Kigogo wa Barrick aikaanga kampuni ya ACACIA

Kigogo wa Barrick aikaanga kampuni ya ACACIA

Mkuu MOU kwa kiswahili cha kawaida ina maana gani? Wewe ni bingwa wa sheria kuliko tume ya Prof. Kabudi. Wewe ni mtangazaji tu kwenye sheria ni kilaza tu!

Sawa tufanye Pascal Mayalla ni kilaza kwenye sheria kama unavyodai, Je alichokiongea kina maana au hakina tija?
Mtu anaweza kusomea na akawa mbobevu wa sheria lakini asiitumie kwa manufaa, kutokusoma sheria hakukufanyi ukose akili ya kuchambua mambo kwa mapana.

Hiyo tume iliyoongoza majadiliano kwa ufupi ni kwamba haikupata muafaka wowote wa maana ndio sababu unaona lile jambo limetelekezwa. Kumbuka wakati timu yetu inatoa taarifa yake mkalimani alizuiliwa kufanya kazi yake.
 
Mkuu kama mwana JF na mwanasheria na mtafuta habari mzuri, unaweza kutusaida vifungu vya sheria ama za kwetu ama za kimataifa ama za nchi ilikosajiliwa BArrick ili tusimamishe mchakato huu mpaka makubaliano yafikiwe baina yetu na wao(barrick)?
Hakuna kitu hapo. Kwa mujbu wa sheria zetu migodi ya BUL, NMR au BUZ [Acacia/Barrick Gold] ni autonomous legal entities ambazo haziwezi kuuzwa au kubadilishwa umiliki bila idhini ya Kamisheni ya Madini. Kwa hiyo tuko salama.
 
Sawa tufanye Pascal Mayalla ni kilaza kwenye sheria kama unavyodai, Je alichokiongea kina maana au hakina tija?
Mtu anaweza kusomea na akawa mbobevu wa sheria lakini asiitumie kwa manufaa, kutokusoma sheria hakukufanyi ukose akili ya kuchambua mambo kwa mapana.

Hiyo tume iliyoongoza majadiliano kwa ufupi ni kwamba haikupata muafaka wowote wa maana ndio sababu unaona lile jambo limetelekezwa. Kumbuka wakati timu yetu inatoa taarifa yake mkalimani alizuiliwa kufanya kazi yake.
You are not informed mkuu cool down soon you will see the outcome of the signed MOU!
 
You are not informed mkuu cool down soon you will see the outcome of the signed MOU!

Unaweza ukawa sahihi kwamba sina taarifa sahihi, lakini MOU gani unaiongelea hapa mkuu. MOU kati ya nani na nani? Unafuatilia kwa karibu kinachoendelea namna ACACIA na BARRICK zinavyoendeshwa kwa sasa?
 
Nadhani wanachokifanya Barrick kinaitwa "let us teach them a lesson that we are above them". Hata mimi nisiyejua sheria nafahamu kabisa kuwa Juma hawezi kuwa Ashura yanapokuja masuala ya kudaiana kisheria hata kama Juma ni Baba mzazi wa Ashura
 
MoU ni hati ya makubaliano ambayo haifungi kisheria.
Umesema vizuri sana kuwa MOU kuwa ni makubaliano kati ya pande mbili ambayo kisheria yanakubalika. Mkikubaliana kuuziana kitu au jambo lolote hiyo hati inaweza kutumika mahakamani kama mbeleni mmeshindwa kuelewana ikiwa hiyo MOU imekidhi kisheria.
 
Hawa jamaa wanaakili mingi sana, wanajua wanachokifanya ....usishangae Barick wakitangaza kuwa wanaungana na serikali kuwadai ACACIA ili tulipwe kishika uchumba chetu, jamaa wanajua kutuchora sana.
 
Umesema vizuri sana kuwa MOU kuwa ni makubaliano kati ya pande mbili ambayo kisheria yanakubalika. Mkikubaliana kuuziana kitu au jambo lolote hiyo hati inaweza kutumika mahakamani kama mbeleni mmeshindwa kuelewana ikiwa hiyo MOU imekidhi kisheria.
No binding kwenye MoU. In fact mimi sio mwanasheria lakini huwezi kwenda mahakamani kwa kutumia MoU maana haifungi kisheria.

Kwa msaada wa google;
A memorandum of understanding (MOU or MoU) is a formal agreement between two or more parties. Companies and organizations can use MOUs to establish official partnerships. MOUs are not legally binding but they carry a degree of seriousness and mutual respect, stronger than a gentlemen's agreement.
 
No binding kwenye MoU. In fact mimi sio mwanasheria lakini huwezi kwenda mahakamani kwa kutumia MoU maana haifungi kisheria.

Kwa msaada wa google;
A memorandum of understanding (MOU or MoU) is a formal agreement between two or more parties. Companies and organizations can use MOUs to establish official partnerships. MOUs are not legally binding but they carry a degree of seriousness and mutual respect, stronger than a gentlemen's agreement.
It is true that MoU is not legally binding but it may be admitted in the court of laws! Inaweza kukubalika mahakamani kama ushahidi ndiyo nimeeleza toka mwanzo! Siyo kila ushahidi au makubaliano lazima yawe legally binding ili yakubaliwe mahakamani.
 
Kusema ukweli huyu MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Profesa John Thornton, ni mtu very intelligent!. Anaishambulia kampuni tanzu yao ya Acacia Mining, ili tuu kuipa Tanzania confidence kuwa Barrick wako na sisi, hivyo kufanya mazungumzo na serikali yetu bila kuwahusisha Acacia, na chochote kitakachofikiwa kwenye mazungumzo ya Barrick na serikali yetu, ni nothing at all Kwa sababu the determinants sio serikali yetu wala sio Barrick, bali ni Acacia.

Mtoto wako akifanya kosa kubwa la kustahili adhabu Kali hata ya kifo, wewe baba ili kumnasua mwanao, utakuwa tayari kuthibitisha kuwa mwanao ni insane, hivyo insanity ni defence kwenye criminal cases.

Anachofanya Boss wa Barrick ni kuendelea kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa, huku Barrick wakiuza shares zao, Kwa sasa tayari wameisha uza 51% majority kwa Rangold na wao kubaki na 49%, next month mkutano mkuu wa share holders unaitishwa kubariki mabadiliko hayo, hivyo sisi kujikuta hatuna chetu!.

Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye uamuzi wa mwisho ni Acacia!, Kwanini hakushirikishwa?!. Je, Tutalipwa?. - JamiiForums

Je, wajua kuna uwezekano Barrick wanatuingiza mkenge?!. Hili la kugawana 50/50 ya faida ni kweli au ni changa la macho tu?. - JamiiForums

Mambo ya Barrick; Barrick Executive Chairman Thornton Ajiuzia Shares na kumiliki Shares Milioni 5!. - JamiiForums

Wakati Tukisubiri $ Milioni 300 zetu Kutoka Barrick, Yauza Hisa za $ Milioni 300 Kwa Mchina Huku Ikinunua Mgodi wa Randgold Kwa $ Bilioni 18.3!. - JamiiForums

Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa? - JamiiForums

P
Thornton kama Bashiru Ali tu. Hamna kitu.
 
Hatuwezi kusimamisha chochote, kwa sababu we have nothing to do with Barrick. We have everything to do with Acacia, and not Barrick, kuna vitu nikivisema humu, nitaonekana mtovu wa nidhamu kwa sababu baadhi ya wahusika wa majadiliano na Accia, sio tuu ni walimu wangu pale UDSM, bali wengine ni ma supervisor wangu wa LL.B dissertation, I don't know ni kwa nini walikubali kufanya negotiations na mtu ambaye is not part to contact, Barrick, na kumuacha Acacia ambaye ndiye mhusika mkuu!.

Barrick anaweza ku offload shares zake ndani ya Acacia, kwenye hostile takeover, bila Acacia wenyewe kujua kwa kuiuza kwa Mchina Ile 64% ya Barrick ndani ya Acacia, hivyo kujikuta hatuna wa kuzungumza naye!.

Tanzania kwenye multinational corporates negotiations, ni waupe na watupu kama vilaza wa chekechea.

Nikupe mfano mdogo wa kusikitisha.
Kwenye mkataba wa Richmond, kulikuwa na kipengele kuwa uamuzi wa MIGA ni final na conclusive, tukasaini.

Kisha tukavunja mkataba baada ya kuhakikishiwa hatutashitakiwa.
Tulishitakiwa, tunashindwa, tukadaiwa fidia, tukajidai hatulipi, kiukweli, tulilipa every cent Kwa siri!. Baadhi ya wanasheria wetu, tena wenye majina makubwa, na wengine Wana titles kubwa, hadi ma professors lakini ni bure kabisa!.
P
Hapa tz kwa msaada wa CCM vilaza kila kitu tunapigwa, kodi hawalipi wao wala hawajali na haiwaumi.
 
View attachment 893492
Ni Profesa John Thornton aliyekuja nchini kuonana na Rais JPM wakati wa sakata la makinikia.

Athibitisha msimamo wa tume ya makinikia kuwa ACACIA imekuwa na tabia ya kukwepa kodi Tanzania.

Asikitika kampuni hiyo kusababisha kuharibika kwa mahusiano ya kibiashara na serikali.

NA Mwandishi maalum
MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Profesa John Thornton, amesema kampuni yao ya Acacia Mining inayofanya kazi Tanzania, haijawahi kulipa kodi ya mapato (Coporate Income Tax) kwa serikali ya Tanzania kutokana na shughuli za uchimbaji wa dhahabu nchini suala ambalo limeathiri uhusiano baina ya kampuni hiyo na serikali.
Kauli hiyo ya Prof. Thornton inaleta matumaini kwa serikali ya Tanzania katika majadiliano yanayoendelea baina yake na Barrick juu ya tozo na kodi ambazo wanatakiwa kuilipa serikali kutokana na usafirishaji wa makinikia kwa miaka 19 tangu Acacia kuanza shughuli zake za uchimbaji nchini.
Tayari kampuni ya Barrick imeshakubali kulipa Tanzania dola milioni 300 kama utayari wa kushirikiana wakati majadiliano yakiendelea baina ya pande hizo.
Kwa mwaka mmoja na nusu sasa serikali imezuia usafirishaji wa makinikia (gold concentrate) nje ya nchi suala ambalo limeathiri utendaji kazi wa kampuni ya Acacia nchini kwa kiasi kikubwa pamoja na kusababisha kuporomoka kwa hisa zake katika soko la hisa la London.
Akizungumza katika mahojiano na The Globe and Mail mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu alisema Migodi ya Barrick inayomilikiwa na Acacia kwa asilimia 64 nchini Tanzania “hajalipa kodi ya mapato kwa Tanzania” zaidi ya kulipa mirabaha na kodi za mishahara tu.

Hata hivyo si Barrick wala Thornton ambao wamekanusha kuhusu ukweli wa kauli hiyo zaidi ya Barrick kujaribu kufafanua kuwa wanafikiri kuwa Mwenyekiti huyo alitia chumvi wakati akimaanisha kuwa kiasi kilicholipwa kwa serikali ya Tanzania ni kidogo sana ikilinganishwa na mapato ya Acacia katika shughuli za uchimbaji dhahabu nchini.
Kauli hiyo imeleta mgongano baina ya Barrick na Acacia baada ya Acacia kuipinga na kusema wanashangazwa na taarifa hiyo isiyo sahihi ya Thornton.
Kwa mujibu wa Globe, Acacia ikiwa imetolewa kwenye mazungumzo kati ya serikali ya Tanzania na Barrick, mafaili kwaajili ya kuunda mkataba mpya yamekabidhiwa kwa Kevin Thomson ambaye Mtendaji Mwandamizi wa Mikakati wa Barrick.
Kampuni ya Acacia iliingia katika kashfa ya usafirishaji wa makinikia na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha kwa mujibu wa tume ya uchunguzi iliyoundwa na Rais John Magufuli kuchunguza ukweli wa kiasi na thamani ya madini yaliyopo katika makontena ya makinikia yaliyozuiliwa.
Kamati hiyo ilibaini kuwepo kwa viwango vingi vya juu vya dhahabu ndani ya makinikia yaliyofanyiwa uchunguzi. Viwango hivyo ni kati ya 671 g/t hadi 2375 g/t, sawa na wastani wa 1400 g/t.
“Wastani huo ni sawa na 28 kg za dhababu kwenye kontena moja lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kwenye makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na wastani wa tani 7.8 za dhahabu yenye thamani ya TZS bilioni 676 (USD 307,292,720),” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa Mei mwaka jana na kuongeza;
“Aidha, kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwenye kontena moja lenye shehena ya tani 20 za makinikia (47.5 kg), kiasi cha dhahabu katika makontena 277 kitakuwa 13,157.5 kg ambazo thamani yake ni Sh trilioni 1.146 (USD 521,300,150).
“Hivyo, thamani ya dhahabu katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147.”
Kutokana na taarifa hiyo ya Kamati ya Mkinikia, Prof. Thornton alikutana na Rais Magufuli Juni 14 2017 na kufanya mazungumzo ambapo aliahidi kuwa Barrick ipo tayari kufanya majadiliano na serikali ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kuendesha shughuli zake hapa nchini.
Julai 31 2017 majadiliano baina ya pande hizo mbili yalianza huku upande wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi na baadae Barrick ikakubali kuilipa Tanzania Dola za Marekani Milioni 300 sawa na Sh bilioni 600.
Hatua hiyo ilifikiwa Oktoba mwaka jana wakati kamati mbili za majadiliano ile ya Tanzania na ya Barrick zilipokuwa zikiwasilisha ripoti ya mazungumzo yao kwa Rais Magufuli ambapo ikiwa ni mara yake ya pili kukutana na Rais Prof. Thornton alitoa salamu za shukrani na kusema kampuni yao italipa kiasi cha dola za Marekani milioni 300 kama njia ya kuonesha utayari wake na uaminifu kwa Serikali ya Tanzania.
Thornton alisema licha ya kuwa kwa sehemu kubwa wameafikiana masuala mengi, lakini suala ya tozo ya malimbikizo ya kodi bado hawajakubaliana kikamilifu na kwamba wameliweka kiporo wakati akiwasiliana na wanahisa wengine ili kufikia makubaliano zaidi.
Kauli yake ya sasa inaleta matumaini makubwa kwa serikali ya Tanzania kuwa huenda kiasi cha zaidi ya Trilioni 400 kilichokadiriwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kikalipwa na kampuni hiyo.
Baada ya Globe kuchapisha kauli hiyo ya Thornton, Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia, Peter Geleta aliibuka na kukanusha taarifa hiyo akisema kuwa si taarifa sahihi.
“Tulishangazwa sana na taarifa zisizo sahihi za Thornton na tumetaka Barrick watoe ufafanuzi,” aliiambia Globe.
Geleta alitoa ufafanuzi kwa wafanyakazi wake kupitia tangazo la ndani la Septemba 18 mwaka huu kuwa Acacia na kampuni zake tanzu umelipa dola bilioni 1 kama kodi na mrabaha kwa serikali kwa miaka zaidi ya 15.
Alisema kwa nusu ya mwaka huu wamelipa kodi ya mapato ya dola milioni 23.3 na mwaka jana dola milioni 34.6 na kwamba kwa miaka 15 wamelipa jumla ya dola milioni 140 kama kodi.
Mnaendelea na matumaini hewa, kwa Barrick hampati kitu.
 
Huko Tarime mara kuna viongozi na baadhi ya walimiki wa mgodi Barack wapo mahabusu mda huu baada ya kufikishwa mahakamani leo kwa ufisadi wa pesa kwa malipo ya milahaba kwenye maeneo ya migodi, wana JF fuatilieni huko mtapata taarifa zote.

Trump threatens 'large' sanctions on Turkey unless US pastor released
Donald Trump has threatened to slap “large sanctions” on Turkey unless Ankara frees an American pastor whose detention has further strained relations between the Nato allies.

The Trump administration escalated its pressure campaign the day after a Turkish court allowed Andrew Brunson to be transferred to house arrest after 21 months in detention. He is on trial on terrorism charges.

“The United States will impose large sanctions on Turkey for their long time detainment of Pastor Andrew Brunson, a great Christian, family man and wonderful human being,” Trump wrote in a tweet.

“He is suffering greatly. This innocent man of faith should be released immediately!“

Shortly before, the vice-president, Mike Pence, a devout Christian, leveled a similar threat directly at Turkey’s president, Recep Tayyip Erdoğan.

“To President Erdoğan and the Turkish government, I have a message on behalf of the president of the United States of America: release Pastor Andrew Brunson now or be prepared to face the consequences,” Pence said at a religious freedom event hosted by the US state department.
 
Mkuu mbona vyanzo vyangu vya huko wananiambia kuwa hakuna kinachoendelea kuhusu taharifahii
Ufisadi ni wa bilion 11 wapo jela kesho nunua gazeti la habari leo wataanika sakata lote yaani A-Z
 
It is true that MoU is not legally binding but it may be admitted in the court of laws! Inaweza kukubalika mahakamani kama ushahidi ndiyo nimeeleza toka mwanzo! Siyo kila ushahidi au makubaliano lazima yawe legally binding ili yakubaliwe mahakamani.

ACHA KUTUJAZIA UZI NA PUMBA ZAKO,
TOKA MWANZO UNAZUNGUUKA TU HUNA POINT, MWANZO ULIJIFANYA MOU INAKUBALIKA KISHERIA, GAFLA UNAJIFANYA KUKUBALI KUWA IS NOT LEGALLY ACCEPTED IN COURT OF LAW. TATIZO MKIISHA MALIZA MWAKA WA KWANZA MNAZANIA TAYARI NA NINYI MMEKUWA WANASHERIA-PATHETIC
ACHA AKINA MAYALLA WATUPE NONDO ZA KI WANAHABARI NA KISHERIA WEWE KUWA MCHANGIAJI KAMA SISI NA SIO MNYAMBULISHAJI WA SHERIA
 
Ufisadi ni wa bilion 11 wapo jela kesho nunua gazeti la habari leo wataanika sakata lote yaani A-Z

KWAMANTIKI HIYOMKUU CCM NDO INAHUSIKA, KINA MSANDO INABIDI WAZUNGUUKE TENA NA TUMEYAO YA KUWASAKA WALAKU WA CCM
 
Back
Top Bottom