Kigoma sio ndondocha

zitto napenda kum-define kwa maneno mawili
1. NDUMILAKUWILI
2.POPO
akivunja katiba ya ACT akifukuzwa atasema hakuna demokrasia anang'ata anapuliza
 

Angehamia basi chama kingine kati ya vile vilivyoko ili kuviimarisha badala ya kuongeza utitiri wa vyama nchini, kwani yeye ana kasoro gani ya kushindwa kujiunga na vyama vingine? ACT hakitakuwa na miiko kwa wanachama na viongozi wake? tusizunguuke hii ni sera ya divide and rule ya CCM.
 
mkuu nilikua sijajua hivi kumbe zito kabwe ni muanzilishi wa chama cha ACT??
naomba vizibitisho,napenda kulifahamu hili
Rasilimali zote wanazotumia ACT makao makuu tangu ianzishwe ni mali binafsi za Zitto kabwe,Mfano lile Landcruiser ya Zitto iliyokuwa na rangi nyeupe ilibadirishwa rangi toka mwaka jana na kuwa rangi ya damu ya mzee na nyota nyeupe ambayo ni rangi ya bendera za ACT na ndiyo imekuwa ikitumiwa kwa uhamasishaji mkoani KIGOMA,hivyo sio siri kuwa Zito alianzisha chama chake akiwa ndani ya CHADEMA siku nyingi sana na kisheria ni uhaini,CHADEMA walichelewa sana kuchukua maamuzi ya kumfukuza Zito,ilitakiwa awe amefukuzwa siku nyingi sana kwani alikuwa ni msaliti.
 
ujumbe wako wana kigoma wameusikia lakini kuingia chama kingine kwa kutumia utashi wako huo sio undondocha kukaa kwenye chama bila kutumia utashi wako huo ndo undondocha by the way una define vipi undondocha????

Ndondocha ni mtu "ZUZU" aliyetokana na kurongwa. Mfano, watu wanaohama chadema na kumfuata Zitto Kabwe kule ACT wanapaswa kufanya hivyo kwa maslahi yao na taifa lao, na sio kwa kumfuata Zitto au ukabila na ukanda. Maana chama ni kundi sio mtu mmoja mmoja, kama mtu amefukuzwa kwenye chama lazima ujiongeze kabla hujamuunga mkono ili ujiridhishe kwanza nini kimesababisha afukuzwe chadema leo na sio jana wala juzi. Kama chama hakina demokrasia alipataje kuteuliwa kuwa mgombea ubunge wa Kigoma Kaskazini kwa vipindi viwili? Hakukuwa na wagombea wengine ndani ya Chadema ambao wangeweza kuteuliwa kugombea Kigoma Kaskazini? bila shaka ni demokrasia ndani ya chama iliyoamua Zitto agombee Ubunge kwa vipindi 2 Kigoma kaskazini. Ni demokrasia ndani ya chama iliyoamua Zitto awe naibu mwenyekiti wa chadema Taifa, ni demokrasia ndani ya chadema iliyokuwa inampatia Zitto uwaziri kivuli ndani ya kambi ya upinzani hadi kuwa mwenyekiti wa PAC. Ndo maana tunasema mtu mwenye akili timamu hawezi kumfuata Zitto ACT kichwa kichwa bila ya kujiongeza kwanza, ukifanya hivyo wewe huna tofauti na ndondocha bana, mapenzi gani hayo!!!! Kwa hali ilivyo sasa ni vigumu saana kutenganisha mafanikio ya Zitto na Chadema ambacho anakituhumu leo kuwa hakina demokrasia.

Unaona sasa Zitto anaiacha Kigoma Kaskazini na kwenda kugombea jimbo lingine, unajua maana yake? Anadhani kwa kufanya hivyo jimbo hilo litapotea na kurudi CCM.
 

Na wewe ni ACT eheee
 
Daniel Nsazugwako, Jafu, Amani Kabourou, ZZK et al ni Wasaliti wa ukombozi wa nchi hii...hawa ni makuwadi wa mafisadi...
 

Kukua ni haua, na asante sana kwa kutufananisha sisi "wana kigoma" na mandondocha
 
Kweli si ndondocha hata kidogo, maana ndondocha huwa ni mtu mwenye akili safi hapo awali ambaye ameathiriwa na uchawi na hivyo akili yake kuwa zezeta. KIGOMA wao sio ndondocha ila ni taahira, yaani watu ambao wamezaliwa na ubongo mbovu kwa mapenzi ya mungu sio wachawi. Asanteni
 
mkuu nilikua sijajua hivi kumbe zito kabwe ni muanzilishi wa chama cha ACT??
naomba vizibitisho,napenda kulifahamu hili

Anataka kuwa juu ya chama asifungwe na kanuni na katiba za vyama, chama cha namna hiyo hakipo nchini labda ACT yake.
 
Kukua ni haua, na asante sana kwa kutufananisha sisi "wana kigoma" na mandondocha

Hayo unayesema wewe mimi nimesema "Kigoma sio ndondocha" Hata hivyo, kama mtahamia ACT kwasababu tu ni ya Zitto basi walakini mtakuwa nao. Maana watanzania wa leo tunatamani saaana kuwe na vyama 2 tu vya siasa ili vipokezane katika kuiongoza nchi badala ya kuongeza vyama tena. Hakuna jina lingine la kumpatia mtu anayetugawa kwa kutuongezea vyama bali MSALITI wetu. Kumbe Nyerere hakuiacha Kigoma kwenye maendeleo kwa bahati mbayaaaa!!!!!
 

ACT wamebadili rangi ya bendera zao?
 
Sasa Kavulata unataka kupanuwa wigo wa ugomvi na watanzania, kumbe kuachwa nyuma kimaendeleo Enzi za mwalimu Nyerere ilikuwa si bahati mbaya?? goja nikuchonganishe na hawa, RUKWA, MTWARA,LINDI, SONGEA, SINGIDA inamaana hadi Mwanasheria wenu mkuu , hawa wote wanaangukia kwenye ile hukumu yako kwa wana wa Kigoma?yaani Ndondocha au weka tu kwenye lugha nyepesi MISUKULE?
 

Inavyoonekana kila sehemu iliyoachwa nyuma kimaendeleo inayo root cause yake si bure, sababu zinatofautiana nyingine hazifahamiki kabisa, lakini za Kigoma ndiyo sasa zinaaza kufahamika. Hebu fikiria hata wewe watu wanaokihama chama wanachokipenda na chenye sera alizozitumia Zitto kuibana serikali ya CCM iwajengee barabara, soko, shule, n.k eti kwasababu tu Zitto kafukuzwa chadema kwa kukiuka kanuni za chama utawafikiria vipi? Kwani hakuna mtu mwingine Kigoma anayeweza kuwawakilisha badala ya Zito? Kigoma itabaki milele lakini Zitto hatabaki milele kwenye ubunge. Msimamo kama huu wa kutegemea mtu mmoja unatosha kabisa kuwarudisha nyuma wanaKigoma kwenye maendeleo yao. Nyerere amekufa lakini nchi inaendelea kuwepo sembuse Zitto? Bahati mbaya mtu huyo akikosea basi wanakosea watu wote, akifukuzwa wanafukuzwa wote, huo ni uzuzu walahi. Mambo ya maendeleo aliyoyafanya Mh. Zitto Kabwe jimboni kwake yaliwezekana tu kwasababu ya kuwa Chadema, vyama vingine vya upinzani ni ma-pro CCM haviwezi kuwa na ujasiri wa kujenga hata choo kimoja cha shule jimboni kwa kuibana serikali. Binafsi ninampenda sana Mh. Zitto hata ukifuatilia threads zangu utagundua hilo, lakini kama anakosea nitamwambia unakosea kwenye hili, kwakuwa malengo yetu ni kuhakikisha kuwa tunakuwa na vyama vichache vyenye nguvu kubwa ya kusema hapana kwa chama tawala kinapokosea.
 
Kigoma haikuendelezwa na wakoloni kwani ilikuwa ni labour reserve area,wangesomeshwa vibarua wa kupeleka kwenye mashamba ya Mkonge wasingepatikana.
 
Kigoma haikuendelezwa na wakoloni kwani ilikuwa ni labour reserve area,wangesomeshwa vibarua wa kupeleka kwenye mashamba ya Mkonge wasingepatikana.

Hao ni wakoloni sawa na Nyerere naye alikuwa na sababu gani kutojenga barabara wala kuipelekea umeme kigoma?
 
kigoma ndio mkoa wa kwanza kupeleka mbunge wa upinzani bungeni wakati wa uchaguzi mdogo mwaka 1994(baada ya mbano kufariki)
leo unawaita watu wa kigoma kuwa wanapinga kuondoa dhuluma??
dhuluma ipi unayoizungumzia??
zzk ameshaondoka cdm kama mlivyotaka kwa maslahi ya mwenyekiti.
sasa mbna povu linawatoka???
kama ni mpango wa Mungu zzk atang'ara na kama co atakuwa kama mrema
me nadhani umefika wakati mfanye kazi muache majungu
zzk is gone!!
 
naamini una akili nyingi sana ila unatumia theluthi yake kutafakari.
kwann hao cdm wenye dhamira ya dhati hawakutaka kuyamaliza ili kuendeleza mapambano??
kwani cdm mlianza na wabunge wangapi??
kwann huyu mtu mmoja anawatoa maneno yote haya??
mlitaka aondoke, ameondoka!
fanyeni yenu naye afanye yake!!
zzk co wa kwanza kufukuzwa cdm na ninaamin hatakuwa wa mwisho.
jengeni chama chenu, ajenge chama chake
 
Wanakigoma ni wakabila sana na wanasiasa za ukabila ,hawafuati sera wanafuata mtu alikuwepo Dr Kaboul naye walimoenda akawatema ,sasa huyu ndumilakuili Mungu atusaidie amtoe kwenye siasa hili tupate ukombozi tulio wanyonge.

Hapana!!!! Usitu- underate kiasi hicho. Wakati Kabourou alipoondoka Chadema wanachama hawakumfuata na leo mdiyo mwenyekiti wa Ccm mkoa wa Kigoma, mbona Chadema ndiyo inaongoza halmashairi ya Kigoma/Ujiji? Zito amefuluzwa yeye na Chadema Kigoma itakuwepo tutaendelea kuiongoza Kigoma tena nwaka huu itakuwa kwa kishindo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…