HaMachiach
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 3,448
- 6,211
Ni mda mrefu hapa jf nilitamani kuweka elimu kidogo kuhusu kifo kutokana na machapisho mbali mbali yaliyo wekwa hapa na maana mbali mbali ambazo members wamekuwa wakitoa kuhusu kifo. Kabla ya yote kujua kifo ninini lazima kwanza tujue mtu ni nani.
Mtu ni roho yenye nafsi inayo kaa ndani ya nyumba na nyumba hiyo inaitwa mwili, mtu sio mwili wala moyo wala akili ndio maana mtu angekuwa moyo usinge sikia mtu akisema moyo wangu unauma hii miili tuliyo nayo ndiyo nyumba zetu sasa turudi kwenye kifo
Kifo ni utengano kati ya mwili na roho na sivinginevyo. roho yako inapotoka ndani ya mwili hapo kwa taratibu za kibinadamu unahesabika umekufa na roho ikirudi ndani ya mwili hapo tunasema umefufuka toka kwa wafu pia tambua hili kuwa mtu aliyekufa huwa hajui kama amekufa
Kufa nikuhamisho kutoka ulimwengu wa mwili kwenda ulimwengu wa roho, roho inahama nisawa na kuhama kutoka vingunguti ukahamia masaki ndiyo hivyo roho inahama kwenye mwili inaingia ulimwengu usio onekana na macho.
Je mtu akifa nini kinatokea nihivi kutoka ulimwengu wa mwili kwenda ulimwengu wa roho umbali wake ni zero distance hivyo kitendo cha roho kuacha mwili sekunde hiyohiyo anajiona sehemu nyingine anakilakitu kinachomfanya aitwe mtu ...... itaendelea