Kigoma yaanza kufunguka

Kigoma yaanza kufunguka

MKEHA

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
716
Reaction score
1,144
Kuna wakati huwa nawaza na kufikiria nyuma kidogo naanza kufurahi. Miaka ishirini iliyopita Kigoma ilikuwa kama si sehemu ya Tanzania.

Umeme ulikuwa makao makuu tu ya mkoa yaani Kigoma Ujiji. Tena ukiwaka mara mbili tu kwa wiki.

Nilikuwa najua ratiba ya umeme kuwaka kuanzia Gungu, Masanga, SIDO, Mwanga sokoni,Kibilizi, Katubuka, Mlole,Majengo na Kilimahewa. Waliokuwa na uhakika wa umeme ni mjini kati na Mji mwema kwakuwa kule waliishi wanene.

Kutoka Kigoma kwenda Kasulu na Kibondo ilikuwa ni Safari ya kutwa nzima na mabasi yetu ya Adventure na Saratoga za wakati ule.

Kutoka Kigoma kwenda Manyovu na Muyama hakukuwa na mabasi bali magari ya mizigo tena ya kuvizia.

Kasulu pamoja na kuwa Mji mkubwa zilitawala kalabai, chemli na vibatali tu,huku Kibondo ikiwa kama mji wa kale wa enzi za ustaarabu wa Kichina yaani China Dynasty.

Hakuna aliyepangiwa kufanya kazi Kigoma aliyekubali kirahisi.

Sasa Kigoma imenza kuwa sehemu nzuri sana kwa kuishi. Barabara ya kuiunganisha na Tabora itakamilika muda si mwingi.

Hata ile ya kuiunganisha na Nyakanazi inaenda vizuri nimepita pale mpakani na mkoa wa Kagera daraja kubwa linajengwa na litaisha muda si mwingi.

Nimeona umeme ukiwaka kuanzia Kakonko, Kibondo yote,Kasulu na vijiji vyake,Heru juu,Kabanga, Muganza, Mwanga,Kasumo,Kalege, Muyama,Biharu,Nyamgali,Buhigwe,Muhaluro,Mnanila na kwingineko.

Mgao haupo tena,
Siku hizi hatusubirii tiketi za kulangua za train maana mabasi tele ya kwenda DSM,Mwanza,Bukoba,Arusha,Tabora,Mpanda na Sumbawanga.

Siku hizi kwenda Kasulu na Kibondo ni muda wowote.

Nimeona maji vijijini yakimwagika mitaani, barabara za vijijini zimeboreshwa sana.
Tunaweza kuwa tunaenda taratibu lakini tunasonga mbele.

Japo bado mkoa wote wa Kigoma tunatumia umeme wa generator lakini unatosheleza mahitaji ya umeme.

Kuishi kwingi ni kuona mengi, kuna vitu vimetokea mazingira yetu sikutarajia kama vingetokea nikiwa bado niko hai.

Mwezi uliopita nimekuta viguzo vya kuonyesha mwisho wa barabara vikiwa nyuma ya choo chetu badala ya kusikitika kwani nyumba yetu yote imeangukia kwenye hofadhi ya barabara lakini nilicheka kwa furaha kwani inawezekana nikaona barabara nzuri sana ya lami ikipita kijijini kwetu

And this happens once in life time.
Mungu nijalie nione mengi zaidi ambayo sikuyategemea kutokea nikiwa bado hai.
 
Acheni ubishi sasa. Kuna Muha mmoja yuko busy hapa jirani anasema UDSM iko Dodoma na yeye AME graduate huko degree ya engineering in human resources
Bujibuji acha utani wako bwana
 
Sasa Kigoma imenza kuwa sehemu nzuri sana kwa kuishi. Barabara ya kuiunganisha na Tabora itakamilika muda si mwingi TANGU ENZI ZA KIKWETE WANACHIMBUA CHIMBUA TU HIYO BARABARA HAIKAMILIKI UCHAGUZI UKIPITA NAO WANAPOTEZEA.

GRID YA TAIFA IMESHAFIKA HUKO? INASIKITISHA KUONA MKOA HUO BADO UNATUMIA UMEME WA KUFUKIWA SIJUI NA MASHINE GANI HUKO.
 
Mungu nijalie nione mengi zaidi ambayo sikuyategemea kutokea nikiwa bado hai.
Kwa hiyo Tanzania inapiga hatua kwenda mbele au sio?

Nilisoma kwa makini andiko lako, nikitegemea kuona 'lawama' na 'pongezi' vikiegemea ulipo ushabiki, lakini sikuona; ndio maana andiko lako likawa la kupendeza kulisoma.

Umeandika kuhusu Kigoma, lakini wapo wengine wanaoweza kuandika mambo yalivyobadilika sehemu nyingine ndani ya Tanzania hii, si katika miundombinu tu, lakini pia katika mambo mengine ya msingi zaidi kama elimu, na kilimo.

Natumaini siku moja utapata fursa ya kutueleza hali ya elimu ya waTanzania hapo Kigoma imebadilika kiasi gani

Wakati tukisherehekea haya uliyoweka hapa, tusisahau mshikamano wetu waTanzania. Ni tunu iliyotutambulisha duniani kote. Ujenzi wa haya m'mavitu' yote yasiwe ndio iwe bei ya kuipoteza tunu hiyo. Haya mavitu tunaweza kuyajenga bila ya lazima ya kuwekeana visasi na kuoneana. Kwa hakika ujenzi huo utakuwa wa furaha sana tukiutekeleza bila ya kuvunja haki za mTanzania yeyote. Na kama ilivyo kawaida, uhalifu unapojitokeza, sheria iachwe ifanye kazi yake bila ya kuipindisha.
 
Ujenzi wa barabara hizi (Kahama-Kibondo-Kasulu) na Tabora-Uvinza zinafanywa kisiasa mnoo in my opinion. Yaani zinakwenda kwa mwendo wa kinyonga. Bila shaka mwakani zitatumika kwenye kampeni. Ombeni Mungu japo ziishe before 2025.
 
Kwa hiyo Tanzania inapiga hatua kwenda mbele au sio?

Nilisoma kwa makini andiko lako, nikitegemea kuona 'lawama' na 'pongezi' vikiegemea ulipo ushabiki, lakini sikuona; ndio maana andiko lako likawa la kupendeza kulisoma.

Umeandika kuhusu Kigoma, lakini wapo wengine wanaoweza kuandika mambo yalivyobadilika sehemu nyingine ndani ya Tanzania hii, si katika miundombinu tu, lakini pia katika mambo mengine ya msingi zaidi kama elimu, na kilimo.

Natumaini siku moja utapata fursa ya kutueleza hali ya elimu ya waTanzania hapo Kigoma imebadilika kiasi gani

Wakati tukisherehekea haya uliyoweka hapa, tusisahau mshikamano wetu waTanzania. Ni tunu iliyotutambulisha duniani kote. Ujenzi wa haya m'mavitu' yote yasiwe ndio iwe bei ya kuipoteza tunu hiyo. Haya mavitu tunaweza kuyajenga bila ya lazima ya kuwekeana visasi na kuoneana. Kwa hakika ujenzi huo utakuwa wa furaha sana tukiutekeleza bila ya kuvunja haki za mTanzania yeyote. Na kama ilivyo kawaida, uhalifu unapojitokeza, sheria iachwe ifanye kazi yake bila ya kuipindisha.
Nimekuelewa sana, Tanzania tunajitofautisha na sehemu zingine kwa TUNU hizo. Hata elimu nayo hatujabaki nyuma, nakumbuka mpaka kufikia miaka ya 90s tulikuwa na shule kama nne za sekondari ambazo ni Kigoma,Mnanila,Muyama na Kibondo girls.
Siku hizi every Ward has it's secondary school
 
Acheni ubishi sasa. Kuna Muha mmoja yuko busy hapa jirani anasema UDSM iko Dodoma na yeye AME graduate huko degree ya engineering in human resources
Hahahaha hahahahahahhahaha khaaaaaa huyo jamaa
 
Miaka hiyo ya ufisadiage nilisikia Kigoma ingalifanywa kuwa Dubai ya Afrika.
 
Back
Top Bottom