Kigoma: Moto mkubwa wawaka usiku huu

Kigoma: Moto mkubwa wawaka usiku huu

Tanganyika1

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
423
Reaction score
90
Ni majira ya saa nane usiku nimeshtushwa toka usingizini na mirindimo mikubwa mithiri ya mabomu. nilipo amka nikawa nasikia kelele za watu kutoka eneo la tukio.

Nilichungulia dirishani nikaona moshi mzito umetanda na kwamba kuna kila dalili kuwa kuna moto mkubwa sana unawaka. Bamaanisha moto mkubwa sana.

nilipotoka nje nikakuta watu kadhaa akishangaa ni nini kinaendelea na mwisho wote tukapata wazo kuwa eneo moto unawaka kuna sheli ya Lake Oil. hivyo yawezekana ni sheli ya lake oil ndio imeripuka moto.

Kama kuna mdau yuko eneo karibu zaidi na najua nini kinaendelea sio vibaya akitupasha habari.

=========
Update:
Ni lori la semi trela limelipuka karibu na bank ya Exim hivi?

Barabara kuu ya mji karibu naKituo cha mafuta na sokoni. Yasemekana mastoo yanaungua na milipuko kama mitatu mikubwa mithili ya ile ya Gombolamboto imetokea.

Vingora na bodaboda, kelele za mbwa ndo milio imetawala. Moto umesambaa eneo kama la viwanja viwili hivi. Tunauona moshi ukiwa umepanda hewani kama kilometa moja. Tumeshtuka sana na kukurupuka usingizini.

Mpaka saa 10.30 moto unaendelea na vingora na ambulansi zinasikika kueelekea na kutoka njia ya Hospitali ya Maweni na uwanja wa ndege hivi?

Saa 12.00 alfajiri moto haujazimika, Usingizi umekata, vingora vinaendelea kusikika Swala zimeanza Misikitini na majogoo yanawika.

Watu wako barabarani lakini, inashangaza milio ya miziki "Lekatugite" ya disko nayo inaendelea.

Picha haijakubali kwani ni usiku bado.
 
Msisogee karibu na kituo msije mkaripukiwa na matanki yaliyozikwa chini. Poleni sana!
 
Ni lori la semi trela limelipuka karibu na bank ya Exim hivi?

Barabara kuu ya mji karibu naKituo cha mafuta na sokoni. Yasemekana mastoo yanaungua na milipuko kama mitatu mikubwa mithili ya ile ya Gombolamboto imetokea.

Vingora na bodaboda, kelele za mbwa ndo milio imetawala. Moto umesambaa eneo kama la viwanja viwili hivi. Tunauona moshi ukiwa umepanda hewani kama kilometa moja. Tumeshtuka sana na kukurupuka usingizini.

Mpaka saa 10.30 moto unaendelea na vingora na ambulansi zinasikika kueelekea na kutoka njia ya Hospitali ya Maweni na uwanja wa ndege hivi?

Saa 12.00 alfajiri moto haujazimika, Usingizi umekata, vingora vinaendelea kusikika Swala zimeanza Misikitini na majogoo yanawika.

Watu wako barabarani lakini, inashangaza milio ya miziki "Lekatugite" ya disko nayo inaendelea.

Picha haijakubali kwani ni usiku bado.
 
Attachments

  • bum 3.jpg
    bum 3.jpg
    442.9 KB · Views: 163
  • HOfuuuuuuuuuu.jpg
    HOfuuuuuuuuuu.jpg
    294.7 KB · Views: 127
Mwaka umeisha,ndo tarehe zetu zakutoa kafara kama shukrani.msishangae kwa hilo dogo,bado makubwa zaidi ya hilo yanakuja.
 
Mi sijui lugha ya kiha "kigoma yawaka motoiku huu" ndo nini?
 
Mi sijui lugha ya kiha "kigoma yawaka motoiku huu" ndo nini?

Wachangiaji watatu walio pita wamemwelewa. Wewe tu? Nenda ukatafute translation ya hicho kiha kwa kutumia google.
 
Poleni aisee,mimi nimelala Veta huku sijasikia,ndo naondoka KIgoma"Kwaheri kigoma"
 
...wakuu ulizieni chanzo,isije ikawa dogo paulo karusha kitu cha nchakali...
 
Mbona mimi nimelala hapa Mwaka Hill Hotel, hotel pekee ya Gorofa hapa Kigoma na ni jirani na jengo la NHC ilipo benki ya Exim na NMB sijasikia kitu kama hicho?
 
Back
Top Bottom