Kigali: Watu wajazana kumuona Diamond Platnumz

Janvier

New Member
Aug 18, 2011
2
4
Nyamirambo - Kigali, Watu kutoka huku na kule walifurika siku ya Jumamosi Januari 20, 208 kumuona mubashara msanii wa kitanzania Diamond Platnumz.

Msanii huyo alikwenda sehemu inaitwa Tapis Rouge iliyoko tarafani Nyamirambo, wilayani Nyarugenge mjini Kigali, ili kuwasalimu mashabiki wake ambao walikuwa wamejitokeza kwa wingi.

Wakati wakitaraji kumuona akiwatumbuizia nyimbo zake, Diamond kwa muda wa dakika kama 20 alizokuwa sehemu hiyo hakuimba wimbo wowote bali alipita katikati ya umati wa watu akiwapungia mikono kama mfalme na baadaye kuwasambazia karanga zake za Diamond Karanga bwerere.

Diamond aliwasili mjini Kigali siku ya Ijumaa Januari 19, 2019, kwa ajili ya kuwatembelea watoto wenye ulemavu wa macho waishio tarafani Gatsata wilayani Gasabo mjini Kigali katika kituo cha Jordan Foundation, ambao aliahidi kugharamia matibabu yao kwa muda wa mwaka mmoja.

Baada ya kuwatembelea watoto hao alikutana na waandishi wa habari kwa mahojiano ambapo alipata kuzindua Diamond Karanga na Chibu Parfume na kuweka bayana mipango yake mingine ya kuanzisha Wasafi FM na Wasafi TV mwaka huu, na hata kuzindua albamu yake nyingine yenye jumla ya nyimbo zisizopungua 18, kwa mujibu wa maelezo yake.

Amesema anataka hata kufungua tawi la lebo yake ya WCB nchini Rwanda, akisema anaamini Rwanda kuna vipaji vingi lakini wasanii hawapati studio zenye uwezo mkubwa wa kuwainua kumuziki.

Amesema pia kuwa anataka kuwa na makazi Rwanda, na kesho yake alipelekwa sehemu tofauti ambazo kuna nyumba nzuri ili azikague na achague anayoona inamfaa. Kaisifia Rwanda kwa usalama na usafi na kusema ameona ana kila sababu ya kuwa na makazi Kigali.

Hizi hapa chini ni picha za jinsi watu walivyofurika Nyamirambo kumuona ambapo wengine walilazimika kusimama juu ya pikipiki zao ili waweze kumuona.
 
Attachments

  • Diamond 1.jpg
    Diamond 1.jpg
    72.3 KB · Views: 143
  • Diamond 2.jpg
    Diamond 2.jpg
    82.3 KB · Views: 150
  • Diamond 3.jpg
    Diamond 3.jpg
    58.7 KB · Views: 115
  • Diamond 4.jpg
    Diamond 4.jpg
    89.6 KB · Views: 137
  • Diamond 5.jpg
    Diamond 5.jpg
    83.5 KB · Views: 124
  • diamond_n_abajyanama_be_basohotse_by_akanya_gato_asuhuza_abafana_asubira_mu_modoka-d99ec.jpg
    diamond_n_abajyanama_be_basohotse_by_akanya_gato_asuhuza_abafana_asubira_mu_modoka-d99ec.jpg
    72.3 KB · Views: 91
Asante sana diamond kwa kututoa kimaso maso kwenye muziki tumetoka kuwa vichwa vya wendawazimu mpaka kusumbua nchi za watu..

wametuonea sana kina pepe kale, kofi olomide, yondo sister zamani walikuwa wanakuja bongo tunawashangilia na kujaa kama nini.. leo mtanzania anaenda ugenini watu wanamshangilia,.... raha sana

ajira hizo za WCB tv na redio ni ukombozi pia kwa vijana wetu...
 
Wale watoto wakare wa Kinyarwanda mbona siwaoni kwenye hizi picha? Ninachokiona ni 'ma polygon' tu!
 
Ali Kiba ashaimba na R Kelly unataka kufananisha na wanyarwanda?
 
Nyamirambo - Kigali, Watu kutoka huku na kule walifurika siku ya Jumamosi Januari 20, 208 kumuona mubashara msanii wa kitanzania Diamond Platnumz.

Msanii huyo alikwenda sehemu inaitwa Tapis Rouge iliyoko tarafani Nyamirambo, wilayani Nyarugenge mjini Kigali, ili kuwasalimu mashabiki wake ambao walikuwa wamejitokeza kwa wingi.

Wakati wakitaraji kumuona akiwatumbuizia nyimbo zake, Diamond kwa muda wa dakika kama 20 alizokuwa sehemu hiyo hakuimba wimbo wowote bali alipita katikati ya umati wa watu akiwapungia mikono kama mfalme na baadaye kuwasambazia karanga zake za Diamond Karanga bwerere.

Diamond aliwasili mjini Kigali siku ya Ijumaa Januari 19, 2019, kwa ajili ya kuwatembelea watoto wenye ulemavu wa macho waishio tarafani Gatsata wilayani Gasabo mjini Kigali katika kituo cha Jordan Foundation, ambao aliahidi kugharamia matibabu yao kwa muda wa mwaka mmoja.

Baada ya kuwatembelea watoto hao alikutana na waandishi wa habari kwa mahojiano ambapo alipata kuzindua Diamond Karanga na Chibu Parfume na kuweka bayana mipango yake mingine ya kuanzisha Wasafi FM na Wasafi TV mwaka huu, na hata kuzindua albamu yake nyingine yenye jumla ya nyimbo zisizopungua 18, kwa mujibu wa maelezo yake.

Amesema anataka hata kufungua tawi la lebo yake ya WCB nchini Rwanda, akisema anaamini Rwanda kuna vipaji vingi lakini wasanii hawapati studio zenye uwezo mkubwa wa kuwainua kumuziki.

Amesema pia kuwa anataka kuwa na makazi Rwanda, na kesho yake alipelekwa sehemu tofauti ambazo kuna nyumba nzuri ili azikague na achague anayoona inamfaa. Kaisifia Rwanda kwa usalama na usafi na kusema ameona ana kila sababu ya kuwa na makazi Kigali.

Hizi hapa chini ni picha za jinsi watu walivyofurika Nyamirambo kumuona ambapo wengine walilazimika kusimama juu ya pikipiki zao ili waweze kumuona.
Mtoa uzi umekosea huyu ni mwanamuziki wa Kimataifa
 
Kuna wakati. fulani miaka ya nyuma nilikutana. na demu wa Kikenya,nikamtongoza,alinieleza kuwa Kenya wanapenda miziki ya Tanzania,wanapenda maudhui iliyopomo ndani ya miziki ya bongo(waimbaji wana sauti nzuri,ujumbe ndani ya muziki una ujumbe murua!,na sauti nzuri.!!!
 
Tanzania ipo sauti nzuri ,na mistari yenye hisia kali ya mapenzi!
 
Back
Top Bottom