Kifurushi cha internet cha Halotel cha 500MB huyeyuka fasta!

Kuna hiki kifurushi cha chuo cha 500MB nashangaa huwa kinaisha fasta sijui ni cha kichina? Kinaisha fasta kwa kuperuzi tu bila hata kudownload chochote! Nyie mliowahi kukitumia mnakionaje?
Kweli kabisa aise. Sijui hizi 500 MB zinayeyuka juani?
 
Tigo ndio wamezidi kabisaa,yaani ukiweka tu Mb 500,umeliwa hata dk 20 hazipiti.Unajiuliza wamekulaje haupati jibu.ukiwapigia wanakuambia ulikuwa unatumia internet eboo! net gani wakati tangu nijiunge sijaingia huko utasikia ohh uliacha data on, saasa unajiuliza kama kusinge kuwa na Mb na data ipo on wangekula nini?
 
Umejiunga IG,SNAPCHAT,YOUTUBE,WHATSAPP....Tena speed unatumia 4G NA unastream muda wote..then utegemee muujiza....
Hapana.....Binafsi MB 500+100 za Halotel (kwa jelo tu) natumia siku nne mpaka tano hapa kwa laptop yangu.
 
Mimi siku moja tuu 500mb zinaisha, zamani ilikuwa siku tatu mpaka nne, sijui tatizo nini au ndio zile tabia zetu za ujanja ujanja
 
Back
Top Bottom