Kigamboni ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete bado ipo au imezikwa?

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,802
Wakati Jakaya anaondoka aliacha mpango kabambe wa kuujenga mji wa kisasa Kigamboni. Ni mji ulitajwa kuwa Dubai ya Afrika Mashariki.

Lakini toka aingie Jiwe mradi hauzungumzwi tena. Ni kama umekufa na haupo tena.

Juzi wakati anazindua Wilaya ya Kigamboni kuna kauli aliziongea kengele ya tahadhari ikagonga kichwani kwamba Mbagala inahamia Kigamboni. Maana alitamka kuwa anairudisha ardhi kwa wananchi wagawiwe viwanja bila kuisahau CCM.

Mwenye taarifa rasmi anisaidie maana kama ule mradi ungekamilika angalau na sisi bongo tungekuwa na sehemu ya kujidai kama majiji ya Johannesburg, Pretoria n.k.

Ramani yake ilikuwa ya kijanja sana ikiwa na Shopping Malls za kijanja, maduka makubwa, viwanja vya michezo, majumba ya starehe, bustani nzuri majengo ya kisasa kabisa beach za kuvutia n.k.

Hata kama kulikuwa na makosa fulani kwenye mradi wa awali nadhani yangerekebishwa bila kuathiri wazo lenyewe.

Maendeleo hayana vyama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Under JK kulikua na projects nyingi proposed ili ambazo kama zingetiliwa maanani, basi Dar asa hivi tungechuana vikali na Cape Town. Jo'burg, Cairo n.k

New Kigamboni City, Kurasini EPZ, Old Ubungo Interchange Design, Coco Beach Project, Kurasimisha Uswazi kuwapa NHC wajenge flats za floor 5 (i.e Manzese, Tandale, Vingunguti, Mbagala, Tandika, Keko n.k )

Ila baada ya kuingia huyu jamaa, sijui yukoje asee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaaani ukiondoa SGR,na Stiglers mi simuelewi kabsaaa! Ameifanya TZ kuwa nchi ya wachuuzi. Anatangaza TZ ya viwanda wakati anawachukia matajiri. Kuwa tajiri awamu hii ni sawa na kuwa mhaini. Praise team wanasifia hadi ujinga. Na wanavyozidi kumsifu ndo anazidi kuyakoroga. kifusi boy,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom