KIGOMA: Waziri Mkuu awasimamisha watumushi watatu wa Hospitali ya Wilaya ya Kasulu kwa wizi wa dawa na vifaa tiba

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa awasimamisha kazi Watumishi watatu wa Hospitali ya Wilaya ya Kasulu

> Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo kutokana na watumishi hao kutuhumiwa kwa kujihusisha na wizi wa dawa na vifaa tiba vya Hospitali hiyo
 
Ninafurahishwa sana na utendaji wa mh. Waziri mkuu.
Hafumbii macho uozo na hana mzaha kwa wabadhirifu na wanaotumia vibaya ofisi za umma kujinufaisha binafsi.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa awasimamisha kazi Watumishi watatu wa Hospitali ya Wilaya ya Kasulu

> Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo kutokana na watumishi hao kutuhumiwa kwa kujihusisha na wizi wa dawa na vifaa tiba vya Hospitali hiyo
Kama hao jamaa ni wezi wapelekwe mahakamani wafungwe kabisa...maana wanatuibia rasilimali zetu...

Laoini kama wanatuhumiwa tu sio poa wala nini ..
Maana inawezekana wanao watuhumu wana chuki binafsi tu
 
Bora Ameondoka Kigoma tupumue daaaahh, siyo kwa purukushani hizo daaaahh hizi siku3 Tumekuona cha moto.
 
Kama hao jamaa ni wezi wapelekwe mahakamani wafungwe kabisa...maana wanatuibia rasilimali zetu...

Laoini kama wanatuhumiwa tu sio poa wala nini ..
Maana inawezekana wanao watuhumu wana chuki binafsi tu
Mkuu huyo PM hajawahi na hana record ya kuonea mtu katika kuchukua hatua za kinidhamu.
Ana mbinu za kuhoji kuliko polisi.
Tena taasisi za umma wasikiapo ziara yake ikiwalenga, asikuambie mtu, huwa wanakosa amani na usingizi hadi atapo maliza ziara.
Na amalizapo ziara yake salama, bila ya wao kuguswa na mizaizai, hukimbilia nyumba za ibada kutoa sadaka ya shukrani kwa Mungu kwa kuwaepusha kukinywea kikombe cha PM.
Ukitaka kuhakiki maneno ninayokueleza, ingia you tube andika "ziara za waziri mkuu" uone clips ambazo wanaume wengine wasomi kabisa wanavyojiumauma kama watoto wadogo na kukosa majibu mujarabu ya kujibu.
Hii maana yake ni kwamba, mtu aidha kutokujua wajibu na majukumu yake, ama ukwapuaji.
 
Ndiyo! Lakini tukitaka mambo yaende sawa tuimarishe utawala wa sheria. Polisi, Mahakama wafanye kazi zao, sio siasa, Wizara za Serikali na taasisi husika zisitumike kwa faida ya kikundi fulani cha wenye nguvu. Ukiona CEO anajihusisha na nidhamu kwa karani au bawabu ujue shirika linayumba!
 
Back
Top Bottom