Kigoma Kaskazini wana sababu ya kumchagua Mh. Zitto kuwa muwakilishi wao tena

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,907
3,261
Heshima mbele wadau,
kwa mara nyingi nimekuwa nikifuatilia siasa na wanasiasa wa Tanzania na hasa huyu kijana mwenzetu Mh. Zitto kabwe, huyu mh ambae pia ni naibu katibu mkuu wa chadema mara nyingi amekuwa anajishughulisha na mambo yake binafsi bila ya kukumbuka wananchi wa kigoma kaskazini ambao kwa kiasi kikubwa ndio wamefanikisha kufanya yeye awepo hapo alipo, tuchukulie mfano mdogo, hivi karibuni tumesikia kuwa anaelekea ughaibuni kufanya Phd ambayo ni kitu kizuri kwake binafsi na ambacho akina maslahi kabisa kwa wananchi wake waliomchagua!! katika kipindi hicho atakapokuwa masomoni nani atakuwa muwakilishi wao?? sasa swali ambalo lipo ni kuwa wananchi wake wana sababu ya kuendelea kumchagua kuwa mbunge wao kwa kipindi kingine

SOURCE
JAMBO TANZANIA
 
Jojipoji,
tuelimishe kwanza, kwenda ughaibuni kusoma kunamnyima nafasi mbunge huyo kuhudhuria vikao vya bunge. Mbunge asiyehudhuria vikao vya bunge kuna kanuni za Bunge ambazo haziruhusu hali hiyo. Sidhani Mhe. Zitto atakuwa Mbunge na wakati huo huo anahudhuria masomo nje ya nchi. Tuweke wazi halafu sisi kama wapiga kura wake tuchangie.
 
mimi nadhani angekuwa muungwana endapo angesubiri kipindi cha kuwawakisha wananchi wake kinachoishia mwakani kiishe ndipo akapige kitabu akiwa hana deni nyuma kwa sasa anakuwa kama mganga njaa mwingine yeyotw wmbaye analipwa mshahara wakati hawahudumii wananchi wake
 
Back
Top Bottom