Barua ya wazi kwa Rais: Rais Samia Billionaire Effect

mathoc

New Member
Jun 3, 2023
1
1
Barua ya wazi kwa Mh Rais, Dkt. Samia Hassan Suluhu.

Nakusalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mh. Rais, unaweza usiione barua hii kutokana na wingi wa majukumu uliyonayo ila naamini Mh. Dkt. Mpango (VP), Mh. Majaliwa(PM), wasaidizi wako binafsi pamoja na viongozi wengine walioko chini yako watakujulisha uwepo wa huu ujumbe.

Mh. Rais, mimi ni Mtanzania maskini ninayepambana leo kuona kesho yangu inakuwa bora kuliko jana, na kwa kuzingatia hili nina wazo (idea) ambalo likitekelezwa aidha na serikali au sekta binafsi maisha yangu na ya jamii kwa ujumla yatabadilika kwa kiasi kikubwa.

Mh. Rais, hili wazo limejikita katika kusaidia kutatua tatizo sugu linaloikumba jamii na taifa toka uhuru, utanisamehe hili wazo sitaliweka wazi sana humu kwa kuwa najaribu kulilinda kwa maana kuna watu wana rasilimali zinazoweza kulitekeleza kwa haraka pasipo kukuandikia ila nitajaribu kueleza faida chache zitokanazo na utekelezaji wake.

Mh. Rais, endapo sehemu ya hili wazo ikitekelezwa na sekta binafsi hasa makampuni ya media kama vile Azam media, Startimes n.k kama sehemu ya marketing strategy basi kampuni hizo zitapata umaarufu mkubwa nchini (kukuza brand zao) na hatimaye kufanya kila familia ya Kitanzania kuona umuhimu na ulazima wa kununua bidhaa zao ikiwemo uuzaji wa ving'amuzi kwa kila familia kwa kuwa hizi kampuni zitakuwa zinashiriki moja kwa moja kusaidia kutatua tatizo husika.

Mh. Rais, nimeboresha (modify) hili wazo ili liweze kutumiwa na serikali yako kutatua matatizo yanayowakabiri wananchi. Mh. Rais hili wazo likitekelezwa na wewe binafsi pamoja na serikali unayoiongoza kwa ujumla mtapewa sifa na pongezi nyingi kutoka kwa wananchi kwa sababu utakuwa umeshiriki moja kwa moja kutatua matatizo makubwa yanayowakumba katika maisha yao kwa njia rahisi zaidi.

Mh. Rais, utekelezaji wa hili wazo utaenda sambamba na kuanzishwa kwa kampeni maalum itakayozindua kipindi maalum (Special Tv Program) kitachoruka hewani kila siku ukisisitiza na kuiasa jamii namna bora ya kukabiliana na tatizo husika. Mh. Rais utekekezaji wake hautaigharimu serikali kwa sababu itashare gharama na sekta binafsi kama vile kampuni za media kwa kuwa hata wao watanufaika kimapato na ukuaji wa brand zao kibiashara.

Mh. Rais, kichwa cha barua hii nimekiita "Rais Samia Billionaire Effect" kwa sababu zifuatazo;

I) Ndio yako itaongeza mapato ya serikali kwa mabilioni kwa kutumia fedha kidogo.

II) Ndio yako itaokoa mabilioni ya fedha za serikali zinazotumika kusaidia kutatua tatizo husika.

III) Ndio yako itaongeza ajira, mapato na mzunguko wa fedha katika jamii.

IV) Ndio yako itasaidia kukua kwa sekta binafsi.

V) Ndio yako itabadilisha maisha yangu kwa kuwa mimi binafsi nitanufaika na mapato yatakayotokana na utekelezaji wa hili wazo.

VI) Mwisho kabisa ndio yako itaweka jina lako kwenye rekodi kama Rais aliyeleta mageuzi makubwa katika sekta husika na kuwa case study kwa nchi nyingi za Afrika.

Nimalizie kwa kusema, kwa kuwa hili wazo linaweza tekelezwa na sekta binafsi hivyo basi kama utaona si busara kwa serikali yako kulitekeleza ningependa kuomba msaada wako ili niweze kulitekeleza kupitia kampuni binafsi. Nakutakia majukumu mema katika ujenzi wa taifa.

Kwa mawasiliano zaidi
Email: mathoc2023@yahoo.com

Asante.
 
Hongera kwa kujaribu kuwa miongoni mwa watu wanaojaribu kutatua matatizo ya watanzania.
 
Inaonekana unaweza kuwa na wazo mujarabu, lakini kwa nchi hii inayopuuza vipaji vya wazawa napata shaka kama watakutafuta.
 
Wakati mwingine uwoga wako ndio msumari wako wa kimaendeleo...unamshauri rais hadharani alafu unaogopa kuweka wazo Hilo wazo jambo lako...ushauri wangu kwako...Nenda kasajali kwanza Hilo wazo Kisha uje hapa kuandika kinachoeleweka
 
Acha kupoteza muda wako.

Njoo na ushauri huu siku CCCM ikifa na tukiipata KATIBA mpya.
 
Barua ya wazi kwa Mh Rais, Dkt. Samia Hassan Suluhu.

Nakusalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mh. Rais, unaweza usiione barua hii kutokana na wingi wa majukumu uliyonayo ila naamini Mh. Dkt. Mpango (VP), Mh. Majaliwa(PM), wasaidizi wako binafsi pamoja na viongozi wengine walioko chini yako watakujulisha uwepo wa huu ujumbe.

Mh. Rais, mimi ni Mtanzania maskini ninayepambana leo kuona kesho yangu inakuwa bora kuliko jana, na kwa kuzingatia hili nina wazo (idea) ambalo likitekelezwa aidha na serikali au sekta binafsi maisha yangu na ya jamii kwa ujumla yatabadilika kwa kiasi kikubwa.

Mh. Rais, hili wazo limejikita katika kusaidia kutatua tatizo sugu linaloikumba jamii na taifa toka uhuru, utanisamehe hili wazo sitaliweka wazi sana humu kwa kuwa najaribu kulilinda kwa maana kuna watu wana rasilimali zinazoweza kulitekeleza kwa haraka pasipo kukuandikia ila nitajaribu kueleza faida chache zitokanazo na utekelezaji wake.

Mh. Rais, endapo sehemu ya hili wazo ikitekelezwa na sekta binafsi hasa makampuni ya media kama vile Azam media, Startimes n.k kama sehemu ya marketing strategy basi kampuni hizo zitapata umaarufu mkubwa nchini (kukuza brand zao) na hatimaye kufanya kila familia ya Kitanzania kuona umuhimu na ulazima wa kununua bidhaa zao ikiwemo uuzaji wa ving'amuzi kwa kila familia kwa kuwa hizi kampuni zitakuwa zinashiriki moja kwa moja kusaidia kutatua tatizo husika.

Mh. Rais, nimeboresha (modify) hili wazo ili liweze kutumiwa na serikali yako kutatua matatizo yanayowakabiri wananchi. Mh. Rais hili wazo likitekelezwa na wewe binafsi pamoja na serikali unayoiongoza kwa ujumla mtapewa sifa na pongezi nyingi kutoka kwa wananchi kwa sababu utakuwa umeshiriki moja kwa moja kutatua matatizo makubwa yanayowakumba katika maisha yao kwa njia rahisi zaidi.

Mh. Rais, utekelezaji wa hili wazo utaenda sambamba na kuanzishwa kwa kampeni maalum itakayozindua kipindi maalum (Special Tv Program) kitachoruka hewani kila siku ukisisitiza na kuiasa jamii namna bora ya kukabiliana na tatizo husika. Mh. Rais utekekezaji wake hautaigharimu serikali kwa sababu itashare gharama na sekta binafsi kama vile kampuni za media kwa kuwa hata wao watanufaika kimapato na ukuaji wa brand zao kibiashara.

Mh. Rais, kichwa cha barua hii nimekiita "Rais Samia Billionaire Effect" kwa sababu zifuatazo;

I) Ndio yako itaongeza mapato ya serikali kwa mabilioni kwa kutumia fedha kidogo.

II) Ndio yako itaokoa mabilioni ya fedha za serikali zinazotumika kusaidia kutatua tatizo husika.

III) Ndio yako itaongeza ajira, mapato na mzunguko wa fedha katika jamii.

IV) Ndio yako itasaidia kukua kwa sekta binafsi.

V) Ndio yako itabadilisha maisha yangu kwa kuwa mimi binafsi nitanufaika na mapato yatakayotokana na utekelezaji wa hili wazo.

VI) Mwisho kabisa ndio yako itaweka jina lako kwenye rekodi kama Rais aliyeleta mageuzi makubwa katika sekta husika na kuwa case study kwa nchi nyingi za Afrika.

Nimalizie kwa kusema, kwa kuwa hili wazo linaweza tekelezwa na sekta binafsi hivyo basi kama utaona si busara kwa serikali yako kulitekeleza ningependa kuomba msaada wako ili niweze kulitekeleza kupitia kampuni binafsi. Nakutakia majukumu mema katika ujenzi wa taifa.

Kwa mawasiliano zaidi
Email: mathoc2023@yahoo.com

Asante.
Si ukashiriki shindano la stories of change sasa?
 
Inaonekana unaweza kuwa na wazo mujarabu, lakini kwa nchi hii inayopuuza vipaji vya wazawa napata shaka kama watakutafuta.
Ni kweli ndo tatizo la nchi zetu nyingi za Kiafrika mara nyingi watu wenye mawazo bora huwa hawazingatiwi. Hii inasababishwa na jamii kubwa ya Kitanzania na Afrika kwa ujumla kuwa na watu wenye uwezo mdogo wa kifikra na mwisho wa siku tunapata viongozi wengi wenye uwezo mdogo kama jamii yenyewe.
 
Back
Top Bottom