Kigwangalla afunguka...

Kigwangalla afunguka...

Le Grand Alexei

Senior Member
Joined
Nov 9, 2011
Posts
116
Reaction score
83
SOURCE: Ukurasa wake wa Facebook

TAMKO LANGU: Baada ya kupokea ushauri kutoka kwa ndugu zangu, familia na marafiki, wananchi wenzangu wa Nzega na sehemu nyingine nimeamua kutoa tamko lifuatalo ili kuweka sawa mambo:

Moja, isichukuliwe kuwa nimeshindwa vita na 'mtu' yeyote kwenye hili kwa kuwa sikuwahi kupigana na mtu awaye yote bali na umaskini, ujinga, maradhi, ufisadi na umbumbumbu.

Pili, ieleweke kuwa sintokata rufaa ya kunyang'anywa uanachama ama vyovyote vile kwa kuwa sikuingia kwenye siasa kutafuta ajira ama cheo cha kuwakoga wengine bali niliamua kutoa mchango wangu kwa taifa (service to the nation) kupitia uwakilishi; ndiyo maana sikuwahi kujua hata mshahara wa mbunge ni kiasi gani kabla sijawa mbunge na niko tayari kugombea ubunge kwa nguvu zaidi hata kama tukiamua leo hii hakuna mshahara wowote ule. Pia hata kama kuna mtu anataka kunishughulikia basi afuate kanuni na taratibu zilizoandikwa...huwezi kuniadhibu bila kunishtaki, na bila kunipa fursa ya kusikilizwa! Na huwezi kunihukumu kwa jambo ambalo lipo mahakamani na hukumu bado haijatoka!

Tatu, naomba ieleweke wazi pia kuwa mawazo ya kuanzisha benki, kuanzisha kampuni ya ujenzi (kuchimba visima na kuchonga mabarabara) si yangu peke yangu, ni maazimio ya vikao vingi ambapo tulipewa ushauri wa kitaalamu na tukaona inawezekana na ni miradi endelevu na yenye tija, mimi nilileta wazo la mwanzo tu. Na kwamba, hoja yangu ni kwamba kama wenzangu wanataka kubadilisha matumizi ya pesa hizi, walete hoja ya kufuta azimio la awali kwa mujibu wa utaratibu wa Kanuni zetu za kudumu za Halmashauri na si kupitisha azimio jingine juu ya azimio la zamani (ambalo liliishaanza kufanya kazi kwa madiwani kwenda semina). Na pia watakachokipendekeza na kukiamulia kiwe ni cha manufaa mapana ya umma na kifuate utaratibu, siyo kugawana fedha za umma kwenye kata. Kama ingekuwa ni kutazama maslahi binafsi ni bora hata tungewalipa kifuta jasho wachimbaji wadogo wadogo walioondolewa Lusu kupisha mgodi huo na mpaka leo wanaishi maisha dhalili kabisa nje ya mgodi na ndiyo walioandamana kudai pesa hizo, na siyo madiwani ambao wanajidanganya kuwa pesa zikienda kwao watapata 10% za miradi. Utaratibu wa kugawa pesa kwa usawa kwenye Kata haupo, na hata kama watabadilisha matumizi basi wazipeleke kwenye miradi na madiwani wasihusike kuchagua nani apewe mradi. Miradi watakayoichagua ni lazima iwe endelevu, inayozalisha kipato na yenye taswira ya kuwa alama ya historia ya uwepo wa mgodi Nzega.

Nne, ieleweke hakuna atakayeweza kuninyang'anya heshima ya kuwa Mbunge wa kwanza kuanzisha hoja ya 'ushuru wa huduma' na akafanikisha miaka 15 toka kuingia kwa uwekezaji kwenye migodi mikubwa - leo walau kwa kiasi kidogo maeneo panapochimbwa madini wamelipwa haki zao; na sambamba na hili wanaojidai leo wanajua zaidi kupanga matumizi wajifunze kutafuta pia, maana kuna bilioni 4 zaidi bado zipo huko, watafute na wenyewe basi! Ukijua kula upende na kulima!

Na kwa kuwa sina maslahi yoyote binafsi kwenye haya ninayoyapigania, ieleweke ninaweza pia kunyamaza na kuacha kufanya lolote. Kwa heshima ya wote mlionipigia simu, mlioniona na kusema nami na mlioni-text, na kwa kuepusha mtafaruku kwa wananchi walionichagua na wanaoendelea kuniunga mkono ninawaahidi walau moja kuwa 'sintowasusia fisi bucha', nitaendelea kuzuia pesa hizi zisiliwe mpaka wakubwa watakapoingilia kati na kuingiza hekima na busara kwenye vichwa vya wenzangu hawa. Nitaendelea kusimamia haki ya wananzega kwa kuzilinda pesa hizi kwa njia ya mahakama kama ambavyo nimefanya na kama ikishindikana kuelewana ni bora zisitumike mpaka tumalize muda wetu. Pengine msimamo huu utawafanya waelewe kuwa sifanyi haya kwa malengo ya kutafuta umaarufu wa kura za 2015, kwanza ni nani anayewadanganya kuwa nitagombea tena Ubunge wa Nzega mwaka 2015?

Wakatabahu,
HK.
 
huwezi kupambana na panya ukiwa ndani shimoni nao ukivaa kama wao, ukinywa kama wao na kukaa kwenye vikao vyao halafu ukataka kuwa ghafla umeona mwanga unaanza kupambana nao huwezi shinda. toka nje ya shimo na uache kutafuna vyao halafu upambane nao ukiwa nje na kuanza kuwamiminia maji ya moto ndani ya shimo kama wanavyofanya chadema na muziki wao mdundo wa wote pamoja daima. kwa hivi sasa wewe ni sawa stori yako inafafana na ile hadhithi ya darasa la pili ya yule nyani mtoto aliyemuuliza mama yake mama mbona tunakula mahindi ya binadamu mama yake akamjibu nyamaza binadamu ndiye ametuibia mahindi yetu ingawa hakumwambia mwanae mahindi yale walilima lini kwahiyo kaka hamisi endelea kutafuna mahindi
 
huwezi kupambana na panya ukiwa ndani shimoni nao ukivaa kama wao, ukinywa kama wao na kukaa kwenye vikao vyao halafu ukataka kuwa ghafla umeona mwanga unaanza kupambana nao huwezi shinda. toka nje ya shimo na uache kutafuna vyao halafu upambane nao ukiwa nje na kuanza kuwamiminia maji ya moto ndani ya shimo kama wanavyofanya chadema na muziki wao wa mdundo wa wote daima pamoja.
 
Ccm ndio adui wa maendrleo ya watanzania ni punguwani pekee anayeweza pinga hoja za HK tatizo ccm na jk wameshakaririshwa msingi wa maendeleo ni pesa ndio maana kila kukicha jk yupo ulaya anaomba misaada kunde viva HK hao ulionao kwenye halmashauri ni mazombi
 
Kigwangallah asipokuwa makini atafukuzwa na maccm! Anazidi kuwakandamiza! Ccm na viongozi wake bila 10% haiendi!
 
Kigwangallah asipokuwa makini atafukuzwa na maccm! Anazidi kuwakandamiza! Ccm na viongozi wake bila 10% haiendi!

Amekata tamaa sasa ameamua kuweka wazi 2015 simooo!! CCM ni janga la kitaifa, sasa sijui viongozi wanalizungumziaje au wamekaa kukodolea macho na kuyasemea ya CHADEMA huku kwao hawana habari, na bado tutasikia mengi hadi 2015 ifike mungu tupe uzima
 
Kupigania haki huku ukiwa mwana CCM ni sawa na kujaribu kukimbia kivuli chako mwenyewe!
 
This is utter cheap popularity seeking, hakuna lolote.
 
Wamfukuze haraka kigwangara aje chadema tuwamaliza magamba

Thubutuuuu!!!! Vile Vi-tenda vyake watavipukutisha vyooote!!!! Mwenyewe analijua hilo. Kaka, sio kila aliyeko Magambani anakupenda huko, ila watoto kaka! Unaweza kujikuta umewafungia mlango wa chooni hivi hivi. Maana ukitaka kupiga dili, hakikisha una kadi ya hao jamaa, hapo hata sembe utauza na ukikamatwa hamna kesi, ref. Prof. Kapuya.
 
Unapigana na hewa wewe ikikata unadanja.Uko ndani ya gamba wewe ni gamba tuu na huwezi kupambana nano mpaka ulivue.Watanzania tunaelewa vipaumbele vya magamba ni pamoja na kujilimbikizia Mali na wewe wamekuwahi tuu.
 
toka huko usilalamike tu.upo kundi la wizi bado unashangaa wanapo taka kuiba? kama wewe mpenda haki utatoka mwenyewe sio mpaka ufukuzwe ccm
 
Nape & Hamis msione soo jiungeni CDM hii ni kwa ukweli kabisa msiogope kama kweli mnataka Mapambano.
 
Huyu Kgwangwallah namkubali ni jembe, lakini ndio hivyo CCM ina wenyewe

Mkuu siyo COM tu hata Chadema ina wenyewe! Kingwagala hawezi kukubalika Chadema kwa kuwa kasoma. Si unajua mwenyekiti wetu aliangukia pua form six!
 
Back
Top Bottom