Kigogo Mwingine wa CCM Arusha amfuata Millya Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigogo Mwingine wa CCM Arusha amfuata Millya Chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Apr 23, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,256
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Jinamizi la viongozi na Chama cha Mapinduzi (CCM) la kukihama chama hicho limeendelea kushika kasi, baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Arusha, Justine Genda, naye kutangaza kukihamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

  Genda ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Karatu Mjini, alitangaza uamuzi huo jana wilayani Karatu na tayari ameshapokelewa na viongozi wa Chadema katika hafla iliyohudhuriwa na Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Karatu Titus Lazaro na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Karatu, Thomas Darabe.

  Genda alisema ameamua kujiunga na wanaharakati wa kupigania haki na kuleta mabadiliko na kuongeza kuwa kwa sasa fursa hiyo inapatikana Chadema.

  “Nimeamua kuhama CCM na kujiunga na Chadema na nina matumaini makubwa kwani nimeona kuwa Chadema kuna fursa ya kumuwezesha kila mmoja kutoa mchango wake katika mchakato mzima wa mabadiliko na ni chama kinachoweza kuleta ukombozi wa kweli katika taifa,” alisema Genda.

  Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi ya Chadema mwanachama huyo, Lazaro aliwataka wanachama na viongozi zaidi wa CCM na vyama vingine wanaotaka mabadiliko ya kweli kujiunga na Chadema kwani ni chama makini.

  Wakati huo huo huko Ruvuma nako Katibu wa Chama Cha Tanzania Labour (TLP) Jimbo la Songea mkoani Ruvuma, Joseph Mkondora, amejiengua katika chama hicho na kujiunga na Chadema ambacho alisema ni chama pekee cha upinzani kinachoonyesha dira ya maendeleo kwa Watanzania.

  SOURCE:NIPASHE JUMATATU
   
 2. Mwanyasi

  Mwanyasi JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 5,560
  Likes Received: 1,646
  Trophy Points: 280
  Movement for change (wireless connection) mpaka Songea!
   
 3. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Asante sana M4C!
   
 4. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,756
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Hamia Chadema.....wewe, ndugu, jama na marafiki zako!!!!
   
 5. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,969
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huyu sio kigogo
   
 6. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,447
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Wakati huo huo huko Ruvuma nako Katibu wa Chama Cha Tanzania Labour (TLP) Jimbo la Songea mkoani Ruvuma, Joseph Mkondora, amejiengua katika chama hicho na kujiunga na Chadema ambacho alisema ni chama pekee cha upinzani kinachoonyesha dira ya maendeleo kwa Watanzania.


  Zaidi ya Chadema, kuna chama gani kingine cha upinzani?, karibu sana ndugu Nkondora
   
 7. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,710
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  masharti na vigezo kuzingatiwa!!!
   
 8. M

  Molemo JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,256
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Sawa mama porojo
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 10,995
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Garagaza sisiem mpk kieleweke!

  Hizi ni cha mtoto tu!
  Hata Salma Jk atatua chama makini hakika!

  Viva CDM pamoja na uongozi wote!!
   
 10. m

  matawi JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Badala ya hamia eyatel sasa imekuwa hamia chadema kudddddaaaadadeki iwarambe nsiwarambe?
   
 11. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 713
  Trophy Points: 280
  Muoneeni huruma Mzee wa kiraracha jamani ametia sahihi kutokua na imani na mtoto wa mkulima!!

  Kweli M4C, with no apology!!
   
 12. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 6,950
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Kubakia kwenye chama cha CCM ni sawa na kula nyama ya mtu! kwakua ukishakula nyama ya mtu huwezi kuacha!
   
 13. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,799
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ye mwenyewe anatamani kuhamia chadema
   
 14. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,615
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Pamoja viongozi wa M4c slaa na lema,2gether w wil go further.
   
 15. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,219
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160
  Kama Nape ni kigogo,hatakiwi CHADEMA kwa bure
   
 16. N

  N series Senior Member

  #16
  Apr 23, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa ni tume switch on bluetooth, wanatutafta wenyewe, we are expecting more makini people from magambaz territory.....
  Viva M4C
   
 17. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 28,635
  Likes Received: 28,452
  Trophy Points: 280
  unapenda vigogo?
  M4C with no apology, jiunge na crew ya kijanja jijini.
   
 18. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,452
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  Wewe ndio kigogo?
   
 19. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Rizi1 na Makamba tunawakaribisha maana hali ni tete sana ndani ya ccm
   
 20. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 9,831
  Likes Received: 3,104
  Trophy Points: 280
  usituletee upuuzi wa lusinde huku..alaa
   
Loading...