Mbunge wa Nzega mjini kwa tiketi ya CCM, DK. Hamis Kigwangallah (pichani) amefikishwa mahakamani mjini Nzega mapema leo, akishitakiwa kwa makosa matatu ya Kufanya Mkutano isivyo halali, Kuingia Mgodini kinyume cha sheria na kula njama za kuteka kituo cha polisi.
Mbunge huyo amepewa dhamana na kesi yake itarudi tena katika Mahakama ya Wilaya ya Nzega baada ya wiki mbili.
DK. Hamis ameingia matatani na vyombo vya dola kutokana msimamo wake wa kuwatetea wachimbaji wadogo wa mgodi wa kijiji cha Mwabangu, Kata ya Nata dhidi ya wawekezaji wanaodai kumiliki eneo hilo.