kubwa sana ambalo linatuonesha pia udhaifu wa vyama vya upinzani katika mazingira ya utawala wa Magufuli. Mange sasa hivi anaweza kuonekana kama ndio Kiongozi wa Upinzani Mtandaoni (UM). Hata wanachama wa upinzani wengi tu n ahata viongozi tayari wamejionesha kwa namna moja au nyingine kuwa ni Wajumbe wa Kudumu Mtandaoni wa Timu Mange (WAKUMTIMA) na wao kama wengine hawakosi kufuatilia kila siku kinachopostiwa na Mange.

4. Mange pamoja na kuvutia “vijana wa kawaida” amevutia pia watumishi ndani ya serikali. Sasa hivi watu wako tayari kumrushia Mange taarifa za kinachoendelea ndani ya serikali – hasa mabaya na wanafanya hivyo wakiamini kabisa kuwa Mange atawalinda. Na kuwalinda Mange anawalinda. Watu hawana imani tena na kutoa taarifa kwenye vyombo rasmi vya uchunguzi kwani hawana uhakika kama watalindwa. Kwa vile tayari baadhi ya watu waliokuwa wakifichua maovu wamejikuta wakikutwa na mkono wa sheria kama waanzilishi wa JamiiForums; watu hawataki tena kujitokeza kama wanaofichua maovu kwani Serikali inaonekana si rafiki yao tena.

Nini Kinaweza Kutokea Alhamisi Aprili 26?

Kwa wale ambao wanafuatilia mwamko wa maandamano ya Mange hadi hivi sasa watakuwa wanajiuliza ni kitu gani kinaweza kutokea siku ya Alhamisi, masaa kama 48 tu kuanzia sasa? Ni mambo gani yanaweza kutokea na mwitikio wa serikali unatakiwa uweje? Naomba kupendekeza kuwa kuna mambo kadhaa yanaweza kutokea siku hiyo. Mambo haya naweza kuyaita kuna “Worst Case Scenario” yaani jambo linalohofiwa kabisa kuweza kutokea na “Best Case Scenario” yaani jambo zuri linaloweza kutokea. Hata hivyo, mambo haya mawili yanaweza kuwa tofauti kwa pande zote mbili; yaani baya la Mange litakuwa zuri kwa Serikali na zuri kwa Serikali linaweza kuwa baya kwa Mange.

JAMBO LA KWANZA: Hakuna Maandamano. Pamoja na kuhamasishana sana siku ile hakuna vijana watakaoamua kukutana kwenye makutano ya barabara, kwenye stendi za mabasi, kwenye njia panda au kwenye vituo ambavyo vimetangazwa na Mange. Kwamba siku ile watu wataenda kwenye sherehe za Muungano na wengine watatulia majumbani kwao na wenye shughuli zao sehemu kubwa ya nchi wataenda na shughuli zao. Hili litakuwa ni jambo jema kwa serikali na kwa Mange litakuwa ni jambo baya na kwa maneno yake mwenyewe kama watu hawatojitokeza kuandamana atakuwa amekatishwa tamaa sana kwani ataona kama Watanzania hawapiganii maslahi na haki zao.

JAMBO LA PILI: Maandamano Yanazimwa Mapema. Katika sehemu mbalimbali ambazo zimetajwa watu kukutana vikosi vya polisi na wana usalama vinaamka na kujipanga kusubiria kuona kama kuna mtu atajitokeza na yeyote atakayeonakana kujitokeza kuandamana atazuiliwa na kusekwa ndani. Uharaka wa kushughulikia wale watakaojitokeza na kusambaa kwa askari (Polisi na JWTZ) kunawatakia hofu waandamani wachache watakaojitokeza na kabla ya kufika saa sita mchana maandamano yanayeyuka. Kwamba, wachache watakuwa wamejitokeza na kutiwa ndani kunaweza kuonesha jinsi serikali haikupuuzia tishio la maandamano haya na hivyo vyombo vya usalama vikapongezwa kwa kuyadhibiti na kupiga mkwara. Maandamano yakayeyuka.

JAMBO LA TATU: Maadamano Yanafanyika Kupewa Ulinzi Hadi Yanamalizika. Vijana kweli wanajitokeza na kuhamasishana kwa nyimbo katika makundi yao mbalimbali na Serikali haiwashughulii kwa kuwatawanya kwa nguvu. Vyombo vya dola vinakuwepo kuhakikisha tu vijana hao hawatishii amani wananchi wengine wala mali zao. Pamoja na hamasa yote, mabango na makusanyiko yote vijana wanafanya maandamano yao na mwisho wa siku wanatawanyika na kumaliza kwa amani. Tatizo la jambo hili ni kuwa lengo la maandamano haya kama mtu anafuatilia kwa Mange siyo tu kuandamana na kutoa malalamiko fulani; Mange amewahamaisha vijana hawa kuandamana ili kushinikiza Rais Magufuli ajiuzulu nafasi yake. Kwa msingi huo, ni vigumu kuona ni kwa namna gani maandamano yenye lengo zito kama hili yanaweza kuisha yenyewe. Wengi wameona maandamano ambayo yamemuondoa Waziri Mkuu wa Armenia na yale yaliyosababisha mabadiliko ya Nikaragua yaondolewe; hili linaweza kuwapa watu hamasa kuwa lengo lao linaweza kufikiwa.

JAMBO LA NNE: Maandamano Yanaanza, Yanazizima na Yanachemka: Hili litategemea kabisa ni kitu gani kinafanyika katika kuzima maandamano yanapoanza. Jambo baya linaloweza kutokea ni polisi au vyombo vya usalama kutumia nguvu na kusababisha mauaji au watu kuumizwa. Kama kutatokea mauaji mahali popote nchini na habari zikaanza kusambaa kunaweza kuwachochea vijana zaidi damu kuchemka na wale wote walioripoti kwa Mange na kuahidi kuwa watajitokeza siku hiyo wakaanza kuhamasishana na kuanza kukimbizana na polisi; wanaweza wakaanza kuharibu vitu na mali na polisi wakajikuta wanalazimika kutumia risasi za moto. Lakini nini kitatokea kama pamoja na watu kuanza kupigwa risasi wakaamua kuendelea kujitokeza kwa wingi siku inavyoendelea? Serikali inaweza kuingiza JWTZ kutuliza vurugu lakini vipi kama mamia zaidi ya vijana wakazidi kujitokeza kwa kadiri siku inavyoendelea na kuelekea jioni ikaonekana hali imeshindwa kudhibitiwa?

JAMBO LA TANO: Yanafanyika Sehemu Moja Yanazimwa Sehemu Nyingine. Mojawapo ya mambo yanayoweza kutokea ni kuwa baadhi ya miji vijana wanafanikiwa kukimbizana na Polisi na kwenye miji mingine yanazimwa mapema kabisa na hivyo yanakuwa yamefanikiwa kidogo na kushindwa upande mwingine. Kwa vile maandamano haya yanatarajiwa kufanyika nchi nzima ni wazi kuwa kushindwa kufanyika katika maeneo mengine itakuwa ni mwisho wake. Hata hivyo, kufanikiwa kwa maandamano haya kunahitaji ni LAZIMA yafanikiwe Dar-es-Salaam. Ni kwa sababu hiyo vyombo vya usalama kwa upande wake vitaweka mkazo mkubwa kuhakikisha kuwa maandamano yanazimika kabla hayajaanza Dar-es-Salaam. Nitaeleza hapa chini juu ya mwitikio wa Serikali.

JAMBO LA SITA: Maandamano Yanachemka na Hayakomi kwa Siku Kadhaa: Hili ndilo “Worst Case Scenario” kwa serikali. Kama vyombo vya usalama vikishindwa kudhibiti na kuzima maandamano ndani ya masaa machache ya mwanzo; na maandamano hayo yakaanza kukolea usiku kucha na siku inayofuatia na katika siku inayofuatia maelefu wakazidi kujitokea basi Serikali ya Magufuli itakuwa matatani. Endapo Jiji la Dar litazizima kweli na shughuli za kila siku zikaathirika kwa kiasi kikubwa na kufanya watu kushindwa kwenda makazini na serikali kuendelea na kazi zake basi yatakuwa ni mafanikio makubwa kwa maandamano ya Mange. Na kama yataendelea kwa siku kadhaa yakitaka mashinikizo mbalimbali kazi kubwa itakuwa ni mwitikio wa Serikali.

Mwitikio wa Serikali Unaweza Kuwaje?

Nimeweza kuonesha mambo yanayoweza kutokea siku ya Alhamisi. Hata hivyo, Serikali ambayo iko madarakani kwa njia halali za kidemokrasia ni wazi itakuwa imejipanga kuchukua hatua mbambali kuhakikisha kuwa utulivu, na usalama unakuwepo hasa kwa vile siku hiyo ni Siku Kuu ya Kitaifa ya Muungano. Je, Serikali inaweza kuchukua hatua gani?

1. KUTUMIA NJIA ZA KITEKNOLOJIA KUZIMA MITANDAO(Internet): Jambo hili linahofiwa siyo na Mange tu bali na watumiaji wengine wa mitandao ya kijamii. Ipo teknolojia inayoweza kutumiwa na TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano) kuweza kuzuia baadhi ya mitandao na hata kuzima upatikanaji wa internet kwa nchi nzima hasa kwa kutumia simu na njia za kawaida za mitandao. Mwaka jana huko Togo serikali ya nchi hiyo ikijaribu kudhibiti mawasiliano ilizima internet na kusababisha upatikanaji wa huduma mbalimbali kuwa wa taratibu sana. Huduma za mitandao na sms ilikuwa haipatikani. Kama hili litatokea Tanzania basi itakuwa imejiunga katika kundi la nchi zaidi ya 50 ambazo kuanzia 2016 zimeweza kuzima internet kwa muda kufuatia matishio ya kisiasa. Baadhi ya nchi za Afrika ambazo zimewahi kutumia hii “kill switch” ni pamoja na Ethiopia, Uganda, Congo, Gambia, Misri, na Morocco. Kwa vile Shirika la Simu la Tanzania lina nguvu kubwa katika kusimamia mawasiliano ya simu kuna uwezekano mkubwa kwa Serikali kuagiza watoa huduma za internet (ISPs) kuzima mitandao yao kwa ajili ya usalama na kwa nchi kama ya kwetu hakuna njia ya kuwazunguka.

2. SERIKALI KUDHIBITI MAANDAMANO: Serikali baada ya kuzima au bila ya kuzima internet inaamua kutumia vyombo vyake vya usalama kuzima maandamano. Na Hili linafanikiwa sehemu kubwa ya nchi na wahusika wake wote ambao watakuwa wamejitokeza wanakamatwa. Kama hadi hivi sasa kamata kamata ya viongozi wakubwa wa upinzani haikusababisha kulipuka kwa maandamano makubwa nina uhakika kukamatwa kwa vijana wachache na kuwekwa ndani hakutasababisha maandamano zaidi.

3. SERIKALI KUAMUA KUSALIMU AMRI (Concessions and compromisse). Kama maandamano yanakuwa makubwa na ambayo yanasababisha kupoteza kwa maisha ya watu na hayaelekei kukoma huku yakisababisha vurugu kubwa nchini hakuna njia nyingine isipokuwa Rais Magufuli ajikute analazimika kuconcede kuwa baadhi ya mabadiliko na hatua alizochukua hazikukubalika kwa wananchi wengi na inabidi abadili mwelekeo. Hivi ndivyo ilivyotokea Armenia na ndivyo ilivyotokea Chile na Nicaragua hivi majuzi. Lakini ni kweli yanahitajika maandamano na vurugu kulazimisha hoja zilizotulia na vichwa vilivyotulia (cooler heads) kutamalaki.

4. SERIKAKALI KUKAZA UZI. Maandamano hata kama ni makubwa kiasi gani si lazima yabadilishe mwelekeo wa Serikali. Rais wa Ufaransa Macron amekuwa katika mgongano na vyama vya wafanyakazi ambavyo vimekuwa na maandamano ya muda kupinga mabadiliko ya masuala ya wastaafu lakini Macron amekaza uzi ule ule na mabadiliko hayo yamepitishwa juzi. Hata Rais Donald Trump anapingwa sana na Wamarekani na watu wamekuwa wakiandamana kila siku na wengine wanakesha nje ya WhiteHouse toka aapishwe lakini anaendelea na mabadiliko yake. Rais Magufuli kama anaamini yuko sahihi na kuwa anaungwa na wengi nchini basi anaweza kuendelea na mabadiliko licha ya kuwepo au kutokuwepo kwa maandamano. Haijalishi watu wangapi wataumia au kuuawa kama yuko sahihi atasimamia anachoamini na ataungwa mkon ona watu wanaomuunga mkono. Hili ndilo ujumbe wa jana wakati akifungua jengo la PSPF huko Dodoma ambapo Makongoro Nyerere amemuambia kupingwa siyo ajabu na atapingwa tu la maana ni kuwa akaze uzi.

Kinachofuatia Ijumaa Aprili 27.

Mwisho wa yote ni kuwa Watanzania wataangalia ni nini kinafuatia baada ya Alhamisi. Je, kutakuwa na maandamano au hakuna. Kama yatakuwepo Aprili 26 yataamkia wapi siku ya Ijumaa. Au yatakuwa ni gumzo la kukebehiwa na wale wote ambao walijitokeza kwa Mange kuonesha kweli wana hasira walikuwa ni sawa na kelele za debe tupu? Je, kama hakutakuwa na maandamano au yakashindwa kufanikiwa na yakapuuzwa kabla siku hata haijaisha na Serikali haikuzima mitandao wala kutumia nguvu kubwa, Mange Kimambi ataweza kuwahamasisha nini tena? Je, watu wataendelea kuripoti mambo mbalimbali au atatafuta siku nyingine au atakuwa na ajenda nyingine?

Maswali Yanayobakia

Vyovyote vile ilivyo, kufanyika au kutokufanyika, kufanikiwa au kutokufanikiwa kwa maandamano ya Mange kunaacha maswali mengi sana kwa wachunguzi wa kisiasa na wananchi wa kawaida. Imekuwaje Mange amejijengea jina kubwa na kuwa tishio la watawala? Imekuwaje, aweze kuaminiwa kuliko vyombo vya serikali? Imekuwaje aweze kuhamasisha watu kiasi hiki kiasi cha watu kuondoa hofu zao mbalimbali? Je, binti huyu akija kuamua kuunga mkono chama fulani wakati uchaguzi mkuu anaweza kuwa na mvuto mkubwa katika kuamua nani anakuwa kiongozi Tanzania? Ikumbukwe kuwa vijana wengi ambao wanajiunga na Mange yawezekana hawajapiga kura bado na watapiga kura zao kwa mara ya kwanza 2020. Je, Mange akilenga kuelekea huko ni nani atazuia wimbi la vijana linalokuja?

Je, Serikali ina namna yoyote ya kuonesha kuwa imejifunza au kuona kuna mambo ya kubadili. Je, Rais Magufuli ambaye amejionesha kuwa hayumbishwi, hatishwi na hapangiwi la kufanya anaweza kuona jambo lolote ambalo anaweza kuwa anapaswa kulifanya tofauti. Je, akifanya hivyo hatokuwa amejionesha udhaifu wake (kwa maoni ya wamoja) au hekima yake (kwa maoni ya wengine)? Je, baada ya Aprili 26, masaa 48 yajayo, ni Tanzania gani iliyoungana tutaenda kuiona? Yawezekana kuwa hadi hivi sasa tayari mambo yameanza kubadilika na Tanzania ile haipo tena na sasa tunaelekea kwenye Tanzania mpya kabisa?

Kama Mange anaamini yuko sahihi kwanini asiendelee na harakati zake licha ya kitakachotokea Aprili 26? Lakini kama damu itamwagika na maandamano yakashindwa au watu wakaumizwa na kujeruhiwa katika kujaribu kuonesha ubabe na serikali Mange atakuwa kwa kiasi gani anawajibika kama “kiongozi” wao? Je, atakubali kubeba lawama zozote zile? Lakini kama Magufuli yuko sahihi na kuwa anaamini mwelekeo wa uongozi wake ndio unaotakiwa na siku hiyo vijana wa Kitanzania wakaumizwa au kujeruhiwa na hata kuuawa, atakuwa tayari kubeba lawama au atazihamisha kwa Mange na wale walioshabikia maandamano hayo na yeye kama Rais atasema kuwa aliwaambia wasimjaribu?

Masaa 48 yajayo yataamua.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

Binafsi naombea yafanikiwe najua hawawezi kupindua Serikali lkn baada ya hapo Serikali yetu na mfumo wetu mzima utakuwa umepata sababu za hit back na uzuri wanajulikana wote Serikali ita purge bila huruma mmoja baada ya mwingine, siku zote baada ya chaos mshindi hutengeneza order jinsi atakavyo yeye, Kwa mfano ni sababu tosha kuwavua Tundu Lisu, Zito Kabwe Ubunge, kukifuta chadema, kumuondolea ulinzi Lowasa pmj na kutaifisha mali zake zote hapa nchini kwa kifupi is us against against them, baada ya hapo TZ mpya itaibuka na CCM ikiwa na absolute power ya kuongoza TZ kwa miaka 50 ijayo, lkn wao hawataamka tena!

If you cant take blows, brother dont throw blows, - P.Tosh!
 
Katika matukio ya utekaji negotiator akiwa anaendelea kuongea na watekaji hua anaangalia signs mbalimbali kujua kama mateka watatoka salama.
Mojawapo ni utayari wa watekaji kuachia labda mateka mmoja na kitu kama hicho.

Ningekua Magufuli, tarehe 24 ningemfuta kazi Gambo, tarehe 25 namfuta kazi Mnyeti, tarehe 25 saa sita usiku namfuta kazi Makonda. Tarehe 26 asubuhi naagiza Sugu na Mbowe waje ikulu tuongee.
 
Back
Top Bottom