Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,639
HADITHI: KIFO SIKU YA HARUSI YANGU
MTUNZI : ERIC J SHIGONGO
MWANZO
Mamia ya watu walikuwa wamefurika ndani ya ukumbi wa Pundamilia ulio ndani ya hoteli ya maarufu ya Atrium, karibu kila mtu maarufu nchini Tanzania alikuwa ndani ya ukumbi huu. Kuanzia Rais, Mawaziri, Makatibu Wakuu, wanamichezo, wasanii na wafanyabiashara wakubwa wa Kiasia na Afrika. Hakika ilionekana siku ya furaha, watu wakiwa wameketi kwenye meza zao wakiendelea kunywa vinywaji taratibu.
Wanaume wakiwa wamevalia suti nyeusi na wanawake magauni ya rangi nyeupe na zambarau, hakika walipendeza. Kila nilipozungusha macho yangu huku na kule ndani ya ukumbi nilionekana kutoamini kilichokuwa kinatendeka, hatimaye baada ya safari ndefu ya kupanda na kushuka milima, nilikuwa namuoa Bianca Rwegoshora, mtoto wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wazazi na ndugu wa pande zote mbili walionekana kufurahia kila kitu kilichokuwa kikitokea ukumbini, kwao hakika ulikuwa ushindi, walikuwa wamefanikisha kutokea kwa jambo ambalo kwa muda mrefu walilihangaikia sana, kuhakikisha kwamba namuoa Bianca badala ya Farida Mbaraka, kisa tu alikuwa ni mtoto aliyetokea familia duni, wazazi wake wakiwa hawana elimu hata ya darasa la saba. Hicho ndicho kilikuwa kikwazo, hakuna aliyeuangalia uzuri wake, wala ukarimu wa moyo wake, alihukumiwa sababu ya umasikini wake, hakika iliuma.
Asilimia kubwa ya ndugu zangu waliokuwa ukumbini, macho yangu yalivyowapitia, sikumpata hata mmoja ambaye hakuwa na digrii! Wengi walikuwa ni madaktari, maprofesa, wenye elimu ya chini kabisa walikuwa ni wenye digrii moja pamoja na wanafunzi waliokuwa vyuoni na sekondari ambao pia walitegemea kuingia kaburini wakiwa na digrii si chini ya tatu.
Hiyo ndiyo ilikuwa familia yangu, familia ya wasomi, walioheshimu watu kwa alama zilizotangulia majina yao, mfano Dk., Injinia, Mchumi, Mwanasheria, n.k. Mtu yeyote ambaye hakuwa na vitangulizi vya taaluma yake, hakuheshimiwa na familia yangu. Hicho ndicho kilichompata Farida Mbaraka, kwa sababu ya familia yake kutokuwa na elimu, alionekana kama kinyaa, ingawa nilimpenda mno, baadhi ya ndugu zangu waliomo ukumbini wakishangilia, walimkashfu na kusema kwamba kumuoa ingekuwa ni kutumia sheria iitwayo “The Dilution Law”.
“Mtoto huchukua akili kutoka kwa baba na mama, ukiwa na akili nyingi, halafu ukaoa mwanamke au kuolewa na mwanaume asiyekuwa na akili, mtoto wako atakuwa na akili kidogo, lakini ukioa mwanamke au kuolewa na mwanaume mwenye akili nyingi, lazima watoto wako watakuwa vipanga sana darasani!” Hayo yalikuwa ni maneno ya Joackim, mtoto wa baba yangu mkubwa ambaye yeye katika umri wa miaka thelathini tu alikuwa anasomea digrii ya tatu nchini Marekani. Alikuwepo ukumbini akishangilia juhudi zake za kuhakikisha simuoi Farida bali Bianca, ambaye karibu familia yake yote ilikuwa ni ya wanasheria.
“Genesis!” Ilikuwa ni sauti ya Bianca akiniita, nikageuza kichwa changu kumwangalia, ili kumfanya asigundue kwamba nilikuwa na mawazo, niliusogeza mdomo wangu karibu na wake na kumbusu, wapiga picha wakafanya kazi yao.
“Yes sweetie!” (Ndio mpenzi)
“What is going on your mind?”( Nini kinaendelea kichwani mwako?)
“Why?”(Kwanini?)
“You seem to be contemplating too hard!”(Unaonekana kufikiria sana)
“No! I am just thinking about our future, where we have come from, where we are and where we are going!”(Hapana! Nafikiria tu kuhusu maisha yetu ya baadaye, tulikotoka, tulipo na tunakokwenda!)
“Isn’t Farida on your mind?”(Farida hayupo kichwani mwako?)
“Me? No way! That drug dealer? Probably she is dead by now.”(Mimi? Huyo muuza madawa ya kulevya? Labda amekwishakufa tayari) niliongea nikichukua kitambaa na kujifuta machoni.
Si kweli kwamba nilikuwa simpendi Farida, kila jina lake lilipotajwa huzuni iliniingia na machozi kunilengalenga, nilimpenda sana msichana huyo na katika maisha yangu sikuwahi hata mara moja kukutana na msichana wa aina yake. Alikuwa na sifa zote, kuanzia uzuri wa sura na maumbile mpaka tabia na mwenendo wake na hicho ndicho nilichohitaji kutoka kwa mwanamke wa kuishi naye maisha, sifa ambazo wazazi na ndugu zangu katu hawakuziona, kwao kitu cha muhimu kilikuwa ni elimu.
“Then why are you so sad? Are you not happy that we are finally married?”(Sasa kwanini una huzuni siku ya harusi yetu? Haufurahii kwamba hatimaye tumeoana?)
“I am so happy and excited, though I can’t stop myself thinking of Farida.”(Nina furaha sana ingawa siwezi kujizuia kumfikiria Farida)
“But a few minutes ago you said she is not on your mind!”(Lakini dakika zilizopita ulisema hayupo akilini mwako)
“Let me just be brutally honest with you! I can’t stop thinking of Farida.”(Acha tu niwe muaminifu kupita kiasi, siwezi kuacha kumfikiria Farida) niliongea nikimwangalia Bianca, akainamisha kichwa chake chini kuonyesha maelezo yangu yalimwumiza, lakini ilikuwa ni bora aumie akiwa ameambiwa ukweli.
Haikuwa rahisi kumsahau Farida, kila siku alisumbua akili na mawazo yangu, mpaka wakati huo nilikuwa sijaamini kabisa kwamba alikuwa ni mfanyabiashara wa dawa za kulevya, aliyekamatwa na madawa hayo nchini Saudia Arabia siku chache tu kabla ya kumvisha pete ya uchumba na kilichokuwa kikisubiriwa ni kupigwa risasi mbele za kadamnasi, hiyo ndiyo ilikuwa adhabu ya watu waliokamatwa na madawa hayo katika nchi za Uarabuni.
“Lakini aliondoka kwa lengo la kwenda kufanya usaili ili ajiunge na Chuo Kikuu cha Riyadh, naye akitamani awe angalau na digrii na familia yangu iweze kumkubali. Alifanya kila kilichowezekana ili wazazi wangu wampende. Hivi ni kweli Farida alikuwa akifanya biashara ya madawa?” nilijiuliza bila kupata majibu.
Ingawa Bianca alikuwa kando yangu, tena siku ya harusi yetu bado kichwani mwangu alikuwemo Farida, fikra za kwamba angekuwa amekwishapigwa risasi mpaka wakati huo zilinisumbua sana kiasi cha kunifanya nisifurahie kitu chochote kilichokuwa kikiendelea ukumbini ingawa karibu kila mtu alishangilia mimi na Bianca kufunga ndoa. Nilichotaka kufanya wakati huo ni kuondoka ukumbini kwenda chumbani kupumzika.
Ghafla nilisikia mlio wa ujumbe wa simu kwenye simu yangu, nikijua ni kutoka kwa baadhi ya rafiki zangu waliokuwa wakinitumia ujumbe wa pongezi. Nilinyoosha mkono na kuichukua simu yangu mezani, kisha kufungua sehemu ya ujumbe na kuanza kusoma, moyo wangu ulishtuka nilipoona maneno “Siri kubwa”. Nikazidi kusogea chini ambako kulikuwa na anuani ya barua pepe ya Bianca, pia ikiwa na alama yake ya siri ya kufungulia kama kuna mtu alitaka kusoma. Chini yake kukiwa na maandishi “Tumekuletea hii, ili uingie kwenye sanduku la barua pepe la mkeo, ili upate kumwelewa vizuri na unyama aliomfanyia Farida.”
Moyo wangu ukaruka mapigo kadhaa, jasho likaanza kunitoka, huku nikihisi kama vile shinikizo langu la damu lilikuwa likishuka kwa kasi. Sikutaka tena kukaa ukumbini, ujumbe huo wa simu ndio ulichochea kabisa hamu yangu ya kuondoka kwenda chumbani kupumzika ambako lengo langu lilikuwa ni kwenda moja kwa moja kwenye kompyuta na kufungua anuani ya barua pepe ya Bianca na kujionea kilichokuwemo ndani. Moyoni nilijawa na hofu, nikiogopa ambacho ningekikuta lakini bado nilitamani kujua.
“Sijisikii vizuri!” nilimgeukia Bianca na kumweleza.
“Nini tena?”
“Nataka kwenda kupumzika, ni vizuri tukaondoka.”
“Genesis, tuondoke mapema kiasi hiki? Kabla wazazi hawajaondoka?”
“Naumwa!” nilitoa kisingizio huku nikigeuza kichwa kuongea na Kelvin, mpambe wangu wa siku hiyo. Mimi na Kelvin tulisoma pamoja Chuo Kikuu cha St. Augustine kilichopo mjini Mwanza, alikuwa rafiki yangu mkubwa na tulishirikiana mambo mengi.
“Vipi tena?” aliniuliza.
“Aisee mwambie MC atangaze kuwa tunaondoka kwenda chumbani kupumzika.”
“Eti shemeji?” Kelvin alimuuliza Bianca.
“Kama yeye ameamua mimi sina kizuizi”
Bila kipingamizi Kelvin alifanya kama alivyoombwa, MC akatangaza juu ya kuondoka kwetu na watu wote wakasimama huku wakishangilia, tukitembea kwa madaha tukiwa tumeshikana mikono kuelekea nje ya ukumbi ambako tuliingia kwenye lifti na kwenda moja kwa moja ghorofa ya tatu, kilipokuwa chumba chetu, Kelvin na mke wake Martina walikuwa pamoja na sisi mpaka ndani ambako bila kuchelewa walituaga na kuondoka.
Kitu cha kwanza nilichofanya ni kwenda kwenye kompyuta yenye mtandao wa Internet, haraka nikaiwasha na kuingia kwenye tovuti ya G-mail nikaandika Bianca10@Gmail.com, kisha kwenye alama ya siri nikaandika neno Hadohado, hiyo ndiyo ilikuwa alama ya siri ya Bianca. Niliyafanya yote hayo akiwa amejilaza kitandani, bila kunisogelea. Nikabonyeza sehemu iliyoandikwa Sign in, muda mfupi tu baadaye sanduku lake la barua pepe likafunguka, iliyokuwa juu kabisa iliandikwa “The truth about innocent Farida Mbaraka”
Maneno yaliyomaanisha ukweli kuhusu Farida Mbaraka asiye na hatia. Moyo wangu ukapiga kwa kasi, jasho likinitoka huku nikisubiri ifunguke, sekunde chache baadaye kila kitu kilikuwa wazi nikaanza kusoma huku nikibubujikwa na machozi, mara kadhaa niligeuza shingo yangu kumwangalia Bianca aliyekuwa amejilaza kitandani, hasira ikazidi kunipanda zaidi na zaidi, nilimwonea Farida huruma kiasi cha kutamani kuua, hakustahili unyama aliotendewa kwa sababu yangu. Sikumchukia Bianca peke yake bali pia familia yangu.
Hatimaye nikafikia uamuzi wa kufanya nilichoona kinafaa, kama Farida alikuwa ameshapigwa risasi sababu ya madawa ya kulevya ambayo hakuyamiliki, basi waliofanya mpango huo nao hawakustahili kuishi hata kama walikuwa ni ndugu zangu na wa kwanza kufa alitakiwa kuwa Bianca! Nikanyanyuka nilipokuwa nimeketi na kutembea mpaka kwenye meza iliyokuwa pembeni, juu yake kulikuwa na sinia lenye chakula, pia vikiwepo visu na uma.
“Hiki kinatosha!” niliwaza wakati nakichukua kisu na kuanza kutembea taratibu kuelekea kitandani alipolala Bianca akiwa hajui kilichoendelea, nikahesabu moja mpaka tatu kisha kushusha mkono kwa kasi kifuani kwake upande wa moyo, damu nyingi ikaruka na kulowanisha nguo zangu, nikakichomoa tena na kukizamisha mara ya pili kisha kuchukua mto na kumgandamiza nao Bianca mdomoni ili kelele zake zisitoke nje, dakika tano baadaye alitulia, tayari alishakufa.
“Mungu wangu nimefanya nini? Kwanini nimeua? Si ningemwacha tu na kutafuta mwanamke mwingine?” niliwaza nikimwangalia, ilikuwa kama vile niliachiwa na shetani aliyekuwa amenifunika na kuuona ukweli wa ubaya nilioutenda.
Lakini kwanini nimeua siku ya harusi yangu? Nimesoma nini kwenye barua pepe hii?