Sijastushwa na kitendo cha Balozi Polepole kujiuzulu ubalozi na utumishi wa umma kama alivyosema kwenye barua yake kwa kuwa toka mwanzo hakupenda jinsi alivyotolewa kwenye ubunge na nafasi yake akapewa Vuai Shamsi Nahodha.
Haikueleweka kipindi kile kama mbunge wa kuteuliwa anaweza kuvuliwa ubunge na nafasi yake kupewa mtu mwingine!.Kwa kuwa tulikuwa na kawaida ya kukaa kimya na kupuuza mambo hatukuona lile ni tatizo lakini sasa ndiyo jipu limepasuka tunaparanganga kutafuta matambara ya kufuta usaha unaosambaa kwa kasi sana.!
Balozi Polepole amestafu na ameandika barua nzito na kali sana na imetoa shutuma kali sana dhidi ya uongozi wa nchi!. Kitendo cha Balozi Polepole kusema nchi imekosa uongozi ni shutuma nzito sana na hazipaswi kuachwa zipite kimya kimya! Lazima tukiri kuwa kuna tatizo mahali na lazima litazamwe kwa makini sana kama tunaipenda hii nchi.
Kilichonistua zaidi ni kitendo cha Balozi Polepole kukimbilia Sweden na kuomba hadhi ya ukimbizi na kupewa mara baada ya kuandika barua ya kujiuzulu yenye shutuma kali sana dhidi ya uongozi wa nchi.
Kitendo hiki ni kizito na kigumu na kibaya sana kwa taifa na uongozi wa taifa.! Balozi Polepole kaomba ukimbizi Sweden maana yake anahofia usalama wake baada ya kusema aliyoyasema!
Tunapaswa kujitafakari kama taifa!.. Hatuko kwenye njia sahihi na kwa kweli giza ni nene sana huko tuendako.
Pia soma > Humprey Polepole ajiuzulu Ubalozi, asema hawezi kuendelea kuwa sehemu ya uongozi usiohamasika na utii wa misingi ya katiba na chama