Kigamboni: Moto wateketeza takribani Maduka 24 eneo la Feri

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,724
2,000
Wana Kigamboni kuna ajali ya moto Ferry maduka ya scaba scuba yanaungua moto.

Kuna moto unawaka kwenye nyumba yenye Maduja mengi maeneo ya Ferry karibu na kituo cha mafuta cha Kobil.

Fire wapo lakini moto bado unawaka. Wenye maduka bora wakawahi kuangalia Usalama wa Mali zao.

Maduka yanayokadiriwa kufikia 24 yameteketea kwa moto.
51712cbbd28968bfa99891d95fb61e45.jpg
57c44417af01e2a5d69f23afc6fcec4a.jpg
ceaea7e2300e5f595fc8b4d80a48df0e.jpg
c3151e842d7ff5a79b516adb8a5d01c5.jpg

POLENI WAHANGA WA AJALI YA MOTO KIGAMBONI.

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa, leo tarehe 11/4/2017 ametembelea eneo la ferry kufatia ajali ya moto iliyotokea maeneo hayo.

DC Mgandilwa akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, amejionea madhara yaliyosababishwa na moto ambao inasemekana ulianza majira ya saa 6 za usiku na chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

DC amewapa pole wahanga wa ajali hiyo ambao Maduka yao yameungua. Amewasihi kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho serikali ya wilaya inafikiria cha kufanya baada ya tathimini ya hasara iliyojitokeza kuwa imekamilika.

DC Mgandilwa amewakumbusha wafanya biashara uhumimu wa kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika maeneo ya biashara zao kama fire extinguishers nk. Pia amewaambia kuwa na utamaduni wa kuziwekea bima biashara zao ili Majanga yanapotokea waweze kulipwa hasara inayokuwa imejitokeza.

Kuhusu magari ya zimamoto ya wilaya ya Kigamboni, DC Mgandilwa amesema kuwa wanajipanga kama wilaya Mpya kupata magari ya Zima moto licha ya kwamba kwa sasa wamekuwa wakitumia magari ya TIPPER na wilaya za jirani moto unapotokea.

Aidha, amewapongeza jeshi la Zimamoto kwa kajitahidi kuwahi katika eneo la tukio mara tu walipopata taarifa licha ya kuwa walipewa taarifa moto ukiwa umeshaenea katika eneo kubwa ya jengo hilo lenye jumla ya Maduka 25, hata hivyo waliweza kuokoa Mali katika maduka 3 yaliyopo katika jengo lililoungua.
 

Jembekillo

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
4,536
2,000
usiwe na hofu endelea na kazi zako hao wamechoma wenyewe ili walipwe na bima
 

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,678
2,000
Dah! Hapo ungumu wa maisha ndio unapoongezeka... Mtu unatamani ujitoe duniani ukaanze maisha mapya sehemu nyingine...
 

Wi-Fi

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
2,082
2,000
Bima hawalipi kizembe,lazima waangalie proximate cause
Licha ya iyo "proximate cause" vipi je hao wafanya biashara walikatia bima ya bidhaa wanazouza? Vipi hasara watakayo pata kwa kutokuwa na eneo lingine la kufanyia biashara kwa haraka?

Nitoe wito kwa wafanya biashara wote kuangalia utaratibu wa bima kwenye majanga kama haya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom