Kigogo wa CHADEMA Mwanza arudi CCM

Upuuzi mtupu, eti kigogo na kinara chadema, vibaraka wote watajiondoa wenyewe. Chadema itaendelea kuimarika kila kukicha
 
Kesho ataondoka CCM na kwenda CUF. Atatoa sababu kwamba CCM kumejaa rushwa, ufisadi, upendeleo wa kupeana vyeo, undugu, udini na ukiritimba. Wanaofurahi hili watasemaje?

Alitoka CCM anarudi CCM, njaa ya madaraka mbaya sana.
 
Hao waliotoka huko acha warudi hukohuko chadema ni kizazi kipya
 
unajua wanachama na viongozi wa cdm ukweli mnajua kuwa mnapingana na ukweli ulio wazi..kuwa cdm ni wapiga debe tu ....hakuna sera hakuna mipango ni chama cha eneo moja mawili ukitoka maeneo hayo basi hakuna cdm....... ili si vibaya mkaendelea kuwa kama fisi
 
akiondoka mnafiki mmoja wanajiunga waungwana 100 hongera kujionesha mapema mngetutesa mbele ya safari......nenda baba ukapewe kiasi kidogo cha mabaki ya swala wenzio wanakula za twiga na faru
 
huyu amerudi kwa mafisadi wemnzake. alitegemea kufanya ufisadi Chadema akagundua haiwezekani ndiyo maana katoka na kibwagizo cha SIZITAKI KWANZA MBICHI. nenda salama.
 

Mbona baadhi ya sera za chadema ccm imezichukua kwa manufaa ya umma kama katiba mpya, kushusha bei kwa vifaa vya ujenz, n.k ila sera zote hizi huzioni? Ama kweli wanaccm mmepigwa upofu kama ilivyo kwa Mfalme Falao wakati hule, hata hivyo mfa maji haishi kutapa tapa....
 
Karibu Mwana mpotevu. Rudi kwa baba yako........

Ana dhambi kweli kweli alimkana baba yake akiwa mzima sasa anamrudia wakati akipumulia Mashine.Inaonekana ni kwa Jinsi gani alivokuwa kahaba
 
.
Soma vizuri sela za ccm hayo wanayoongea chadema yote yalikuwepo tokea enzi za ukoloni ...... Cdm kama mmekopi na kusema majukwa
 
Amechoka kuandamana anataka kujenga nchi.waambie na wengine
 
Kama aliona CDM hakina sera alikuja fanya nn?. Jibu hili ukiona watu wa aina hiyo lengo lao kubwa ni kuchumia tumbo baada ya mtu kuona huku ni vita vya ukomboz kwa mtanzania mnyonge tu anaamua kukimbilia kule ambako anapewa kitu fulani.
 
Kachoka na matamko ya uongo maandamano yasiyoisha ambayo yanafanya vijana wabaki walalamikaji kazi hawafanyi et wanasubili serikali iwalipie kodi za pangp....nyinyi cdm mnawapotosha watz jamani ....uwongo wenu umepitiliza .... Watu sasa wamegundua kumbe cdm saccos
 
Ni bora wabaki wawili lakini wa ukweli kuliko kuwa 100 mamluki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…