Jambo moja ambalo wengi hatulijui ni kuwa Vijiji vya Kigoma vimendelea sana vikilinganishwa na sehemu nyingine hapa nchini.Kwa mfano maeneo ya Manyovu, Kalinzi, Mwandiga n.k. yako juu sana kulingana au kukaribia maeneo ya Uchagani. Tatizo lililokuwa linasumbua ni nishati ya umeme na miundombinu ya barabara za kuunganisha mkoani na nje ya mkoa.Mwelekeo ulioko ni mzuri kwani Kigoma mjini sasa wana umeme angalau wa kuaminika na nafikiri kwa wakati huu wilaya za Kasulu na Kibondo zitakuwa zimeshapatta umeme. Ikumbukwe kuwa wananchi wa vijijini kama Kalinzi na Manyovu tangu zamani wana mwamuko wa kutumia jenereta na umeme wa jua. Kwa upande wa barabara, iko ya lami kutoka Kigoma mjini nadhani kwa wakati huu itakuwa imeishafika Manyovu hadi mpakani na Burundi. Kwa upande wa ile ya Kigoma kuunganisha na mikoa ya Magharibi, lami imefikia Kazuramimba. Ukweli ni kuwa Kigoma iko juu na wananchi wana mwamko wa maendeleo tofauti na taswira iliyoko kwa baadhi ya watu wengi ambao hawajawahi kufika Kigoma hususan maeneo ya vijijini.