Tukumbushane kazi alizofanikisha Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
5,270
7,932
Mengi sana yanasemwa kuhusu mafanikio ya Mwendazake kama vile watangulizi wake hawakufanya lolote. Kimsingi JK amefanya kazi kubwa sana. Kimsingi amefanya hata kazi za awali kwa yale aliyoyakamilisha Mwendazake kama uwanja wa Terminal III, Daraja la Mfugale, Daraja la Kijazi, SGR na barabara za Dar es Salam Metropolitan Project.

Mambo "kiduchu" aliyofanya Jakaya;

1. Daraja la Kigamboni
2. Daraja La Kilombero
3. Daraja la Umoja
4. Daraja la Maragarasi
5. Chuo Kikuu cha Dodoma
6. Hospitali ya Mloganzila
7. JNIA terminal III
8. DART(Mwendo kasi)
9. Sekondari za Kata nchi nzima kila kata ina shule.
10. Mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria
11. Songwe Airport
12. Kigoma Airport
13. Tabora Airport
14. Umeme wa REA
15. Benjamin Mkapa hospital Dodoma
16. Chuo kikuu cha Nelson Mandela Arusha
17. Dangote industry
18. Bomba la gesi Mtwara Dar
19. Kinyerezi I&II
20. Hospitali ya Moyo
21. MOI
22. Nchi nzima kuunganishwa kwa barabara za lami(zaidi km 14000 zilijengwa nchi nzima)
23. Umeme kwa makao makuu ya wilaya
25. Ujenzi wa Mkongo wa taifa wa mawasiliano(leo tunajimwambafai na internet matunda ya JK)
26. JNICC Conference center(Ukumbi wa kisasa)
27. Hata CCM wenyewe aliwajengea ukumbi wa kisasa Dodoma.
28. Nyongeza ya mishahara kwa watumishi kila mwezi julai
29. Ajira kila mwaka
30. Annual Increment ilikuwa haki ya Mtumishi.
32. Diplomasia ya kimataifa ilikuwa juu katika ukanda wa maziwa makuu.
33. Demokrasia iliyopevuka
34. Aliwagomea CCM na kuwaambia hoja za kisiasa hujibiwa kisiasa, sio kwa kipigo cha polisi.

Hayo ni machache ya Jakaya Mrisho Khalfani Kikwete lakini hakujimwambafai.

Hawa wanaomtukana na kusema kuwa hakufanya chochote zaidi ya wizi na ufisadi walikuwa wanaishi nchi gani?

Hivi huyo wanaemtukuza amefanya jambo gani kubwa linalofikia hata robo ya mkubwa aliyoyafanya Kikwete?

Kwakuhitimisha Kikwete alifanya makubwa na Mikopo aliyokopa kila mmoja ananufaika nayo na vitu vinaonekana.

👉Kubwa zaidi lingine aliwaunganisha watz kwa pamoja bila kujali vyama vyao tofautu na sasa ambapo mpinzan anaonekana kama adui.
 
"....pesa za epa siyo za serikali...."

bunge la katiba liliowainua akina Makonda, binti Burembo kuwa wanasiasa makini, Mh. Vick Kamata, Magige, nk walipata upenyo wa kufaidi keki ya taifa kwenye awamu yake (sasa hivi wanakimbizana na mirathi) Mtwara ikatawaliwa Kijeshi, watu ambao hata kuongoza kijiji wasingeweza ila waliweza kuwania Urais wa JMT maana ilionekana kumbe inawezekana!
 
75% ya list hiyo ilifanywa na JPM kwa kulazimisha akiwa waziri wa ujenzi😜!
Jakaya alifanikiwa kukaa angani kwa masaa mengi zaidi kuliko hata rubani wa ndege mashuhuri!
Waziri yeyote chini ya leadership sahihi angeweza kutekeleza, lazima credit zimuendee Rais aliyekuwa anaudhinisha mafungu ya fedha no matter anasafiri sana angani. Kudos JK
 
Kikwete alifanikisha Kushamiri kwa biashara ya madawa ya kulevya yaliyoathiri kizazi Kizima cha nguvu kazi ya waTanzania!

Alinajisi utaratibu wa nchi kupata katiba mpya baada ya matumizi makubwa ya fedha za walipa kodi.

Aliingiza rushwa katika nchi kwa kuwaingiza wafanyabiashara kwenye siasa za chama tawala.
 
"....pesa za epa siyo za serikali...."

bunge la katiba liliowainua akina Makonda, binti Burembo kuwa wanasiasa makini, Mh. Vick Kamata, Magige, nk walipata upenyo wa kufaidi keki ya taifa kwenye awamu yake (sasa hivi wanakimbizana na mirathi) Mtwara ikatawaliwa Kijeshi, watu ambao hata kuongoza kijiji wasingeweza ila waliweza kuwania Urais wa JMT maana ilionekana kumbe inawezekana!
Kwa uwezo mdogo na vituko vya Hayati Magufuli,kama aliweza kuwa raisi wa nchi hii,hivi kuna mtu wa kushindwa kuwa raisi katika nchi hii?
 
🙌🙌🙌. Umesahau mafanikio mengine ya JK ni;
1. Magorofa ya makazi ya wanajeshi kila kambi nchi nzima
2. Usafiri wa polisi nchi nzima (Land Cruiser 1200)
3. Vituo vya afya nchi nzima
4. Vyuo vikuu kutoka 8 hadi 40 nchi nzima
5. Mikopo ya elimu ya juu mpaka kufikia 💯
Asante kwa kuongezea Mkuu Last emperor. Tuendelee kutetea kazi za viongozi wetu waliomtangulia Mwendazake, maana yeye aliamua kujenga propagada za UWONGO.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom