Kigogo wa Barrick aikaanga kampuni ya ACACIA

Naomba nisikuite kilaza,

Kwanza hakuna mkataba wowote kati ya Barrick na Tanzania, kilichopo ni MOU tuu!.

Pili, ukiuza kampuni unaweza kuuza assets tuu na sio liabilities.

Tatu lile deni letu kwa Acacia ni deni hewa, haliko registered popote, hata Acacia ikiuzwa leo, hakuna popote deni hilo litakapo onekana.

P
Wambie wambie wambie
 
kadiri navyopata ufahamu wa haya mambo ndipo maumivu yanapoongezeka ni heri ningekuwa maamuma kama kina jingalao etc..
 
Wewe umejificha kwenye ID fake unatoa povu kwa Verified user hovyo kabisa. Pascal pole sana.... Usichoke kutupatia ukweli pale unapoona upotoshaji. Humu wengi ni mihemuko ya itikadi na ushabiki usio na tija.
Kwa hiyo wewe unadanganyika na verified user? Naye ni mtu tu kama wewe na uelewa wake wakawaida tu ndiyo maana kuna comments zake nyingi tu humu amabuma. Asitudanganye kuwa MoU eti si chochote kwa sababu tu it is not legally binding kuamini hivyo ni upofu wa macho na akili wa kutoangalia issue kwa upana wake. Kwa mwanasheria hata ambaye hajabobea sana kwenye sheria hawezi ku conclude eti MoU si chochote kwenye sheria. Ila naye ni haki yake kutoa maoni yake ila kuiponda tume simply umepata info kiduchu wakati hata MoU yenyewe hujaiona wala kuisoma eti anaiponda tume lakini hatuonyesha yeye kama mwanasheria ameshaifanyia nini nchi hii ili tumwone basi kabobea kwenye sheria. Mimi namjua Pascal Mayalla amebobea kwenye utangazaji
 
Kusema ukweli huyu MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Profesa John Thornton, ni mtu very intelligent!. Anaishambulia kampuni tanzu yao ya Acacia Mining, ili tuu kuipa Tanzania confidence kuwa Barrick wako na sisi, hivyo kufanya mazungumzo na serikali yetu bila kuwahusisha Acacia, na chochote kitakachofikiwa kwenye mazungumzo ya Barrick na serikali yetu, ni nothing at all Kwa sababu the determinants sio serikali yetu wala sio Barrick, bali ni Acacia.

Mtoto wako akifanya kosa kubwa la kustahili adhabu Kali hata ya kifo, wewe baba ili kumnasua mwanao, utakuwa tayari kuthibitisha kuwa mwanao ni insane, hivyo insanity ni defence kwenye criminal cases.

Anachofanya Boss wa Barrick ni kuendelea kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa, huku Barrick wakiuza shares zao, Kwa sasa tayari wameisha uza 51% majority kwa Rangold na wao kubaki na 49%, next month mkutano mkuu wa share holders unaitishwa kubariki mabadiliko hayo, hivyo sisi kujikuta hatuna chetu!.

Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye uamuzi wa mwisho ni Acacia!, Kwanini hakushirikishwa?!. Je, Tutalipwa?. - JamiiForums

Je, wajua kuna uwezekano Barrick wanatuingiza mkenge?!. Hili la kugawana 50/50 ya faida ni kweli au ni changa la macho tu?. - JamiiForums

Mambo ya Barrick; Barrick Executive Chairman Thornton Ajiuzia Shares na kumiliki Shares Milioni 5!. - JamiiForums

Wakati Tukisubiri $ Milioni 300 zetu Kutoka Barrick, Yauza Hisa za $ Milioni 300 Kwa Mchina Huku Ikinunua Mgodi wa Randgold Kwa $ Bilioni 18.3!. - JamiiForums

Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa? - JamiiForums

P

Hapa ndipo unapoweza kutofautisha watu wanaowaza kwa kutumia vichwa na wala wanaowaza kwa kutumia.....................ngoja niishie hapa maana naweza tukana bureeeee
 
View attachment 893492
Ni Profesa John Thornton aliyekuja nchini kuonana na Rais JPM wakati wa sakata la makinikia.

Athibitisha msimamo wa tume ya makinikia kuwa ACACIA imekuwa na tabia ya kukwepa kodi Tanzania.

Asikitika kampuni hiyo kusababisha kuharibika kwa mahusiano ya kibiashara na serikali.

NA Mwandishi maalum
MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Profesa John Thornton, amesema kampuni yao ya Acacia Mining inayofanya kazi Tanzania, haijawahi kulipa kodi ya mapato (Coporate Income Tax) kwa serikali ya Tanzania kutokana na shughuli za uchimbaji wa dhahabu nchini suala ambalo limeathiri uhusiano baina ya kampuni hiyo na serikali.
Kauli hiyo ya Prof. Thornton inaleta matumaini kwa serikali ya Tanzania katika majadiliano yanayoendelea baina yake na Barrick juu ya tozo na kodi ambazo wanatakiwa kuilipa serikali kutokana na usafirishaji wa makinikia kwa miaka 19 tangu Acacia kuanza shughuli zake za uchimbaji nchini.
Tayari kampuni ya Barrick imeshakubali kulipa Tanzania dola milioni 300 kama utayari wa kushirikiana wakati majadiliano yakiendelea baina ya pande hizo.
Kwa mwaka mmoja na nusu sasa serikali imezuia usafirishaji wa makinikia (gold concentrate) nje ya nchi suala ambalo limeathiri utendaji kazi wa kampuni ya Acacia nchini kwa kiasi kikubwa pamoja na kusababisha kuporomoka kwa hisa zake katika soko la hisa la London.
Akizungumza katika mahojiano na The Globe and Mail mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu alisema Migodi ya Barrick inayomilikiwa na Acacia kwa asilimia 64 nchini Tanzania “hajalipa kodi ya mapato kwa Tanzania” zaidi ya kulipa mirabaha na kodi za mishahara tu.

Hata hivyo si Barrick wala Thornton ambao wamekanusha kuhusu ukweli wa kauli hiyo zaidi ya Barrick kujaribu kufafanua kuwa wanafikiri kuwa Mwenyekiti huyo alitia chumvi wakati akimaanisha kuwa kiasi kilicholipwa kwa serikali ya Tanzania ni kidogo sana ikilinganishwa na mapato ya Acacia katika shughuli za uchimbaji dhahabu nchini.
Kauli hiyo imeleta mgongano baina ya Barrick na Acacia baada ya Acacia kuipinga na kusema wanashangazwa na taarifa hiyo isiyo sahihi ya Thornton.
Kwa mujibu wa Globe, Acacia ikiwa imetolewa kwenye mazungumzo kati ya serikali ya Tanzania na Barrick, mafaili kwaajili ya kuunda mkataba mpya yamekabidhiwa kwa Kevin Thomson ambaye Mtendaji Mwandamizi wa Mikakati wa Barrick.
Kampuni ya Acacia iliingia katika kashfa ya usafirishaji wa makinikia na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha kwa mujibu wa tume ya uchunguzi iliyoundwa na Rais John Magufuli kuchunguza ukweli wa kiasi na thamani ya madini yaliyopo katika makontena ya makinikia yaliyozuiliwa.
Kamati hiyo ilibaini kuwepo kwa viwango vingi vya juu vya dhahabu ndani ya makinikia yaliyofanyiwa uchunguzi. Viwango hivyo ni kati ya 671 g/t hadi 2375 g/t, sawa na wastani wa 1400 g/t.
“Wastani huo ni sawa na 28 kg za dhababu kwenye kontena moja lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kwenye makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na wastani wa tani 7.8 za dhahabu yenye thamani ya TZS bilioni 676 (USD 307,292,720),” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa Mei mwaka jana na kuongeza;
“Aidha, kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwenye kontena moja lenye shehena ya tani 20 za makinikia (47.5 kg), kiasi cha dhahabu katika makontena 277 kitakuwa 13,157.5 kg ambazo thamani yake ni Sh trilioni 1.146 (USD 521,300,150).
“Hivyo, thamani ya dhahabu katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147.”
Kutokana na taarifa hiyo ya Kamati ya Mkinikia, Prof. Thornton alikutana na Rais Magufuli Juni 14 2017 na kufanya mazungumzo ambapo aliahidi kuwa Barrick ipo tayari kufanya majadiliano na serikali ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kuendesha shughuli zake hapa nchini.
Julai 31 2017 majadiliano baina ya pande hizo mbili yalianza huku upande wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi na baadae Barrick ikakubali kuilipa Tanzania Dola za Marekani Milioni 300 sawa na Sh bilioni 600.
Hatua hiyo ilifikiwa Oktoba mwaka jana wakati kamati mbili za majadiliano ile ya Tanzania na ya Barrick zilipokuwa zikiwasilisha ripoti ya mazungumzo yao kwa Rais Magufuli ambapo ikiwa ni mara yake ya pili kukutana na Rais Prof. Thornton alitoa salamu za shukrani na kusema kampuni yao italipa kiasi cha dola za Marekani milioni 300 kama njia ya kuonesha utayari wake na uaminifu kwa Serikali ya Tanzania.
Thornton alisema licha ya kuwa kwa sehemu kubwa wameafikiana masuala mengi, lakini suala ya tozo ya malimbikizo ya kodi bado hawajakubaliana kikamilifu na kwamba wameliweka kiporo wakati akiwasiliana na wanahisa wengine ili kufikia makubaliano zaidi.
Kauli yake ya sasa inaleta matumaini makubwa kwa serikali ya Tanzania kuwa huenda kiasi cha zaidi ya Trilioni 400 kilichokadiriwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kikalipwa na kampuni hiyo.
Baada ya Globe kuchapisha kauli hiyo ya Thornton, Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia, Peter Geleta aliibuka na kukanusha taarifa hiyo akisema kuwa si taarifa sahihi.
“Tulishangazwa sana na taarifa zisizo sahihi za Thornton na tumetaka Barrick watoe ufafanuzi,” aliiambia Globe.
Geleta alitoa ufafanuzi kwa wafanyakazi wake kupitia tangazo la ndani la Septemba 18 mwaka huu kuwa Acacia na kampuni zake tanzu umelipa dola bilioni 1 kama kodi na mrabaha kwa serikali kwa miaka zaidi ya 15.
Alisema kwa nusu ya mwaka huu wamelipa kodi ya mapato ya dola milioni 23.3 na mwaka jana dola milioni 34.6 na kwamba kwa miaka 15 wamelipa jumla ya dola milioni 140 kama kodi.

Jinsi huyo prof anavomuangalia Jiwe.......mmmmhhh.....mwenye akili unaelewa tu kuwa hamna kitu hapa.
 
Kusema ukweli huyu MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Profesa John Thornton, ni mtu very intelligent!. Anaishambulia kampuni tanzu yao ya Acacia Mining, ili tuu kuipa Tanzania confidence kuwa Barrick wako na sisi, hivyo kufanya mazungumzo na serikali yetu bila kuwahusisha Acacia, na chochote kitakachofikiwa kwenye mazungumzo ya Barrick na serikali yetu, ni nothing at all Kwa sababu the determinants sio serikali yetu wala sio Barrick, bali ni Acacia.

Mtoto wako akifanya kosa kubwa la kustahili adhabu Kali hata ya kifo, wewe baba ili kumnasua mwanao, utakuwa tayari kuthibitisha kuwa mwanao ni insane, hivyo insanity ni defence kwenye criminal cases.

Anachofanya Boss wa Barrick ni kuendelea kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa, huku Barrick wakiuza shares zao, Kwa sasa tayari wameisha uza 51% majority kwa Rangold na wao kubaki na 49%, next month mkutano mkuu wa share holders unaitishwa kubariki mabadiliko hayo, hivyo sisi kujikuta hatuna chetu!.

Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye uamuzi wa mwisho ni Acacia!, Kwanini hakushirikishwa?!. Je, Tutalipwa?. - JamiiForums

Je, wajua kuna uwezekano Barrick wanatuingiza mkenge?!. Hili la kugawana 50/50 ya faida ni kweli au ni changa la macho tu?. - JamiiForums

Mambo ya Barrick; Barrick Executive Chairman Thornton Ajiuzia Shares na kumiliki Shares Milioni 5!. - JamiiForums

Wakati Tukisubiri $ Milioni 300 zetu Kutoka Barrick, Yauza Hisa za $ Milioni 300 Kwa Mchina Huku Ikinunua Mgodi wa Randgold Kwa $ Bilioni 18.3!. - JamiiForums

Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa? - JamiiForums

P
Wateuliwa wa rais hawawezi kukuelewa maana wao ni wajuaji kuliko wewe na ndo maana hadi sasa trln 400 na kishika uchumba bado tuna uhakika nacho coz hao ni wanaume kwelikweli..hivi hujawahi kujiuliza kwanini kina kabudi hawqtaki tena kusikia hii story ya makinikia popote pale?jinsi story ya faru john ilivofungwa ndivo na hii ilivofungwa na hatuna pa kuulizia maana ukiulizia tu kuna mawili either upotee kwa kutekwa au utupwe ndani kwa kuhujumu juhudi za rais
 
"..........Thornton alisema licha ya kuwa kwa sehemu kubwa wameafikiana masuala mengi, lakini suala ya tozo ya malimbikizo ya kodi bado hawajakubaliana kikamilifu na kwamba wameliweka kiporo wakati akiwasiliana na wanahisa wengine ili kufikia makubaliano zaidi.
Kauli yake ya sasa inaleta matumaini makubwa kwa serikali ya Tanzania kuwa huenda kiasi cha zaidi ya Trilioni 400 kilichokadiriwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kikalipwa na kampuni hiyo.
Baada ya Globe kuchapisha kauli hiyo ya Thornton,........."

Kama vipi tuwatume MAJEMBE AUCTION MART ili wakazidai hizi pesa zetu za kununulia noah, tushachoka mwendokasi
 
Kusema ukweli huyu MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Profesa John Thornton, ni mtu very intelligent!. Anaishambulia kampuni tanzu yao ya Acacia Mining, ili tuu kuipa Tanzania confidence kuwa Barrick wako na sisi, hivyo kufanya mazungumzo na serikali yetu bila kuwahusisha Acacia, na chochote kitakachofikiwa kwenye mazungumzo ya Barrick na serikali yetu, ni nothing at all Kwa sababu the determinants sio serikali yetu wala sio Barrick, bali ni Acacia.

Mtoto wako akifanya kosa kubwa la kustahili adhabu Kali hata ya kifo, wewe baba ili kumnasua mwanao, utakuwa tayari kuthibitisha kuwa mwanao ni insane, hivyo insanity ni defence kwenye criminal cases.

Anachofanya Boss wa Barrick ni kuendelea kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa, huku Barrick wakiuza shares zao, Kwa sasa tayari wameisha uza 51% majority kwa Rangold na wao kubaki na 49%, next month mkutano mkuu wa share holders unaitishwa kubariki mabadiliko hayo, hivyo sisi kujikuta hatuna chetu!.

Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye uamuzi wa mwisho ni Acacia!, Kwanini hakushirikishwa?!. Je, Tutalipwa?. - JamiiForums

Je, wajua kuna uwezekano Barrick wanatuingiza mkenge?!. Hili la kugawana 50/50 ya faida ni kweli au ni changa la macho tu?. - JamiiForums

Mambo ya Barrick; Barrick Executive Chairman Thornton Ajiuzia Shares na kumiliki Shares Milioni 5!. - JamiiForums

Wakati Tukisubiri $ Milioni 300 zetu Kutoka Barrick, Yauza Hisa za $ Milioni 300 Kwa Mchina Huku Ikinunua Mgodi wa Randgold Kwa $ Bilioni 18.3!. - JamiiForums

Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa? - JamiiForums

P
Angalia pm yako
 
Kwa hiyo wewe unadanganyika na verified user? Naye ni mtu tu kama wewe na uelewa wake wakawaida tu ndiyo maana kuna comments zake nyingi tu humu amabuma. Asitudanganye kuwa MoU eti si chochote kwa sababu tu it is not legally binding kuamini hivyo ni upofu wa macho na akili wa kutoangalia issue kwa upana wake. Kwa mwanasheria hata ambaye hajabobea sana kwenye sheria hawezi ku conclude eti MoU si chochote kwenye sheria. Ila naye ni haki yake kutoa maoni yake ila kuiponda tume simply umepata info kiduchu wakati hata MoU yenyewe hujaiona wala kuisoma eti anaiponda tume lakini hatuonyesha yeye kama mwanasheria ameshaifanyia nini nchi hii ili tumwone basi kabobea kwenye sheria. Mimi namjua Pascal Mayalla amebobea kwenye utangazaji
Hakuna hata siku moja, nimewahi kujinasibu humu kuwa mimi ni mwanasheria, nilichosema na ninaendelea kusema, mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, ambaye pia nimefuta tongotongo za sheria pale UDSM, kusoma tuu sheria, hakumfanyi mtu kuwa mwanasheria. Mimi sio mwanasheria.

P.
 
Huko Tarime mara kuna viongozi na baadhi ya walimiki wa mgodi Barack wapo mahabusu mda huu baada ya kufikishwa mahakamani leo kwa ufisadi wa pesa kwa malipo ya milahaba kwenye maeneo ya migodi, wana JF fuatilieni huko mtapata taarifa zote.
sawa mkuu sisi wana habari tutafuatilia
 
Hakuna hata siku moja, nimewahi kujinasibu humu kuwa mimi ni mwanasheria, nilichosema na ninaendelea kusema, mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, ambaye pia nimefuta tongotongo za sheria pale UDSM, kusoma tuu sheria, hakumfanyi mtu kuwa mwanasheria. Mimi sio mwanasheria.

P.
jibu mujarab kabisa
 
Kusema ukweli huyu MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Profesa John Thornton, ni mtu very intelligent!. Anaishambulia kampuni tanzu yao ya Acacia Mining, ili tuu kuipa Tanzania confidence kuwa Barrick wako na sisi, hivyo kufanya mazungumzo na serikali yetu bila kuwahusisha Acacia, na chochote kitakachofikiwa kwenye mazungumzo ya Barrick na serikali yetu, ni nothing at all Kwa sababu the determinants sio serikali yetu wala sio Barrick, bali ni Acacia.

Mtoto wako akifanya kosa kubwa la kustahili adhabu Kali hata ya kifo, wewe baba ili kumnasua mwanao, utakuwa tayari kuthibitisha kuwa mwanao ni insane, hivyo insanity ni defence kwenye criminal cases.

Anachofanya Boss wa Barrick ni kuendelea kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa, huku Barrick wakiuza shares zao, Kwa sasa tayari wameisha uza 51% majority kwa Rangold na wao kubaki na 49%, next month mkutano mkuu wa share holders unaitishwa kubariki mabadiliko hayo, hivyo sisi kujikuta hatuna chetu!.

Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye uamuzi wa mwisho ni Acacia!, Kwanini hakushirikishwa?!. Je, Tutalipwa?. - JamiiForums

Je, wajua kuna uwezekano Barrick wanatuingiza mkenge?!. Hili la kugawana 50/50 ya faida ni kweli au ni changa la macho tu?. - JamiiForums

Mambo ya Barrick; Barrick Executive Chairman Thornton Ajiuzia Shares na kumiliki Shares Milioni 5!. - JamiiForums

Wakati Tukisubiri $ Milioni 300 zetu Kutoka Barrick, Yauza Hisa za $ Milioni 300 Kwa Mchina Huku Ikinunua Mgodi wa Randgold Kwa $ Bilioni 18.3!. - JamiiForums

Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa? - JamiiForums

P
Mkuu P kwani ww siyo mtz na km ni mtz kwann tunaongozwa na wasioona mbali wasiofikiria nje ya box...mkuu unawaza nje box always kinachooneka machoni hakikupofushi
 
sawa mkuu sisi wana habari tutafuatilia
Waliopo jela wapo 7 na MZUNGU ni mmoja ambaye ni Raia wa Africa kusini tuhuma yao ni upotevu wa bilion 11 fuatilia vizuri watafikishwa mahakamani tarehe 24 nenda Takukuru watakupa taarifa zote kwani wao ndiyo waliwakamata na kuwafikisha mahakamani na hatimae kupelekwa gerezani mpaka tarehe 24 kesi yao itaposomwa tena.
 
Hakuna hata siku moja, nimewahi kujinasibu humu kuwa mimi ni mwanasheria, nilichosema na ninaendelea kusema, mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, ambaye pia nimefuta tongotongo za sheria pale UDSM, kusoma tuu sheria, hakumfanyi mtu kuwa mwanasheria. Mimi sio mwanasheria.

P.
Mayala tunakuomba uende Takukuru ufualitilie hilo sakata la wizi wa pesa huko Acacia Barrick huko Tarime mara ambalo watuhumiwa wanasota Lupango mpaka tarehe 24/ 10 kesi yao itasomwa tena.
 
Hii thread inatakiwa kujadiliwa na wenye akili timamu tu,ukifuatilia michango ya members baadhi hapa ni bure yaani weupe kabisa. Naendelea kusoma ujinga wa wengi kudandia gari kwa mbele.

Paschal bravo
 
Back
Top Bottom