Kigoma yaanza kufunguka

Ujenzi wa barabara hizi (Kahama-Kibondo-Kasulu) na Tabora-Uvinza zinafanywa kisiasa mnoo in my opinion. Yaani zinakwenda kwa mwendo wa kinyonga. Bila shaka mwakani zitatumika kwenye kampeni. Ombeni Mungu japo ziishe before 2025.
Yaani wanazingua ni shida licha ya kuwa na mawaziri senior lakini ni bure kabisa imagine barabara ya mpanda Tabora ina wakandarasi 3 na itakamilika kabla ya hizo zilizoanza awamu iliyopita,mwaka huu mpanda wanapata umeme wa grid huko haieleweki.Katavi kuna waziri mmja tu wa ujenzi wao wana mawaziri 3 lakini hakuna wanachosaidia
 
Kanyonza Vs kibonge. Barabara ya nyakanazi ina zaidi ya miaka kumi haiishagi na mkandarasi Nyanzaroad yuko site anakumbatiwa tu.
Mkuu ukiona hivyo jua ni ujenzi wa pesa za ndani yaani za madafu hapo tatizo sio mkandarasi bali mtoa pesa hata huku Swax barabara ya swax kasanga toka 2009 mchina yuko site haiishagi wakati ni 115 km tu labda mwaka huu itaisha wako hatua za mwisho napo ni kwa msukumo binafsi wa waziri wa ujenzi kufanya lobbying maana ni mtu wa Katavi vinginevyo.
Hiyo road uliyoisema haiishi leo au kesho maana hata bajeti yake ni kiduchu sana
 
Asante sana kwa habari..adventure na saratoga za juzi hizo..kulikuwa na ..superstar..kanyonza..kibodeco..maruzuku..kiganza ..mgalaganza..hey few to mention
Zamani kulikuwa na basi mara moja kutoka Mwanza hadi kigoma wakati nikienda kinonko shule ya msingi pale kakonko 1980, tumshukuru anayepigwa vita na akina Quinine na BAK . Nasisitiza maendeleo ni infrastructure tu, vingine vikolombwezo
 
Visasi vyaweza kuwepo iwapo kuna watu wanaona kazi unayofanya ni ya hovyo!!inatia hasira.ndo maana Mungu aliamua kumfukuza Shetani na malaika zake kwa kosa LA kuanza kuona kazi na sheria za Mungu ni za hovyo! Watu wa hovyo ni mbora wasiwepo
 
Fika na ujiji na kibirizi ujionee mradi mkubwa wa bandari, fika ujiji na uvinza ujionee miradi mikubwa ya maji, pia upo mradi mkubwa wa barabara kutoka kabingo mpaka manyovu unaenda Burundi kilometres zaidi ya 200 mradi utaanza muda wowote sababu pesa tayari zipo, gridi ya taifa inakuja mkandarasi yupo njiani, SGR nayo inakuja, serikali imepanua kilimo cha michikichi huko Kigoma kwa maelfu ya mahekari.

Msipomshukuru JPM mtakua wehu. Hata kama ni kodi zenu lakini sio peke yenu wenye uhitaji wa Miundombinu yote hii kwa wakati mmoja.
 
Muongo wewe hiyo barabara ya kasulu - Kibondo- kakonko ni vumbi tupu na sidhani kama itawekwa lami.. Maana ile lami ya kuanzia nyakanaz kuja kibondo imeanza kupigwa lami kuanzia mwaka 2012 ila mpaka sasa haijafika hata kakonko ... Sasa sijui unazungumzia kigoma IPI..


Kigoma iliyoendelea ni Kigoma Municipality tu kasulu na kibondo bado wako kwenye medieval era .. Naongea kwasababu nimeishi maeneo yote ya Kigoma ... Halafu hiyo kasulu na kibondo ndio kuna mawaziri kama Ndalichako, waziri mpango , naibu waziri wa habari .. Kigoma mjini haijawahi kutoa waziri lakini ina maendeleo kushinda huko kibondo na kasulu .. Wameanza kutoa mawaziri miaka na miaka ... Kibondo na kasulu wamejaa wajinga sana sijui kama wataendelea wale ...



Unapoitaja Kigoma uwe specific kabisa kuwa kuna Kigoma mjini na hizo takataka zingine
 
Hivi nani alaumiwe na nani tumpongeze kwa hili la kigoma?
 
Hapo ndipo tunapokosea, ni kweli Magufuli kateua seniors minister wawili toka Kigoma, lakini mawazili ni wa Watanzania yote na hawapaswi kuwa wabinafsi kwa kupeleka miradi nyumbani kwao.
Prof Mbwiliza alishawahi kuwa waziri hakujipendelea na Mporogomyi nae alishawahi kuwa naibu waziri wa fedha wakatie wa serikali ya Mkapa lakini hakujipendelea kwa chochote kwani Manyovu na Muyama kulibaki kama pangoni.
Watu wa Kigoma wana uzalendo wa kupenda Watanzania wenzao bila kujipendelea.
 
Acha maneno ya kisiasa siasa..
 
Nakumbuka miaka ya mwanzoni mwa 90 kuna jamaa mmoja alikuwa na Landover anaitwa Rombo kwa usafiri wa kutoka kigoma mjini mpaka manyovu huko..kweli hii nchi imetoka mbali.
 
Hicho unachoongea wewe hakiendani na falsafa ya charity bigins at home,hii ndio inayoiongoza Tzn ever since
So brother mtachelewa sana ikiwa watu wenu hawaanzi na kwao na hakuna atakayewaona wamefanya jambo zaidi ya wa kwao.Wakati mikoa mingine inaweka lami barabara za mikoa Kigoma hakuna trunk road yoyote imekamilika kuunga na mkoa mwingine ukiacha ya Manyovu kwenda Burundi.
Mfano Dodoma,Arusha,Kilimanjaro,Iringa,Mwanza,Dar,Singida karibu barabara zote kuu za kuingia na kutoka ni lami..Mbeya,Morogoro,Njombe,Songea,Rukwa zimesalia barabara moja moja ili kumaliza mtandao wa lami wa barabara kuu
 


Hizo unazoongea hapa ni KUFURU tupu, Kigoma inayo maendeleo gani ya kuja kadamnasi kutamba??!!,

Unataka "waleta maendeleo" waone mmeridhika na hicho kidogo mnachojivunia??!!, wewe hujui mnajiroga??
 
Zamani kulikuwa na basi mara moja kutoka Mwanza hadi kigoma wakati nikienda kinonko shule ya msingi pale kakonko 1980, tumshukuru anayepigwa vita na akina Quinine na BAK . Nasisitiza maendeleo ni infrastructure tu, vingine vikolombwezo
Maendeleo sio infrastructure ndugu is more than that.
 
Zamani kulikuwa na basi mara moja kutoka Mwanza hadi kigoma wakati nikienda kinonko shule ya msingi pale kakonko 1980, tumshukuru anayepigwa vita na akina Quinine na BAK . Nasisitiza maendeleo ni infrastructure tu, vingine vikolombwezo
TANGANYIKA BUS
 
TANGANYIKA BUS
Kumbe nawe ni mhenga. Ulikuwa ukisubiri basi la kurudi kwa wiki nzima. Halafu Barabara ya Kasulu Kibondo ilikuwa ni tabu sana. Mvua ikinyesha, utelezi na wakati wa kiangazi poda (vumbi). Kama sasa ni lami lazima Quinine , pamoja na ubishi wake, akubali kuna maendeleo (bila kusahau kuwa Magu kiboko ya njia) therefore maendeleo ni infrastructure. Mtu akitoka ulaya haangalii kama kuna mikutano au Lissu kapigwa shaba au Kabendera yupo ndani au Mbowe ananyimwa kibali cha kuhutubia; anaangalia infrastructure then anaconclude kuwa hii nchi aidha imeendelea au la.
 
sasa Kuna maana gani ya kukomaa na kitu ambacho hakiishi? Huoni kama ni kupoteza fedha zaidi? Kwa Kama ni pesa za ndani ndio ziendelee kutolewa tu kwa Kazi isiyoonesha mwisho wake? Nadhani wangeweka fungu la kutosha na kumakiza project moja kwa ukamilifu kisha wanaanza nyingine kuliko kujificha kwenye hoja ya NI FEDHA ZA ndani. Kwa hiyo zenyewe hazfai kukamilisha? Na kwa nini kila miaka hizi tender ni kwa Nyazroad ? Huku ni failure wakubwa?
 
Unachosangaza unasahau hata Malaysia walikuwa kama sisi bado huoni tatizo, nakusikitikia sana, ukikua utajifunza kama tayari ni mtu mzima pole muda umeshakupita hutaelewa tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…