Halotel fiber

Halotel fiber

DexterLab

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2024
Posts
432
Reaction score
564
Ukitembea kwenye mitaa ya makazi Dar es Salaam, Mwanza, au Dodoma, utaona picha inayochanganya kidogo. Kwenye nguzo kama za umeme, kuna nyaya za mtandao zimetandazwa hadi mitaani ambako familia nyingi bado zinategemea bando za kawaida za simu. Wakati huo huo, TTCL wanaomiliki Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) wameweka nguvu zao kwenye majengo ya serikali na mitaa ya kitajiri tu.

Kwa upande mwingine, kuna dhoruba mpya ya ruta unlimited ya mchongo ambazo zimeteka soko la nyumba nyingi. Watu wengi wanaamini kuwa ruta hizi za bila waya ndizo hatima ya baadaye ya intaneti ya nyumbani nchini Tanzania.

Lakini ukichunguza kwa umakini, ruta hizi si hatima—ni suluhisho la muda tu. Vita halisi ya intaneti ya nyumbani inapigwa chini kwa chini, na mfumo unaowekwa kimyakimya mitaani ndio unaenda kumiliki soko hili lote na bado wengi hawaja jua bado.

Ruta za nyumbani za bila waya zinapata umaarufu kwa sababu ni rahisi kuzinunua na kuzichomeka tu, lakini zina gharama kubwa na changamoto kubwa. Kifurushi cha kawaida cha Mbps 20 kwenye ruta ya bila waya kinagharimu takriban TZS 70,000 kwa mwezi, wakati gharama ya spidi hiyo hiyo na zaidi ya hapo kwenye intaneti halisi ya FAIBA ni takriban TZS 50,000 tu pengine au pungufu ya hapo.

Mbali na bei, mawimbi ya bila waya yanabanwa na msongamano pindi watu wengi wanapoingia mtandaoni usiku, pamoja na kuathiriwa na hali ya hewa. Watumiaji wanaonunua ruta hizo wanaanza kugundua haraka kuwa minara ya simu inayotumiwa na watu wengi haiwezi kulingana na utulivu wa faiba inayovutwa kama umeme hadi nyumbani.

Airtel kwa sasa inatawala soko la ruta za bila waya, lakini muundo wa biashara yao una ukuta mgumu mbele yake. Airtel haina mbinu wala miundombinu mikubwa ya kebo za Fiber za majumbani. Minara ya simu haiwezi kuendelea kuongezwa uwezo bila kikomo ili kuhimili matumizi makubwa ya majumbani kama kutazama TV za 4K au kufanya kazi mtandaoni (Hususani content, make kila mtu sasa hivi creator). Siku wateja wa ruta za bila waya watakapochoshwa na msongamano na kutaka kuhamia kwenye kebo halisi, Airtel haina faiba wala miundombinu ya kutosha mitaani za kuingiza majumbani mwao.

Kwa upande wa TTCL, wao wanamiliki barabara kuu (mkongo wa taifa), lakini wamepuuzia njia za kuingia milango ya watu. Kuelekeza nguvu kwenye majengo ya serikali na mitaa ya kitajiri pekee kumeacha maeneo makubwa ya mitaa ya kawaida ikiwa wazi kabisa bila huduma ya faiba, na voda pia wanafanya mchezo huu huu tu.

Katikati ya utulivu huu, Halotel ndiyo inayocheza mchezo wa akili wa muda mrefu na kuibuka kidedea kwenye soko hili.

Kwa kutandaza kebo za fiber mitaani mapema kabla hata maombi hayajaongezeka, Halotel inatekeleza mbinu ya kiufundi ya kumiliki eneo mapema:

Siku familia inagundua kuwa ruta yao ya bila waya ni ghali au ina msongamano, inagundua pia kuwa faiba ya Halotel tayari inaning'inia kwenye nguzo ya umeme nje ya geti lao. Mchakato uliopaswa kuchukua wiki kadhaa unakuwa kazi ya masaa 24 tu.

Mara tu Halotel inapotandaza nyaya zake kwenye mtaa fulani, inatengeneza ukuta mgumu wa kuzuia wapinzani kama TTCL au Vodacom kuingia. Hakuna kampuni itakayokubali kuingia gharama za kutandaza nyaya zake kwenye mtaa ambao tayari Halotel ina faida ya kuwahi kwanza na gharama nafuu za kuunganisha wateja au tayari inawateja huko.

Mwingine anaye jitahidi hapa ni Savannah ila yupo Dar na Dodoma tu, kwa sasa hivyo bado mpinzani wa kweli kwenye hii sekta ni HALOTEL, na tofauti na mitandao mingine yeye ana kibali kabisa toka serikalini cha kusambaza mkongo.

Ruta za bila waya ni hatua ya kwanza tu ya kuonjesha Watanzania ladha ya intaneti ya nyumbani. Kadri uelewa wa kidijitali unavyokua na matumizi ya data kuongezeka, watumiaji watadai intaneti ya faiba halisi iliyo ya bei nafuu, ya haraka, na isiyo na kikomo. TTCL inaenda taratibu mno, Airtel, voda na Yas hawana nyaya za kutosha mitaani, na Halotel tayari ipo nje ya geti lako ikisubiri uichomeke tu.

Ni mawazo yangu, na ninakubali kabisa kukosolewa.
1791290923018.jpg
 
Ni mawazo yangu, na ninakubali kabisa kukosolewa.
Mambo ya copy and paste
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom